Kadhia ya VODACOM na Utaifa wetu: LUNDENGA Kufungwa Kengele Rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kadhia ya VODACOM na Utaifa wetu: LUNDENGA Kufungwa Kengele Rasmi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mohammed Shossi, Sep 13, 2011.

 1. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #1
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Jana kwenye mtandao wa kijamii niliona jinsi watu walivyokuwa kiishambulia kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania baada ya kuendesha sherehe za Miss Tanzania 2011 kwakweli hali ilikuwa mbaya zaidi kwa dada yetu Mwamvita Makamba lakini baadae nilifarijika kuona Vodacom wametoa namba za kuchangia kwa walioadhirika na maafa ya Zanzibar. Naleta hoja mbele yenu je Vodacom wamefanya sawa kuchangisha pesa baada ya kilichojiri usiku wa Jumamosi?

  Binafsi nadhani bado kuna kitu kina miss maana tangazo lao linaeleza unatuma msg unakatwa shs 1000 na utume pesa kwa njia ya m pesa kuanzia shs 1000 ina maana hizi pesa ni sisi wenye majonzi ndio tunaoweza kuzituma ikisha zikawakilishwa kwa walioadhirika na janga lile na sio wao kama wao? Au pengine nitakuwa sijalielewa vizuri tangazo lilio kwenye tweeter na nitakuwa radhi kusahihishwa.

  Naomba niwakilishe na mtoe mawazo yenu.

  Shukran.
   

  Attached Files:

 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ukosawa kabisa mkuu, kuwa wanao toa pesa hiyo siyo voda ila ni watumiaji wa voda watakao amua kuchangia...
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Nadhani hii arrangemnt yao haijakaa sawa kabisa mkuu na ni kuzidi kujipalilia makaa kwa walioshikwa na hasira juu ya mwenendo wao hasa ukizingatia tukio la usiku wa jumamosi ambapo hadi watalii (wasiokuwa watanzania/wala wafrika) walionekana wenye kuchoka/taabani kuhudumia walioadhirika na janga lile lakini wao kupitia Lino Agency walikuwa kwenye full shangwe.
   

  Attached Files:

 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  very true mkuu

  chochote kitakachopatikana si cha VODACOM bali cha watanzania wote.... in short wao wamekubali kuwa conduit tu

  but they could spend 100M for vichupi context... aisee
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hivi watu wakiacha kuchangia/kutoa misaada kwa sababu ya Vodacom, tutakuwa tuanmkomoa nani? Kama umeguswa toa tu mchango wako si lazima upitie Vodacom.
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kadhia ya VODACOM na Utaifa wetu: LUNDENDA Kufungwa Kengele Rasmi


  Kadhia hii ilianza kama mchezo wa kuigiza na sasa imezigubika siasa za Nchi kwa kutoka katika sura yake ya wali na kuwahusisha wanasiasa wanaoelezwa kuwa na mkono wa kibiashara katika Kampuni hii.

  Binafsi nisingependelea sana suala hili kuhusishwa na wamiliki au wanahisa ambao kwa namna moja ushauri na maamuzi yao yatahitajika sasa kutanzua kadhia hii iliyopikwa na watendaji wazembe ambao wao wamewapa dhamana kusimamia mradi huu.

  Tatizo kubwa kwa watendaji wengi wa Kitanzania ni udhaifu katika maamuzi ya haraka na mipango ya dharura katika matukio muhimu kwani kila siku huwa tunapanga bila kuwa na mpango wa kando (sio ule wa Kenya katika kampeni za Ukimwi) kuweka hadhari kama jambo hili litajitokeza nini mbadala wake kwa kuwa tunaamini katika nadharia kuliko nguvu za kimaumbile (Nature – ambayo ni unpredictable)

  Kwa Kampuni kubwa kama VODACOM ambayo inajiendesha kibishara kwa kutegemea mapato yake kwa aslimia 100 kutoka kwa individual consumer in aggressive competitive market arena walipaswa kuwa makini sana na kujihusisha na kadhia yoyote ambayo ingechafua image yao katika jamii.Kutokana na muendelezo wa mijadala mbalimbali juu ya hujuma hii ya VODACOM ambayo sauti ya kwanza ilipazwa kutoka hapa JF, kila mtanzania ana mtazamo wake.

  Wapo wanaoona kabisa Kampuni hii imefanya kitendo si cha kiungwana na wengine wanaamini hakuna sababu yoyote ya kuwalaumu VODACOM.
  Kwa mchambuzi mzuri na mwenye taaluma ya MASOKO hasa Marketing of service, VODACOM hana pakuweka uso wake kwa kadhia hii. Hili ni doa kubwa sana kwao.

  Nikiwa napanda Boti kurudi Unguja asubuhi ya leo, nimearifiwa na chanzo changu muhimu kuwa umeandaliwa mpango wa sasa ni kuhakikisha LINO agency International wanajitokeza hadharani na kuelezea mkasa mzima kwa lengo la kubainisha Tatizo na kwa nini shindano la kumska mnyange wa Vodacom lilifanyika katikati ya Simanzi kubwa iliyoligubika Taifa.

