Ajali ya Meli: "Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu shakani!" - Zitto Kabwe

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,615
CHANZO: http://www.fikrapevu.com/habari/zitto-taifa-msibani-umoja-wetu-na-utu-wetu-shakani

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu 2,000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba.

Habari hazikuwa za uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii. Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokuwa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake wakikatika viuno na hata ngoma za asili. ‘Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha kusikitishwa kwake na kituo hiki.

Hadi jioni tulikuwa tumepata taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570 hivi walikuwa wameokolewa. Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla alipona, aliokolewa. Nilimwambia Leyla atapona na kurudi shuleni.

Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa. Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana, ilitulia na kuonyesha uongozi dhabiti katika juhudi za uokoaji.

msiba-zanzibar.jpg


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta. Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao Kampuni ya simu za mkononi ya VodaCom ambao miongoni mwa waliofariki wamo wateja wa VodaCom, waliendelea na shindano hili. Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu. Nimeamua kutotumia simu yangu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya abiria 800! Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12. Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria. Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama hii.

Mwenyezimungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu wa haraka majeruhi wetu.

Makala haya yameandikwa na Mhe. Zitto Z. Kabwe (kama raia) na kusambazwa kwa vyombo vya habari
 

kanyanga

Senior Member
Jul 15, 2011
110
68
Huu ujinga wa kuwafanya wa TZ kama NDONDOCHA kwa viongozi wanaoongoza Taasisi za Serikali kutokujali kile kinachowatokea Wananchi kwa kuwa tu wanajua hakuna anayeweza kuwawajibisha ndiyo Jadi. Hawa TBC1 si kwamba ni watu wa ajabu bali walichokifanya ni KITUKO CHA MWAKA.

Roho za Watanzania wenzetu zidi ya 200 zimetokomea kwa uzembe wa Waapuzi wachache waliopewa Dhamana ya kuangalia hicho kilichostahili kuangaliwa kabla Meli haijang'oa nanga Bandarini Malindi, lakini kwa hali ya kushangaza hadi sasa hujasikia kuna Kiongozi ameachia ngazi, si Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari au Waziri wa Mawasiliano.

Lakini jambo la pili hawa VODA Ubinadamu ZERO wao wanachoona ni bora kushuhudia walimbwende na mikogo ya kuiga kwenye jukwaa, eti kwa kisingizio cha kupata hasara kuliko kuonyesha utu,heshima na huzuni ya pekee kwa janga hili la Taifa.Ni faida kiasi gani wametengeneza tangu walipotia mguu hapa Bongo, hao waliopoteza maisha yao wamechangia kwa kiasi kikubwa sana (kama wateja wao) hata kufikiria na hatimaye kukubali kudhamini Miss TZ.

Mimi nasema hakika MWENYEZI MUNGU hausiki na ujinga uliotokea na kusababisha balaa kubwa kiasi hiki, kwa kuwa yeye huwapenda waja wake na huwaita kwake kwa staha kubwa na kamwe si kwa njia hii ya mateso kwenye maji hadi Roho inaacha Mwili.

Sasa kwa kuwa MUNGU mwenyewe ana Mbinu zake za kuwaadhibu aliowakabidhi jukumu la kuangalia wenzao kwa kupitia Viongozi (kwa kuwa Mamlaka iliyoko Duniani ni mfano wa Mamlaka iliyoko Mbinguni)sasa nami nasali nikimuomba awapige na adhabu kali hapahapa Duniani hao wote waliojifanya hamnazo, kwa kuwa najua kwa hali ya kawaida hakuna hatua itakayochukuliwa toka kwenye mfumo waliouzoea.

MUNGU AWAPUMZISHE NDUGU ZETU WALIOTUACHA NA AWAPE NAFUU MAPEMA WOTE WALIOPATA BAHATI YA KUNUSURIKA.AMEN
 

Tuntu

JF-Expert Member
Jan 28, 2009
211
23
Kwanza naungana na wote waliosikitishwa na kitendo cha TV zetu kutolionyesha tukio hilo kwa ukaribu, sirka ya kufichaficha majanga imepitwa na wakati, TV zetu ziwe macho ya jamii yote katika janga lililotokea.

