Yes SMZ, Yes Naunga mkono.. nawatia hamasa zaidi.. Watu wamezama majini.. ndugu zetu, marafiki zetu tuliowajali.. halafu nani asiye na utu anayetetea hili.. unaweza kutetea kwa kuwa hayajakufika, yakikufika utajua uchungu wake.. Imagine mojawapo wa hao washindani wa miss tz, nduguye angepotea kwenye ajali, au ndugu wa mmojawapo wa majaji wa shindano au.. unadhani shindano lingefana.. HAWANA UTU JAMANI..
MBAYA ZAIDI.. Chama tawala (usiumie, msinizibe mdomo wacha nseme) Ikiwa Bado shughuli za uokozi zinaendelea, Watu wako kazini wakiokoa ndugu zetu, mama zetu na dada zetu, walioshikiliwa na mauti ya maji (mbaya), watoto wasiojua lolote wanamezwa na ukatili wa maji, wanawake wasiojua kuogelea maskini ya mungu maji yanawazamisha kwa kifo cha uchungu na kilio, wanapiga kelele ila maji kwa ukatili yanaingia mdomoni na kuwanyamanzisha milele, wakati huo huo shirika la uokozi la Afrika kusini likikimbia kuingia ichini kuongeza nguvu ya kuwaokoa ndugu zetu hawa.. cha ajabu CCM Inazindua kampeni zake IGUNGA.. jumamosi hiyo-hiyo (Kitendo hicho unakiita UTU!!).. tena chini ya Aliyekuwa Rais wa JMT.. aibu.. sipati picha wakati SA rescue team inaingia nchini kwa helcopter, wanachungulia chini TZ, wanaona wanachi wamekusanyika, wanatamani kushuka wakidhani wamefika kwenye tukio, wanashangaa wanaona mauno ya ze comedy.. wakitupa macho kule mitaarabu ya TOT inamiminika.. nadhani watakuwa wamejiulia is this the right country or we were missleaded!!?? SMZ imulike tochi yake na huko CCM nao wapate BAN vilevile..
Upanga wa SMZ usiishie hapo, Maalim Seif, Mtu wa Pemba, Katibu Mkuu wa CUF, mtu tunayejua yuko makini.. wakati taifa bado liko kwenye maombolezo mazito.. jamaa anaorganize ufunguzi wa kampeni IGUNGA (No excuse.. ni katibu mkuu.. ndo mtendaji wa shughuli zote za chama hata kama siye yeye aliyeorganize ila hajitoi kwa hili, ni ofisi yake.. ni yeye).. asee!! hii sasa ni zaidi, Wapemba CUF mliyokubali kuifia zat uchaguzi, CUF kipenzi chenu !! ai huku watu wanapanda Punda, wanazindua kampeni.. aisee Mie sina tafsiri ya jambo hili.. Please please.. Inauma.. tafadhali SMZ BAN kitu hii..
Ni kweli kwamba msaada wa pesa unawasaidia wahanga, ila msaada kwa mtu anayekung'onga ni msiba mwingine!!