Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Au labda wangehairısha shndano lile wangepata hasara.
 
Jamani tusikimbie kuangalia matawi badala ya mizizi ya tatizo. Kwa nini tusiwabane wahusika wanaoruhusu meli na vifaa vya usafiri vibovu vitumike? Kama kila mtu angekuwa mahala pake pa kazi tusingekuwa na hizi thread za kuwalaumu voda.
Na kama tukiiachia hii hali ya kuwakomalia sponsors, tujiandae janga lingine litakuja na litaondoa maisha ya wengi, na kipindi hicho tutawabana sponsors tena!
Hivi hawa SUMATRA uwezo wao ni kukimbizana na daladala tu? Maana huonekana wanafanya kazi pale ajali inapokuwa imetokea na siyo intelijensi kabisa.
 
Naungana na ghost, ni kweli kabisa invisible ameikosea haki hii mada ya Kuzama kwa meli. Kwani hata mimi nimeona akizitia kapuni. Mkuu unauwa democracy ya JF. Nomba uwe makini vinginevyo watu watakuchukia kwa staili uliokuja nayo ya kuminya democracy ya JF.
 
Suala la TBC litachukuliwa na Serikali ya JMT kwani pasi na shaka Rais wa JMT alitangaza pia maombolezo hayo na hata kukatisha safari yake ya ughaibuni. Hao watakuwa wamedharau mamlaka sio tu za SMZ bali pia hata za JMT na hivyo wanastahikhi kuchukuliwa hatua na JMT.

Vodacom kama taasisi binafsi lazima ichukuliwe hatua na JMT ambako imesajiliwa lakini vile vile SMZ lazima wawa adhibu sio tu kwa kukataa misaada yao lakini pia kuwazuilia wasifanye shughuli zao ndani ya mamlaka ya SMZ kama fundisho kwao kwa kudharau maisha ya watu na kundekeza starehe.

Mkuu Barubaru,
Kuna mengi sana ambayo yamegharimu maisha ya wananchi na serikali imeyapuuza tu! Kama kila mtu angewajibika hapa tusingeomboleza.
Kuahirisha lile shindano kusingeweza kurejesha maisha ya ndugu zetu.
Yangu macho na masikio, angalia kama kuna mtu atawajibishwa pale TBC, wote wataendelea tu kupeta.
Tuwakabe wanaohusika na ukaguzi wa hivi vyombo, wanafanya kazi ajali ikitokea tuu?
 
Suala la TBC litachukuliwa na Serikali ya JMT kwani pasi na shaka Rais wa JMT alitangaza pia maombolezo hayo na hata kukatisha safari yake ya ughaibuni. Hao watakuwa wamedharau mamlaka sio tu za SMZ bali pia hata za JMT na hivyo wanastahikhi kuchukuliwa hatua na JMT.

Vodacom kama taasisi binafsi lazima ichukuliwe hatua na JMT ambako imesajiliwa lakini vile vile SMZ lazima wawa adhibu sio tu kwa kukataa misaada yao lakini pia kuwazuilia wasifanye shughuli zao ndani ya mamlaka ya SMZ kama fundisho kwao kwa kudharau maisha ya watu na kundekeza starehe.

Think twice.
 
V
Inasikitisha sana katika hili suala jinsi ambavyo VTL walivyochemsha katika suala hili. Watendaji wao hasa wa masoko wamesaahu suala la 'corporate social responsibility' na hasa katika janga hili la kitaifa. Naona picha za mama masoko akijirusha kuelekea MC zimeondolewa kule 'kata kona'

Vodacom wameonesha corporate social responsibility kwa kutaka kutoa ubani na serikali mbumbumbu imekataa kupokea. Ulitaka wafanye nini zaidi ya hapo? Yale mashindano wao ni wadhamini tu na sio waandaaji ambao nao hawakuwa na makosa yoyote, sio kiutamaduni wala kisheria. Msitake kukuza saaaaana hii issue ati kwa sababu kuna watu wamekufa basi wengine waache mambo yao. Kama mnaona wamekosea, muwafutie leseni na sio kujaza upuuzi wa maneno maneno. (mimi sio mdau wa voda)
 
KANI VODAKOM NDIO WAANDAAJI?? WAO NI WADHAMINI TU NA HAWAKUA WADHAMINI PEKEE IWEJE LAWAMA WAPEWE WAO?? na vipi kuhusu CCM KUZINDUA KAMPENI IGUNGA NAO WAMESUSIWA AU??
 