Lakini, NAPINGANA NA WOTE wanataka Watu woote wa nchi hii eti waache kuendelea na shughuli zao kama kawaida, haiwezekana woote tukae tumepooza tu eti msiba wa kitaifa!! haiwezekana eti TV zote zisionyeshe muziki wala vipindi vingine vya starehe eti kwa sababu tupo kwenye maombolezo!! NO.

Maisha ni lazima yaendelee, kama vile Wafanyakazi wote wa umma watakavyofanya kazi kesho kama kawaida, vivyo vivyo wanaoendesha maisha yao kupitia urembo wanavyopaswa kuendelea na urembo wao kama kawaida, ndivyo wanaopenda muziki wanavyopaswa kuendelea na miziki yao kama kawaida, ndivyo wanaopenda mipira wanavyopaswa kuendelee na mipira yao kama kawaida, bali sie sote kama Taifa bendera itapepea nusu mlingoti kuonyesha maombolezo, na kabla ya urembo, mipira, siasa tutawakumbuka marehemu wetu kwa dakika 1 na kisha tutaendelea na mambo yetu kama kawaida.

Msitake kuturudisha kwenye mambo ya miaka ya 47, kwa kuwa eti Rais kasema maombolezo basi sooote tunyong'onyee. TBC na TV zoote nchini zinastahili kuendeleena na vipindi vyenu kama kawaida, hatuwezi tukalazimishana nchi yetu ilale na kupoooza eti kwa sababu ya msiba wa kitaifa, TBC na TV zoote pigeni miziki kama kawaida, onyesheni mipira mkiweza kama kawaida, wekeni komedi bila shaka LAKINI tupeni pia habari za janga hili.
 

junior05

Senior Member
May 3, 2011
186
46
Asemayo Kabwe Zito ni kweli, hakika baadhi ya wananchi wenzetu wamekosa uzalendo, kamati ya miss Tanzania,wadhamini Vodacom na baadhi ya media hasa TBC1 hakika wametushangaza, yani tumekuwa watu wa kupata updates kutoka CNN,BBC na Aljazeera hili jambo hakika lifanyiwe kazi.
 

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
74
Asemayo Kabwe Zito ni kweli, hakika baadhi ya wananchi wenzetu wamekosa uzalendo, kamati ya miss Tanzania,wadhamini Vodacom na baadhi ya media hasa TBC1 hakika wametushangaza, yani tumekuwa watu wa kupata updates kutoka CNN,BBC na Aljazeera hili jambo hakika lifanyiwe kazi.

Zitto,

Ni bora jambo hilo umelisema wewe mwenyewe, kwa ulivyoandika ni kwamba Vodacom na TBC1 sio tu wameonyesha kutojali bali ni kama usaliti fulani mkubwa sana kwa kutojiunga na watz wengine katika janga/msiba/tukio kama hilo.

Nataka kukuambia kipimo hicho cha usaliti na uchungu unaousikia ndio ambao Watz na CDM wanaopata pindi ambapo CDM kinakuwa katika tukio/janga/ issue fulani halafu wewe unaonyesha kutojali na unaendelea na mambo yako(mifano ipo mingi).

Sio kwamba naunga mkono TBC1 na Vodacom na Miss TZ, ila nakukumbusha kuwa hata wewe unawaumiza-ga sana Watz.............

Na kama ungekuwa umeumia sana usingezima simu ya Vodacom kwa siku moja bali ungejitoa kabisa kutumia mtandao huo- Huo ndio unakuwa msimamo wa mwanasiasa wa kweli ambaye yuko focused and mwenye kumaanisha
 

Ndinani

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
6,878
3,725
Kila kukicha huku bara ikiwa ni pamoja na Kigoma maelfu ya watanganyika wanakufa kwenye ajali za mabasi lakini sijawahi kusikia mnataka watu waache kufanya matamasha yao! The only difference na hili ni kwamba hawa waliokufa kwenye hii ajali walikuwa pamoja.