  Huu ni usanii na mchezo mbaya ambao bado si uungwana.
  Siku zote waswahili wanasema Muungwana ni Vitendo, VODACOM simameni mbele ya watanzania na muondoe kadhia hii, kwani wanaofanya kazi hapo ni binadamu na waliokosea ni binadamu. Wahusika wawajibike kwa mustakbali wa Kampuni na majaaliwa yake katika ushindani wa soko.

  (UPDATES TO FOLLOW............Kutoka PRESS Conference hiyo)

  Sote tunafahamu nyie kama wadhamini wakuu mngeamua kusitisha shughuli hiyo ambayo mnaifadhili kwa zaidi ya asilimia 90, LINO hangekuwa na ujanja wala hadithi yoyote mpya zaidi ya kukubali maamuzi yenu, na huu ndio msingi unaowatia katika dhambi hii. Busara na maamzui magumu yakitumika hapa itaonyesha uzalendo na uwajibikaji wa dhati.


  ADIOS
   
 7. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #7
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kule kwenye ile boycott ya say no to voda kwenye fb wamewahimiza wazenji wanaoishi UK kuishitaki Voda kwa brand name vodaphone kwa kitendo chao. Hapo kwenye red naunga na wewe yaani mie binafsi imenitia kinyaa. Wasema Voda ni sponser tu walaumiwe Lino who knows Lino? kuna watanzania wangapi wanaijua Lono na wangapi wanaoijua Vodacom?
   
 8. kade030

  kade030 Member

  #8
  Sep 13, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wa kulaumiwa ni Lino agency wala c vodacom.
  Lakini dhambi hii ni kubwa mno..!
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  Sep 13, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Kibiashara zaidi.

  Watu walishalipia Ukumbi.

  watu walishakodi makorombwezo yote.

  Mengine yote ni Blah! blah! na siasa tu.
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapa ishu ni fedha ya nani imetumika kulipia?
   
 11. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #11
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Una maana sio lazima uchangie kupitia Vodacom uchangie kama wewe.
   
 12. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #12
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wangeshauriana vizuri wote wawili wangeweza kuziepusha kampuni zao na kadhia hii. Tatizo walitia pamba masikioni hata siku ile ya Tukio walitumia muda mwingi kushabikia miaka 50 ya uhuru na wakasahau kama kuna watu wamepoteza Maisha huko Zanzibar.

  Wenzetu katika kadhia kama hizo ambazo huwezi kuahirisha tukio wangevaa vitambaa vyeusi mikononi wakati wanyange wanapita ingewagusa sana watanzania.

  Na walikuwa na uwezo wa kutuma special message LIVE wakati tukio linaendelea kuonyesha kuguswa kwao.
   
 13. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #13
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu unafahamu kwamba contribution yao mmeikataa, sasa nadhani walichoamua ni kuwawekea platform watanzania wengine waweze kushiriki kupitia kwao, kwani si watu wote wenye uwezo wa kufikisha rambi rambi zao kwa wahusika.

  Nadhani watatumia mwanya huo wa wateja wao watakaokuwa wamechangia na wao wataongezea na kile mlichokikataa na kuwakabidhi wahusika kwa kuwa utakuwa ni mchango wa watanzania wote na si vodacom pekee ambao wametakiwa kuomba radhi kwanza kabla ya kukabidhi mchango wao!!
   
 14. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #14
  Sep 13, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa vodacom wamekosea jamani. Hata hao LINO pia wamekosea kabisa. Unaju hata kama vodacom walitishia kutowapa udhamini basi LINO wao wangeonyesha msimamo wao. Hapa inabidi tuchukue hatua zaidi ikiwa ni pamoja na kutomtambua mshindi wa hilo shindano.

  Mimi nitashangaa kabisa eti huyo mlimbwende anajihusisha katika shughuli za kusaidia jamii. Ni jamii ipi hasa anilenga wakati tangu mwanzo hakuwa na huruma kama hiyo? Huyu pia yapaswa tumkatae kwa sauti kuu, tumwambie hatukutambui na pia hatutaki misaada yako. Iweje utukumbuke leo wakati ulitudharau siku tulipopatwa na majonzi makuu ya taifa letu?

  Hapa ili vodacom wajisafishe kwa jamii ni lazima wafanye haya mambo yafuatayo
  1.Kwanza inatakiwa kuwafukuza kazi wale wahusika wa moja kwa moja na jamii(Mkurugenzi wa mahusiano ya jamii, hapa ni Mwamvita Makamba), pia meneja mahusiano bwana Salumu mwalimu.

  2.Wasitishe huduma kwa huyu mshindi wa miss Tanzania kwa kipindi chake choote atakachokuwepo katika taji lake.
  3.Wafute udhamini kwa mashindano ya miss Tanzania kuanzia mwakani.
  4.Waombe radhi hadharani kwa kitendo chao cha kukosa utu.
  5.Wajitathimini upya mahusiano yao na jamiii kwa sasa na penye tatizo walishughulikie mara moja. Hapa waje na sura mpya kabisa kwenye safu ya uongozi na si kuwaona tena Mwamvita Makamba na Salum Mwalimu.

