Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Wakubwa kwa hili la Vodacom kwa kweli halikuwa la busara. Lakini ni aibu kwa Serikali kuifanya vodacom kuwa Bangusilo (Mbuzi wa kafara) kwa uzembe wake yenyewe!!! Yenyewe ndiyo ilikua katika nafasi ya kuzuia janga hilo lisitokee!!! Leo hii PM anasema Serikali itajifunza kutoka katika janga hilo... huo si upuuzi jamani??!!! Kama hawakujifunza kwa lile la MV Bukoba.... mpaka waje kujifunza si tutakua tumekwisha wote??!!

ndugu yangu si unajuwa tena kila siku sisi tunajifunza tu,likitokea lingine tena tutasema bado tunajifunza,sijui ni mpaka lini tutakuwa tayari kupambana na majanga

ama kwa kuwa ni serikali ya umoja wa kitaifa kwa hiyo bado wanajifunza tu kwani wao hawakuwepo serikalini wakati la bukoba latokea

A
kwa kweli waandaaji wa miss tanzania na sponsors walipaswa kuonyesha utu wao. Hata kama wasingeahirisha shindano, wangefanya kitu cha kuonyesha kuwa wameguswa na ajali ile, hata kwa kufanya shindano bila burudani

bepari hana utu, kwake pesa tu. Waliamini watapokelewa kwa kutoa pesa walizoingiza kutokana na shindano hilo.

Smz, hongereni sana kama ni ya kweli, kwani radio ujerumani huwa ni saa saba mchana na saa hizi ni 12:47, nina mashaka na taarifa hiyo.

Kama kweli hiyo imetokea vodacom hawakutendewa haki hata kidogo. tuache jazba. tuna hakika kuwa ukiondoa vodacom hakuna mtanzania aliyekuwa kwwenye starehe, club,hotel gloceries, bars nk? Istoshe katika hili kama tukikubaliana kuwa vodacom wanakosa, je, hakuna wengine wenye makosa?(eg.mmiliki, sumatra,serikali,abilia maaana nao waliona meri imejaa, wafanyakazi wa bandari etc.). list ni ndefu so kama utaratibu wa adhabu ya vodacom utatumika bila double standard niwazi misaada itakataliwa mingi. Naelewa tukio hili limeleta majonzi makubwa na kuwapa wakati mgumu sana wafiwa na sisi watanzania kwa ujumla lakini tusiruhusu huzuni itawale busara. miss tanzania hawakuwa wanashangiria msiba jamani.

vodacom kwa hili hawakupaswa kuweka kitanzini kiasi hicho kwa ajiliya miss au ligi ya bara ... je ni yapi yalitokea baada ya maafa???
1. kulikuwa na uzinduzi wa kampeni igunga chini ya mkapa na alipomaliza alienda znz ,,, je kwa nini awalimpokea bila kujali aliyofanya igunga na ze comedy???
2. ligi kuu bara iliendelea japo nayo mdhamini ni vodacom
3. miss tanzania mdhamini vodacom
4. TBC ambayo tunaamini ni televiseni ya taifa haikutoa hata taarifa nini kinaendelea (je tususie kuangali tbc????)
bado naamini tff na lungenga walikuwa na maamuzi.... je tbc inahukumiwaje???

Siungi mkono hata kidogo, serikali inajikosha!. Nawashauri wazanzibari kwa kutumia uzalendo huuhuu wakatae misaada yote ya SMZ kwani SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kichakavu kikabeba abiria?, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikaongezwa urefu na mafundi mchundo?!, smz ilikuwa wapi hadi chombo kika-overload?!- who's better: a private donor or serikali irresponsible?!. Sitaingamkono hili hatasiku moja-ni kujisafisha @ the expense ya kumkera muhisani. Onyo kwa wazanzibari na watanzania wenzangu- hakuna jema kutoka kwa mafisadi wa madaraka.

Ipo tofauti hapo, smz wazembe wakati voda insensitive ,inhuman ,inmoral

Binafsi si mshabikii wa mambo ya Ulimbwende kama ya Miss so and so! Ila kwa serikali ya Zanzibar kuukataa msaada wa VODACOM kisa walendelea na shughuli za kumtafuta Miss Bongo inamaanisha wanaitambua na kuikubali hiyo shughuli. Vinginevyo wangeweza kuipuuza tu kama ambavyo wamepuuzia Ligi kuu na uzinduzi wa kampeni kule Igunga.Maana kwanza haiwahusu na hawana ushirika wowote ule na mambo ya umiss. Wangekuwa na mshiriki walao tungesema walikuwa na haki ya kugoma. Lakini pia mbona hawalalamikii mabaa ambayo huku Bara yalikuwa wazi na mziku juu? Huu ni unafiki tu kutaka kujiosha kwa serikali ya SMZ.