Life must go on but our government must know that by condoning corruption many lives will be lost and they will be full of blood in their hands. Ujinga wao unawafanya wasitambue uhusiano uliopo kati ya rushwa/ kulindanana na ajali zinazosababisha wananchi kupoteza maisha!
 

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,477
1,692
UJAMAA NA UPEBARI ni vitu viwili tofauti, siasa za ujamaa zainajali UTU.....tumeingia wenyewe kwenye ubepari ambapo faida ina nafasi kubwa kuliko utu twalaumu....VODACOM...si wa kulaumiwa pekee,wadhamini wengine walikuwepo kama ...

NAO WANA NAFASI, WASHIRIKI NYIE MWAITA WALIMBWENDE.....WAPO WALIOTOA GARI LA MILIONI 80.....WHY VODA PEKEE?

TBC.... kama chombo cha habari lazima kikusanye taarifa iliyokamilika na kuirusha hewani,hawawezi kurusha TETESI NA UVUMI....when we judge them we have to be fair enough
 

Kumbakumba

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
222
18
Toka jana nalalamika kuhusu hili, inakuaje tv zetu zinashindwa kutuonyesha nini kinaendelea..hata tu kauli ya rais kuhusu siku 3 za maombolezo, nini maana yake? Sio watanzania wote wanaofahamu maana ya siku tatu za maombolezo...kuna haja ya kufanya overhaul shirika la TBC
 

Babuu blessed

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
1,363
488
TBC wana makosa makubwa sana, vodacom wamo pia lakni na Lundenga anawajibika bila kusahau chama cha magamba walifanya sherehe za uzinduz wa kampeni kwan na wenyew walishindwa kusogeza muda wa uznduzi.
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Mwabweni

Member
Apr 23, 2011
28
3
Zitto umeonyesha uwezo wako wa kuongoza na kusema kweli, umeona baadhi ya watanzania walivyokuwa na fikra ambazo ndio waliokuwa nazo jamaa wa ....................
 

Mwabweni

Member
Apr 23, 2011
28
3
Hali ya kuto kujali mambo ya znz hata baadhi ya wabunge ndio mtazamo zitto ww unaonyesha utofauti na hao
 

kaly

Member
Aug 6, 2011
63
3
Nasikitika sana kwa kuwa kodi yangu pia inaendesha TBC1 ambayo haina faida kwa kweli. Pia nafikiri na uzinduzi wa kampeni kule Igunga wangestop lakin waliendelea. Tuna viongozi wa aina gani jamani?. Tusubiri mamlaka zinazohusika zitachukua uamuzi gan
 

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,701
UJAMAA NA UPEBARI ni vitu viwili tofauti, siasa za ujamaa zainajali UTU.....tumeingia wenyewe kwenye ubepari ambapo faida ina nafasi kubwa kuliko utu twalaumu....VODACOM...si wa kulaumiwa pekee,wadhamini wengine walikuwepo kama ...NAO WANA NAFASI, WASHIRIKI NYIE MWAITA WALIMBWENDE.....WAPO WALIOTOA GARI LA MILIONI 80.....WHY VODA PEKEE?TBC.... kama chombo cha habari lazima kikusanye taarifa iliyokamilika na kuirusha hewani,hawawezi kurusha TETESI NA UVUMI....when we judge them we have to be fair enough

Kila kukicha huku bara ikiwa ni pamoja na Kigoma maelfu ya watanganyika wanakufa kwenye ajali za mabasi lakini sijawahi kusikia mnataka watu waache kufanya matamasha yao! The only difference na hili ni kwamba hawa waliokufa kwenye hii ajali walikuwa pamoja. Life must go on but our government must know that by condoning corruption many lives will be lost and they will be full of blood in their hands. Ujinga wao unawafanya wasitambue uhusiano uliopo kati ya rushwa/ kulindanana na ajali zinazosababisha wananchi kupoteza maisha!