  Vodacom chukueni hatua vinginevyo mtaangamia kibiashara. Ninyi ni kampuni achaneni na mambo ya kuwabeba watu waliosababisha muwe katika hili zogo.
   
 15. P

  Paul S.S Verified User

  #15
  Sep 13, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Katika hii dunia ya utandawazi kuna mambo mengi yanaendele inabidi utulie kutafakari kabla ya kutoa hukumu.
   
 16. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180

  Mimi naona idara ya masoko ya Vodacom inahitaji a kiss of life ili itengamae. Hapo kabla kulikuwa na kijana alikuwa anaiongoza hiyo idara na kuyapeleka mambo sawa, lakini mmmmmhhhh bada ya kuondoka (kwenda Serengeti??? Chibuku???? TBL??? Konyagi???); mambo naona hayaendi sawa. Vodacom jipangeni upya vizuri.
   
 17. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Jamani hebu tutumie busara japo kidogo tu. Hivi kosa hasa la Vodacom ni nini? Wao ni wadhamini tu wa mashindano ni si waendeshaji. Kinachoonekana kuleteleza hizi chokonoachokonoa ni kwamba tu mashindano wanayoyadhamini watu wengi hawayakubali kwa sababu tu za kitamaduni au kimazoea. Vodacom hao hao wanadhamini ligi kuu ambayo siku hiyo hiyo ya tukio kuna mechi ilichezwa kati ya Azam na timu nyingine. Mbona hilo halitajwi? Au kwa nini msisusie bidhaa za Bakhressa au kusafiri na boti zake kwa vile timu yake ya Azam ilicheza mechi wakati kuna msiba? Jaribuni kuwa balanced jamani.
  Kama kuna lawama zozote ziende kwa kampuni ya Lundenga sababu wao ndiyo wenye kibali cha kufanya mashindano yale. Ni kutokana na kuwa na ujuzi finyu wa marketing ndiyo maana kwenye haya mashindano inajulikana Vodacom peke yake badala ya kampuni ya Lino ya Lundenga ndiyo wanaohodhi Miss Tanzania.
  Isitoshe wapo wadhamini wengine kadhaa wakiwemo Redd's na CFAO Motors, mbona hatusikii mkizungumzia kadhia inayowahusu na hawa?
  Hii ni propaganda ya kukwepesha lawama kwa utendaji wa kipumbavu wa serikali ya Zanzibar na rushwa zao na badala yake wanaibebesha Vodacom zogo lisilowahusu. SMZ kwanza ieleze kwa nini ajali imetokea wakati vyombo vyote vya uangalizi vipo halafu kama kuna wengine wa kulaumiwa ijulikane. Huwezi kulazimisha watu wavuruge ratiba zao sababu ya uzembe wa wajinga wengine.
  Tuwe makini na kujiingiza kwenye mchezo wa lawama zisizo na kichwa wala miguu. Matatizo yanatakiwa yatatuliwe kwenye chanzo. Katika mkasa huu chanzo ni SMZ na si kampuni binafsi.
   
 18. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa jamaa walichemka, LINO pamoja na VODACOM, tatizo wapo kimaslahi zaidi, wanashindwa kuelewa kuwa wanatumikia jamii, na hawakuangalia madhara yatakayofuata.
  Sio rahisi kufikiria, lakini katika watanzania wenye msimamo thabiti ni pamoja na watu wa visiwani, wanauwezo hata wa kuisusia mtandao wa vodacom, Hapo ndio mtaona madhara ya kiburi chenu.
  Si kama nachochea bali ndo hali halisi ilivyo.
   
 19. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Angeitwa Miss REDD'S, CFAO MOTORS and VODACOM Tanzania. Mkuu VODACOM ndio main sponsor ambaye anabrand show hawa wengine ni cooperate sponsors amabo hawana mandate yoyote nje ya VODACOM this time walikuwepo pia TANAPA na wengine kibao.

  Hufuti Kosa lako kwa kosa la mwingine. Kama unahisi na hao wengine pia wanahusika justfy huo ulazima na si kutetea Kampuni ambayo sie tunaona walikosea kwa namna moja.

  Alizungumza E.L tatizo inapofika katika maamuzi magumu watanzania tunapaka poda sana.
   
 20. M

  Maganiko Senior Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poor PR Management,
  Poor CSR,
  Poor Marketing.
  Vodacom ikiwa ni household name in telecom in Tanzania walipaswa kupima hali hii tangu mwanzo. Huko majuu kwenyewe marketing, PR & CSR inakuwa sensitive sana na society ambayo ndo consumers. Vyovyote iwavyo VTL wamechemsha big time na kuwatetea ni kutowapa nafasi ya kujua walipokosea. Huko majuu hata big time investors wako sensitive sana na aina za investments ambazo zinaweza kusababisha negative social attitudes and ndo sababu PR-CSR pamoja na marketing ni veitengo muhimu.

  VTL this time are caught with pants down.
   
Loading...