Wale wote ambao wanahusika na mamlaka ya usafirishaji majini huko Zenj ndo wanapaswa kuwajibishwa na hii ni kuanzia Waziri mwenye dhamana, Uongozi wa Bandari na mmiliki wa hiyo meli! Wote lazima wapate kibano!!!!!

wengi wanaangalia kwa kuhukumu pasi kuliangalia kwa kina

Mkatae na misaada (kama ikitolewa) ya tvz,maana walindelea kupiga taarab,tbc-waliendelea kuonyesha katuni, endeleeni na uzalendo huohuo wa kumtambua adui kwakuwa tu ni mzanzibari mwenzenu na kumkomalia asiyehusika.
Hatudanganyiki, bora mtulie mnatuzidisha hasira kwa kujifanya kuhamishia hasira zetu kwingine. Mmetumia pesa nyingi sana kuosha nyota yenu kupitia vyombo vya habari. Mnaingia hasara tu na kuzidisha hasira za wananchi. Vodacom is inhuman

Hongera SMZ, Hongera Zanzibar na Hongera sana waZnz kwa msimamo wenu.

Hakika hio msaada ulikuwa ni kejeli kwenu kwani wao hawakuona kabisa umuhimu wa majonzi yenu na taifa kijumla. Kwao wao ilikuwa bora ni kuendelea na burdani zao na kukwepa gharama.

Mimi nashauri Znz na SMZ ni vizuri mkaenda mbali zaidi kwa kuifungia kabisa Vodacom isi operate Znz ili kutoa fundisho kwa wengine wenye dharau na kibri kama Hao.

Nazidi kujiuliza kama maafa yale angetokea ukerewe au hata Mafia, wangeendelea na miss Tz?
Ninakuhakikishia hata kama ingetokea popote pale wangeliendelea, kwani kama walivyosema wengine hapo juu, Vodacom ni wadhamini tu. Ludenga kama walafi wote, hata kama angekufa mzee wake, angewakilisha mtu mazikoni au angemaliza U-miss kwanza ndio siku ya pili mazishi. Wasokuwa na haya wana mji wao!

hatimae kilio cha wengi kimesikika kwani ule msaada uliotolewa na vodacom kwa wale wahanga wa kuzama kwa meli zanzibar umekataliwa

kwani pale watu wa jamhuri ya muungano wakilia na maafa yaliyo wakuta hawa wenzetu kutoka sa walikuwa wakisheherekea miss tanzania

hongera serikali ya zanzibar

habari hii ni kutoka redio ujerumani kiswahili

niliweka thread wazi kama wazanzibar mtapokea mtakuwa mmejizaalilisha sana awakutahamini watu wakiwa aherawaje kuthamini kutoa michango kisa rais kaelekea huko shame on them

Siungi mkono hata kidogo, serikali inajikosha!. Nawashauri wazanzibari kwa kutumia uzalendo huuhuu wakatae misaada yote ya SMZ kwani SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kichakavu kikabeba abiria?, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikaongezwa urefu na mafundi mchundo?!, smz ilikuwa wapi hadi chombo kika-overload?!- who's better: a private donor or serikali irresponsible?!. Sitaingamkono hili hatasiku moja-ni kujisafisha @ the expense ya kumkera muhisani. Onyo kwa wazanzibari na watanzania wenzangu- hakuna jema kutoka kwa mafisadi wa madaraka.

Biravo, bravo Gama! watu makini, wanaofikiria, wapembuzi yakinifu, wasiokurupuka ndio wanaweza kuliangalia janga hili kwa jicho ambalo wewe umeliangalia. Kuna watu wanajaribu kukwepa lawama au uwajibishwaji, hivyo kwa namna moja ama nyingine wanajaribu kuhamisha hisia za watu kwa kampuni binafsi ya Vodacom kwa kitendo kile ambacho imekifanya, tunasahau kuwa wao sio chanzo cha ajali ile pia wao ni wafanya biashara, na ikumbukwe kwamba Vodacom ina mchango mkubwa sana katika pato la taifa hili na katika kusaidia kutokomeza matatizo mbalimbali nchini.

Nisingependa kurudia uliyosema lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanasukumwa na ushabiki katika suala hili. Wenye akili wamejaribu kuibua hoja kuwa wakati ajali hii imetokea CCM walikuwa wanazindua kampeni Igunga, Tabora je na misaada ya chama hiki ikataliwe. Vodacom isihukumiwe kwa kile ilichotenda kwa kukataa kupokea misaada yake badala yake ishirikishwe katika kulimaliza suala hili.

Gama amezungumza ukweli ambao unafichwa hivi sasa, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kichakavu kikabeba abiria?, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikaongezwa urefu na mafundi mchundo?!, smz ilikuwa wapi hadi chombo kika-overload, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikabeba watu zaidi ya idadi ya kawaida(mmoja wa walionusurika katika ajali ile wakati akihojiwa na kipindi kimoja cha redio jana jioni aliweka wazi kuwa Meli ilibeba zaidi ya watu 2000). Haya ndio maswali yanayopaswa kujibiwa kwa sasa.