1. Marekani na nchi kubwa za Magharibi kwenye majanga wanaungana na kuwa kitu kimoja. TV, radio na vyombo vingine vya habari husitisha shughuli zote na kuwapa watu habari za kina toka eneo la tukio. (Rejea matukio ya Sept. 11, mauaji ya wanafunzi na walimu Virginia Tech University 2007, n.k.) Ubepari si kisingizio, utu kwanza.

2. Vodacom unaowatetea wana faida gani kwetu watanzania zaidi ya kutukamua na kupata faida ya kibiashara? Kama ni service yao tayari kuna substitutes!!!! Hata kati ya walipa kodi 15 wa juu hawamo na kila siku wanajinadi "Mtandao unaoongoza Tanzania". Wenzeo airtel walao kwa kodi tunawaona.

3. Lilikuwa jukumu la TBC kupeleka waandishi mara moja kwenye site na kuchukulia suala hili kama suala nyeti: Urgent issue. Waandishi wangeweza kuwa wanatoa taarifa za eneo la tukio moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na kuhoji majeruhi na maafisa husika na kurusha kwa watanzania moja kwa moja, na hii si tetesi wala uvumi ndo namna vyombo vya habari vinafanya kazi kwenye matukio kama haya.

4. Nadhani tuwe tayari kukosolewa. By the way mkuu Mahesabu, katika nyakati nyeti kama hizi tuwe sensitive na nini tunapost, kuna machungu mengi so just tuwe sensitive.

5. Watanzania tunaweza kuionesha VODACOM kuwa mteja ni mfalme. Tunaweza kususia huduma yao kama hawajali thamani ya roho za ndugu zetu.
 

Kabembe

JF-Expert Member
Feb 11, 2009
2,551
1,733
While they don't care about us why should we care about them? Mangapi yanawapata Watanganyika wakati wao wakila bata huku wakitoa mineno ya kashfa kwamba watanganyika malaya,walevi na ndo maana wanachoma bar na kususia biashara zetu huko kwao,WHY? Kwanini ya kwao yawe na umuhimu na yakwetu yawe ya kipuuzi na eti kujitakia?
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Mimi nadhani hasira zetu hazijaelekezwa mahali sahihi. Maana walipokufa watu Gongo la Mboto, Mbagala, watoto 21 pale Tabora tena siku ya Idi ni wachache wetu tuliona jambo hili. Miss Tanzania wangeacha kufanya show kungetufanya tujisikie vizuri kidogo lakini kusingeondoa ukweli kuwa tatizo ni serikali na mfumo wake uliopo. Wanaotakiwa kukatyaliwa na kuadhibiwa ni serikali ya CCM na watendaji wake.

Hivi serikali ilitangaza saa ngapi kuwa taifa limeanza maombolezo ya siku tatu maana wengine wamehesabu siku za maombolezo kuanzia leo Jumapili na siyo jana Jumamosi.
 

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,185
2,296
Kwanza naungana na wote waliosikitishwa na kitendo cha TV zetu kutolionyesha tukio hilo kwa ukaribu, sirka ya kufichaficha majanga imepitwa na wakati, TV zetu ziwe macho ya jamii yote katika janga lililotokea.

Lakini, NAPINGANA NA WOTE wanataka Watu woote wa nchi hii eti waache kuendelea na shughuli zao kama kawaida, haiwezekana woote tukae tumepooza tu eti msiba wa kitaifa!! haiwezekana eti TV zote zisionyeshe muziki wala vipindi vingine vya starehe eti kwa sababu tupo kwenye maombolezo!! NO.