KANI VODAKOM NDIO WAANDAAJI?? WAO NI WADHAMINI TU NA HAWAKUA WADHAMINI PEKEE IWEJE LAWAMA WAPEWE WAO?? na vipi kuhusu CCM KUZINDUA KAMPENI IGUNGA NAO WAMESUSIWA AU??

Kwani Yule mshindi alikuwa mshindi wa nini. Angalia title yake.

Kumbuka miongoni mwa waliofariki ni wateja zao? Je hawa wanathamini wateja wao?
Je maafa hayo yangetokea mafia au Ukerewe wangefanya hivyo?
 
Watanzania kama wewe ndio wanasababisha tuendelee kuwa maskini wa kifikra .Umepanga maneno vyema ila sidhani kama unachangia kitu ulichokielewa .Hoja ya msingi ilikuwa Vodacom kama wadahamini wakuu ndio wenye sauti ya mwisho kwenye mashindano yale .Kamati ingesema tuahirishe yale mashindano wasingeweza kwa sababu sorce yote ya Fedha inatoka kwa Vodacom kwa asilimia zaidi ya 85.Wanatoa msaada kwenye maafa ili hali waliyapuuza maafa! Msaada mkubwa ungekuwa wao kubeba gharama za tamasha na kuliahirisha ,hilo lingeonyesha utu zaidi ya fedha wanazopeleka sasa.Waafrika tumefika mahali tuwe tunajithamini ,kitendo kile kimeonyesha baadhi ya watanzania wachache wanatumiwa vibaya na haya makampuni ya kigeni kwa manufaa yao yao binafsi.Mbaya Tamasha lile limekaa kitaifa zaidi na hufanyika mara moja kwa mwaka na limekaa kiburudani zaidi,ndio maana watu wamelishupalia kwa hoja nzito.Nawasilisha
Sioni logic ya kukataa 'ubani' wa Vodacom na kuwalaumu kiasi hicho kwa sababu;
Vodacom hawakuwa wadhamini pekee katika shindano hilo. Kulikua na wadhamini wengine kama Ngorongoro, TANAPA, Star TV, Giraffe Ocean View Hotel na wengineo. Kwa nini lawama ziende kwa Vodacom pekee? Hata kama Vodacom ndio mdhamini mkuu lakini bado sio haki kupewa lawama zote wakati yeye ni mdhamini kama wengine na sio muandaaji???

Vodacom hajachangia lolote katika kutokea kwa maafa yale, uzembe ulianzia serikalini ambako waliruhusu ile boti/meli kutoka bandarini wakati wakijua ilibeba mzigo mkubwa zaidi ya mara 2 ya uwezo wake wa kawaida. Wao hawajaomba msamaha, hawajafukuzwa walipoenda kuangalia wahanga, misaada yao imepokelewa na pia wengine wameenda kujinufaisha kisiasa kwa makosa waliyoyafanya wenyewe.

Lawama nyingine kubwa inabidi ziende serikalini pia kwa sababu walitaarifiwa mapema kabisa meli ilipokua inaanza kuzama, laiti kama wangekua na utaratibu mzuri wa kukabiliana na majanga watu wengi wangeokolewa na vifo vichache sana vingeripotiwa. Kuchelewa kwao kupeleka kikosi cha uokoaji ndio sababu kubwa ya kutokea vifo vingi kiasi kile. Ingekua imetokea maandamano ya kuwalaumu wao huko Z'bar wangeenda muda ule ule tena kwa boti ya kasi ili kwenda kuwalipua kwa mabomu ya machozi na kuwapiga risasi ila kwa sababu ilikua haiwahusu hawakuona umuhimu, kwa kosa hilo ilibidi walaumiwe vikali na kuwajibishwa. Kwa maana hiyo, sioni sababu ya kulaumiwa kwa Vodacom ili hali wasababishaji na waliofanya uzembe wa wazi hawajalaumiwa.

Taarifa zaidi zilisambaa mida ya mchana, ingawa mpaka mida ya jioni wengi walikua hawajajua kilichotokea. Hakukuwa na uwezekano wa kutangaza kuhairishwa kwa tukio lile mida ya jioni wakati watu wengi kutoka sehemu mbalimbali nchini walikua wamefika kwa ajili ya tukio lile. lakini pia hata maombolezo yalikua bado hayajatangazwa siku ile, hata wewe msomaji hapa nina uhakika 'ulispend' wik end yako kwa furaha as if hakuna kilichotokea.

