Sioni logic ya kukataa 'ubani' wa Vodacom na kuwalaumu kiasi hicho kwa sababu;
Vodacom hawakuwa wadhamini pekee katika shindano hilo. Kulikua na wadhamini wengine kama Ngorongoro, TANAPA, Star TV, Giraffe Ocean View Hotel na wengineo. Kwa nini lawama ziende kwa Vodacom pekee? Hata kama Vodacom ndio mdhamini mkuu lakini bado sio haki kupewa lawama zote wakati yeye ni mdhamini kama wengine na sio muandaaji???
Vodacom hajachangia lolote katika kutokea kwa maafa yale, uzembe ulianzia serikalini ambako waliruhusu ile boti/meli kutoka bandarini wakati wakijua ilibeba mzigo mkubwa zaidi ya mara 2 ya uwezo wake wa kawaida. Wao hawajaomba msamaha, hawajafukuzwa walipoenda kuangalia wahanga, misaada yao imepokelewa na pia wengine wameenda kujinufaisha kisiasa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.
Lawama nyingine kubwa inabidi ziende serikalini pia kwa sababu walitaarifiwa mapema kabisa meli ilipokua inaanza kuzama, laiti kama wangekua na utaratibu mzuri wa kukabiliana na majanga watu wengi wangeokolewa na vifo vichache sana vingeripotiwa. Kuchelewa kwao kupeleka kikosi cha uokoaji ndio sababu kubwa ya kutokea vifo vingi kiasi kile. Ingekua imetokea maandamano ya kuwalaumu wao huko Z'bar wangeenda muda ule ule tena kwa boti ya kasi ili kwenda kuwalipua kwa mabomu ya machozi na kuwapiga risasi ila kwa sababu ilikua haiwahusu hawakuona umuhimu, kwa kosa hilo ilibidi walaumiwe vikali na kuwajibishwa. Kwa maana hiyo, sioni sababu ya kulaumiwa kwa Vodacom ili hali wasababishaji na waliofanya uzembe wa wazi hawajalaumiwa.
Taarifa zaidi zilisambaa mida ya mchana, ingawa mpaka mida ya jioni wengi walikua hawajajua kilichotokea. Hakukuwa na uwezekano wa kutangaza kuhairishwa kwa tukio lile mida ya jioni wakati watu wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini walikua wamefika kwa ajili ya tukio lile. lakini pia hata maombolezo yalikua bado hayajatangazwa siku ile, hata wewe msomaji hapa nina uhakika 'ulispend' wik end yako kwa furaha as if hakuna kilichotokea.
Hakuna haja ya kuwalaumu Vodacom kwa tukio lile ambalo lilizingatia na kutambua vifo vilivyotokea na walianza tukio lile kwa maombolezo kwa namna ambayo imeelezwa kwenye 'press release' yao. Hata hivyo, tukio lilisheheni watu wengi ambao pia kama ndio hivyo walistahili kulaumiwa kwa kuhudhuria huku wakijua kulikua na maombolezo.
Ninaomba kumalizia kwa kuwatahadharisha; inawezekana kuna watu ambao wanaitumia nafasi hii ya udhamini wa Vodacom kujinufaisha kibiashara. Wanadhamini wanafiki na wazushi ili kupunguza soko la Vodacom kibiashara, wanatumia njia nzuri ila wakati huu sio muafaka kuwafanyia hivyo Wazanzibar na WaTz kwa ujumla katika kipindi hiki cha majonzi. Mshikamano kati yetu sote bila kujali tuliitumia vipi siku ya jumamosi ndo utakaotupitisha salama ila tukianza kulaumiana kwa mtindo huo mwishoni watu wa Zanzibar watatuzuia wabara kwenda kule kisa tuliendelea na kazi siku ambazo wao walikua wanaomboleza. Hivyo, ninawashauri wale wote wanaopandikiza hizo chuki dhidi ya Vodacom waache kwa sababu madhara yake yanweza kuwa makubwa na pia serikali ipokee msaada wa Vodacom kwa maana hauwapunguzii chochote wafiwa ila utawafariji kwa namna moja uau nyingine na pia isijiingize katika malumbano au ugomvi usio na maana.
Huo ni mtizamo wangu, kila mtu anao mtizamo wake.