Maisha ni lazima yaendelee, kama vile Wafanyakazi wote wa umma watakavyofanya kazi kesho kama kawaida, vivyo vivyo wanaoendesha maisha yao kupitia urembo wanavyopaswa kuendelea na urembo wao kama kawaida, ndivyo wanaopenda muziki wanavyopaswa kuendelea na miziki yao kama kawaida, ndivyo wanaopenda mipira wanavyopaswa kuendelee na mipira yao kama kawaida, bali sie sote kama Taifa bendera itapepea nusu mlingoti kuonyesha maombolezo, na kabla ya urembo, mipira, siasa tutawakumbuka marehemu wetu kwa dakika 1 na kisha tutaendelea na mambo yetu kama kawaida.

Msitake kuturudisha kwenye mambo ya miaka ya 47, kwa kuwa eti Rais kasema maombolezo basi sooote tunyong'onyee. TBC na TV zoote nchini zinastahili kuendeleena na vipindi vyenu kama kawaida, hatuwezi tukalazimishana nchi yetu ilale na kupoooza eti kwa sababu ya msiba wa kitaifa, TBC na TV zoote pigeni miziki kama kawaida, onyesheni mipira mkiweza kama kawaida, wekeni komedi bila shaka LAKINI tupeni pia habari za janga hili.


Kwanza nakudharau na pili kukupuuza kwa kauli za ukatili kwani inaonyesha hujawahi patwa na janga la namna hii bali huwa unasikia tu kwa wenzako. TV za taifa kote duniani hasa katika nchi zinazojali utu huwa zinapiga kambi katika eneo la tukio kuwahabarisha wananchi na hii huwasaidia wale ambao hawajui kuhusu hatima ya ndugu zao kupata habari ya kinachoendelea. Jana nilishangaa kwani taarifa hizi nilizipata Aljazeera na BBC kwani walitoa taarifa na picha kwa kina zaidi kuliko TBC.

Nilipokuja kuangalia TBC1 usiku hawakuwa na kitu cha maana kwani taarifa za aljazeera na BBC zilikuwa na coverage kubwa sana ya hili tukio na walikuwa wanalirudia kila baada ya saa 1 ila TBC ,ITV waliona biashara zao ni muhimu zaidi kuliko ku ripoti tukio hili kubwa ambalo kila Mtanzania alitaka kujua kulikoni.

Utashangaa rais akifungua mkutano TBC1 wanaripoti live na hata bunge linatangazwa kwa masaa 3-4 live je ilikuwaje hawa TBC1 wanaoongozwa kwa kodi zetu kushindwa ku cover hili tukio hata kwa siku moja tu?

Uongozi wa hili shirika la KINAFIKI unatakiwa uangaliwe upya kwani linakuwa la kisiasa zaidi kuliko kuongozwa professionally.
 

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,044
4,954
Msiba ulio tokea nchi jirani kwanini utuharibie ratiba? Mbona kwenye yale mauaji ya Rwanda Tanzania hatukupumzika sasa hawa wa zenji wana tuhusu nini?? Si nayo ni nchi jirani? Na Zitto usijifanye wewe ndo mzarendo sana kushinda hata hao wapemba.

nimesoma haya maelezo yako hunu nikitikisa kichwa...... "meli hiyo ilikuwa inapiga ruti unguja .. pemba .. tanga"
 

BENSON MSEMWA

Member
Aug 10, 2010
30
2
vyombo vyetu vya habari vinakuwa vyombo vya hatari,nilikuwa nikifuatilia vyombo vyetu vya ndani ni aibu mtupu,na kikubwa hata takwimu bado ni za magumashi hadi sasa,ombwe lipo wazi kwa sasa, wenzetu amerika waliifanya dunia nzima wafuatilie lile tukio la sept 11 na hata leo wanakumbuka bado wanataka dunia iungane nao.

Hapa kuna baadhi ya wasakatonge watasema uhuru wa vyombo vya habari na technology,ila mbona mikutano ya kampeni wanaweza kurusha live kwanini hili jambo tena la kitaifa tusielekeze vyombo vyetu vya habari vyote huko kwa manufaa ya taifa letu?

Hakika umoja wetu upo mashakani na mbaya zaidi kuna watu walikuwa na ze comedy huko igunga wanakatika viuno
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

19 Reactions
Reply
Top Bottom