Hakuna haja ya kuwalaumu Vodacom kwa tukio lile ambalo lilizingatia na kutambua vifo vilivyotokea na walianza tukio lile kwa maombolezo kwa namna ambayo imeelezwa kwenye 'press release' yao. Hata hivyo, tukio lilisheheni watu wengi ambao pia kama ndio hivyo walistahili kulaumiwa kwa kuhudhuria huku wakijua kulikua na maombolezo.

Ninaomba kumalizia kwa kuwatahadharisha; inawezekana kuna watu ambao wanaitumia nafasi hii ya udhamini wa Vodacom kujinufaisha kibiashara. Wanadhamini wanafiki na wazushi ili kupunguza soko la Vodacom kibiashara, wanatumia njia nzuri ila wakati huu sio muafaka kuwafanyia hivyo Wazanzibar na WaTz kwa ujumla katika kipindi hiki cha majonzi. Mshikamano kati yetu sote bila kujali tuliitumia vipi siku ya jumamosi ndo utakaotupitisha salama ila tukianza kulaumiana kwa mtindo huo mwishoni watu wa Zanzibar watatuzuia wabara kwenda kule kisa tuliendelea na kazi siku ambazo wao walikua wanaomboleza. Hivyo, ninawashauri wale wote wanaopandikiza hizo chuki dhidi ya Vodacom waache kwa sababu madhara yake yanweza kuwa makubwa na pia serikali ipokee msaada wa Vodacom kwa maana hauwapunguzii chochote wafiwa ila utawafariji kwa namna moja uau nyingine na pia isijiingize katika malumbano au ugomvi usio na maana.

Huo ni mtizamo wangu, kila mtu anao mtizamo wake.
 
kwa hiyo wangefuta mashindano hao wateja wao wangepona kifo?

Mbona ujiulizi Rais Kikwete alihairisha Safari yake ya Ughaibuni kwa nini?

Je Vodacom au hata hao waandaaji wana mamlaka ya juu kuliko Rais kisheria?

Jiulize . Je maafa hayo yangetokea mafia au Ukerewe, je wangefanya shindano hilo?

Fikiria kabla kunena.
 
Serikali mbumbumbu ya Zanzibar imekataa ubani wa wahuni wenye kupelekea wewe na wenzio wachache uione kuwa ni mbumbumbu
V

Vodacom wameonesha corporate social responsibility kwa kutaka kutoa ubani na serikali mbumbumbu imekataa kupokea. Ulitaka wafanye nini zaidi ya hapo? Yale mashindano wao ni wadhamini tu na sio waandaaji ambao nao hawakuwa na makosa yoyote, sio kiutamaduni wala kisheria. Msitake kukuza saaaaana hii issue ati kwa sababu kuna watu wamekufa basi wengine waache mambo yao. Kama mnaona wamekosea, muwafutie leseni na sio kujaza upuuzi wa maneno maneno. (mimi sio mdau wa voda)
 
Nimeiosoma hiyo habari vyema na kugundua aliyeshawishi suala hilo ni Jussa amaye ni mbunge wa CUF, kama walivyofanya TISS cUF nao wamedla hoja hii ya VODACOm kwa lengo la kuwafumba wapemba wao waliopotea maisha kwa wingi ili kulinda usanii wanauendelea kuufanya kwa kushirikiana na CCM katika Serikali ya Zanzibar.

Ni dhahiri CUF ilikuwa ikitambua hadha wanayopta wapemba katika usafiri wa majini. Hivyo kitendo cha Waziri wa Miundo mbinu toka CUF kulihakikishia Barza la Wawakilishi kuwa hali ya usafiri wa majini ni shwari miezi miwili iliyopita na ndipo itokee ajali hii CUF wanastahili lawama kubwa kwa kutojali shida za wanacvhi wa Pemba/ Ndio maana mara kwa mara tumekuwa tukisisitiza kuwa ukishirikiana na mwizi na wewe lazima utajifunza wizi. Tazama CUF ikiongozwa na Maalim Seif walivyokuwa mstari wa mbele kuisadia CCM na Serikali kuwahadaa wananchi kuwa ile ilikuwa ajali ya kawaida na ndio mapenzi ya mungu.