Lawama kwa Vodacoma haina tija isipokuwa siasa na kukwepa mzigo wa lawama, viongozi wa serikali wawajibishwe ikiwemo waziri husika, Vodacom waachwe watoe misaada yao kama ambavyo imekuwa ikifanya.

Mkuu kaduguda, hivi huko zanzibar bar, mahoteli na madanguro yalifungwa?!, nauliza tu.
Binafsi si mshabikii wa mambo ya Ulimbwende kama ya Miss so and so! Ila kwa serikali ya Zanzibar kuukataa msaada wa VODACOM kisa walendelea na shughuli za kumtafuta Miss Bongo inamaanisha wanaitambua na kuikubali hiyo shughuli. Vinginevyo wangeweza kuipuuza tu kama ambavyo wamepuuzia Ligi kuu na uzinduzi wa kampeni kule Igunga.Maana kwanza haiwahusu na hawana ushirika wowote ule na mambo ya umiss. Wangekuwa na mshiriki walao tungesema walikuwa na haki ya kugoma. Lakini pia mbona hawalalamikii mabaa ambayo huku Bara yalikuwa wazi na mziku juu? Huu ni unafiki tu kutaka kujiosha kwa serikali ya SMZ.

Wale wote ambao wanahusika na mamlaka ya usafirishaji majini huko Zenj ndo wanapaswa kuwajibishwa na hii ni kuanzia Waziri mwenye dhamana, Uongozi wa Bandari na mmiliki wa hiyo meli! Wote lazima wapate kibano!!!!!

Jaman vodacom walikuwa kazin nan kasema walikuwa wanasherehekea..watu walikuwa kazin eti kwa sababu kuna msiba watu wasiende kazin miss tanzania ni kaz halal kama kaz nyingine emu achen kudharau kaz za watu.SMZ waache unafki wakat bar na makanisa yanachomwa walikuwa kmya

ONE OF MWAMVITA BEST FRIENDs on her FB WALL-''Really watanzania some of us are soooo freaking stupid......Gosh, Mpaka now huko ZNZ hawajajua hata who was the owner of ile meli iliyozama ila wamekazania tu kulaumu why miss tz took place. instead of kuelekeza hasira on why meli yenye uwezo wa kubeba watu 600 ilibeba watu 1000 wao wameng'ang'ana on who was having a jolly good time that day,how the **** is that going to make things better? meli imeondoka bandarini''inaelemea one side kwa mizigo mingi,why not deal na watu waliofanya uzembe.instead stupid politicians wa chadema wamepata opportunity ya ku attack CCM, and waznz wamepata opportunity ya ku question muungano na bara.how unfair is that? DEAL WITH THE REAL ISSUES JAMANI,,MNGEPIGIA KELELE PUBLICLY NA KUDEMAND KUJUA MMILIKI WA MELI ILE MTAISAIDIA ZAIDI ZNZ na sio kuuliza why miss tz went down.septembe . r 11th ilitokea marekani na oscars hazikuwa cancelled ila watz bila majungu hamuoni raha.stupid... ANAENDELEA KUTOA MSISITIZO-''KAMA UNA ANY OPINION YA KISHAMBA YA KUBLAME VODACOM OR MISS TZ DONT COMMENT ON MY STATUS, IF U DONT AGREE WITH WHAT I SAID FEEL FREE TO REMOVE ME FROM YOUR FRIENDS'S LIST....''SASA SIJUI MTU KAMA HUYU ATAMSHAURI NINI MWAMVITA KAMA UUNGWANA KWAKE NI KAULI CHAFU.

Huyo dada ndo wale wale,Mpuuzi! Hebu muanike hapa tumfundishe adabu akome! Kuhoji walichofanya voda na hao Lino hakutuzuii kuhoji watu wote wawajibike.angekuwa muungwana angeponda wote wahusika wa meli,serikali na wasio na uzalendo wote kwa kuendesha onyesho tena live dunia nzima ikituhurumia sisi tunaserebuka live! Tutahoji yote haponi mtu tena ngoja kanipa hasira huyu sista du.

Jamani tuwachieni Wazanzibar waamue mambo yao wenyewe msiba ni wa kwao, mbona sisi wakati Mv. Bukoba, ilipozama hawakutuingilia wala kutulaumu mpaka tukaitoboa Meli ili kutoa watu hatimae ikazama kabisa kwa ujinga wetu. Kwanza kwenye hiyo Meli.
Hakuna Wachagga, hakuna Wakinga, hakuna Wahaya, hakuna Wakweree, hakuna Wakurya, waacheni kulalamika na nyie subiri mabasi yapate ajali ndio mlalamike.

Vodacom ni wapuuzi sana tu

Back
Top Bottom