Aidha Profesa Lipumba amabye mara kwa mara yanatokoea majanga kama haya huita mikutano ya waandishi wa habari na kuwataka mawairi wajiuzulu sfari hii kajichimbia Igunga kimya kabisa kana kwamba hakuna lolote lililowafika wananchi wa Pemba. Ni wabunge mmoja mmoja wa Pemba ambao wanajaribu kupaza sauti zao kueleza hali halisi kuwa mamia ya wananchi hawajawapata ndugu zao au miili ya maiatai lakini uongozi wa juu wa CUUF ndani ya Serikali upo kimya na kwa maan ingine umewatelekeza wabunge hawa na wananchi katika ajali hii.

CUF ni lazima itapata adhabu kutoka kwa wapemba kwa kuwasaliti katika kipindi hiki kigumu na kushuirikiana na CCM kuficha ukweli.
 
watanzania kama wewe ndio wanasababisha tuendelee kuwa maskini wa kifikra .umepanga maneno vyema ila sidhani kama unachangia kitu ulichokielewa .hoja ya msingi ilikuwa vodacom kama wadahamini wakuu ndio wenye sauti ya mwisho kwenye mashindano yale .kamati ingesema tuahirishe yale mashindano wasingeweza kwa sababu sorce yote ya fedha inatoka kwa vodacom kwa asilimia zaidi ya 85.wanatoa msaada kwenye maafa ili hali waliyapuuza maafa! Msaada mkubwa ungekuwa wao kubeba gharama za tamasha na kuliahirisha ,hilo lingeonyesha utu zaidi ya fedha wanazopeleka sasa.waafrika tumefika mahali tuwe tunajithamini ,kitendo kile kimeonyesha baadhi ya watanzania wachache wanatumiwa vibaya na haya makampuni ya kigeni kwa manufaa yao yao binafsi.mbaya tamasha lile limekaa kitaifa zaidi na hufanyika mara moja kwa mwaka na limekaa kiburudani zaidi,ndio maana watu wamelishupalia kwa hoja nzito.nawasilisha

utaweza kuonyesha kujiamini kwa kukimbia tatizo alisi yaani uzembe uliosababisha jali ya meli na kuua idadi ya watu wasiojulikana haidi sasa na kurukia kulaumu mashindano yaliyokuwa yameandaliwa toka mwaka jana. Kama huo ndio unaouita waafrika kujiamini basi napata wasi wasi kama tutaweza kuto0ka hapa tulipo.
 
suala la tbc litachukuliwa na serikali ya jmt kwani pasi na shaka rais wa jmt alitangaza pia maombolezo hayo na hata kukatisha safari yake ya ughaibuni. Hao watakuwa wamedharau mamlaka sio tu za smz bali pia hata za jmt na hivyo wanastahikhi kuchukuliwa hatua na jmt.

Vodacom kama taasisi binafsi lazima ichukuliwe hatua na jmt ambako imesajiliwa lakini vile vile smz lazima wawa adhibu sio tu kwa kukataa misaada yao lakini pia kuwazuilia wasifanye shughuli zao ndani ya mamlaka ya smz kama fundisho kwao kwa kudharau maisha ya watu na kundekeza starehe.

ushuhuda toka kwa walionusurika unaonyesha ya kuwa mamalka ya bandari iliarifiwa kuhus eli hiyo kupakia kupita uwezo wake na baadhai ya abiria waliingia katika mgongano wa wahudumu wa maeli hiyo kwa kutaka kushuka baada ya meli kujaza kupita uwezo wake, wakati yote haya yakitokea vyombo vya dola vilikuwa wapi? Itakuwaje smz na jmt vilivyozembea kwa kiwango kikubwa hivi viiadhibu vodacom? Hii ni ghiliba na kuwahadaa wananchi kuwa mkosaji ni vodacom
 
Mbona ujiulizi Rais Kikwete alihairisha Safari yake ya Ughaibuni kwa nini?

Je Vodacom au hata hao waandaaji wana mamlaka ya juu kuliko Rais kisheria?

Jiulize . Je maafa hayo yangetokea mafia au Ukerewe, je wangefanya shindano hilo?

Fikiria kabla kunena.

Sasa kuna uhusiano gani kati ya safari ya rais na mashindano ya urembo? Janga limetokea nchini mwake, ni wazi mwanasiasa yoyote anayepata kura kwa kuhurumiwa na watu atafanya kama alivyofanya JK. Pili, shughuli ile ya uokozi inahitaji pesa na mwenye pesa ndiyo huyo rais wenu. Lazima aende akahakikishe msaada unatolewa. Kwa maneno mengine Kikwete kwenda Zanzibar kwenye ajali si fadhila, ni sehemu yake ya kazi na analipwa posho kwa shughuli ile. Sasa turudi kwa vodacom; wao kama wafanyabiashara wanaangalia opportunities za kukuza masoko yao mojawapo ikiwa ni mashindano ya miss tz. Pia wanafanya shughuli zao kulingana na sheria za nchi na sio hisia za wanajamii. Kwa hiyo kama maafa yangetokea Ukerewe na wao wakaona itawaharibia biashara yao wangesitisha kwa minajili hiyo. Lakini hebu angalieni thread ngapi zinaisema vodacom JF na ngapi zinakemea uzembe uliotokea. Hamuongei ukweli mnabaki tu kujiliwaza kwa kupitia vodacom. Majungu hayo hayawafikishi popote zaidi ya kukabiliwa na ajali nyingine hivi karibuni kama hamkuchukua hatua. Kwa taarifa yako ni juzi tu boti ya Seagul ililazimika kukimbia abiria baada ya kugundulika waliuza tiketi nyingi kuliko uwezo. Nalo mtawasema vodacom?
 
Wazanzibar wenyewe hawajitambui. Hawautambui muungano na bado wanakomalia ya bara. Hawa watu zimo kweli?
<br />
<br />
Mkuu Raia Fulani, tafakari kabla ya kusema. Wazanzibar hawajitambui kivipi? Mbona hili shindano halikuitwa Miss Tanganyika. Hujui kwamba hakuna kitu Tanzania bila ya kuwepo Zanzibar. Acha upuuzi.
 
Watanzania kama wewe ndio wanasababisha tuendelee kuwa maskini wa kifikra .Umepanga maneno vyema ila sidhani kama unachangia kitu ulichokielewa .Hoja ya msingi ilikuwa Vodacom kama wadahamini wakuu ndio wenye sauti ya mwisho kwenye mashindano yale .Kamati ingesema tuahirishe yale mashindano wasingeweza kwa sababu sorce yote ya Fedha inatoka kwa Vodacom kwa asilimia zaidi ya 85.Wanatoa msaada kwenye maafa ili hali waliyapuuza maafa! Msaada mkubwa ungekuwa wao kubeba gharama za tamasha na kuliahirisha ,hilo lingeonyesha utu zaidi ya fedha wanazopeleka sasa.Waafrika tumefika mahali tuwe tunajithamini ,kitendo kile kimeonyesha baadhi ya watanzania wachache wanatumiwa vibaya na haya makampuni ya kigeni kwa manufaa yao yao binafsi.Mbaya Tamasha lile limekaa kitaifa zaidi na hufanyika mara moja kwa mwaka na limekaa kiburudani zaidi,ndio maana watu wamelishupalia kwa hoja nzito.Nawasilisha

Tafsiri yangu binafsi ya kujithamini ingekuwa pamoja na wahusika kuhakikisha taratibu za vyombo vya usafirishaji zinafuatwa ili kuepusha ajali kama hizi. Pale unapowajaza abiria na mizigo ndani ya chombo ambacho una hakika kabisa hakina uwezo (capacity) huo unaangalia nini maslahi yako binafsi kama mmiliki au kweli una moyo wa huruma sana kuhakikisha abiria wote wanaotaka kufika kwao kwa siku hiyo wafike regardless ya hatari unayowatumbukiza kwayo? Wahusika wa hiyo meli walitakiwa wawe wa kwanza kuonyesha thamani hiyo ya binadamu kuliko kuweka maslahi yao mbele!

Kwa mtindo huu tutaishia kuwatupia lawama kila tunaowaona just to make ourself feel better huku tukiwaacha wahusika wakuu wamekaa kwenye viti vya kuzunguka wakifurahia maisha!

Kwa hili, nawaona Voda kama makando kando sana, wakati wahusika wakuu 'wamekalishwa' kando kivulini....
 
Back
Top Bottom