Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Hivi leo serikali ndio inauwezo wa kukataa msaada kwa kigezo hicho?
Upuuzi wangekuwa makini kwanza wao kwa kuhakikisha meli ile inasafiri kwa masharti husika yaliopelekea ajali lakini watu wasamehe hawakuisusia serikali kwa uzembe wao, leo wanafanya hivyo kuwahamisha watu kutoka katika uzembe wao na uonekana ubaya wa Vodacom.
Vodacom ni wadhamini tu wa shindano lile ingawa nao wanakasehemu kao lakini waliopanga kama wameamua au wameona kuhairisha ni kusababisha hasara unategemea Vodacom wangefanya nini?.
Nchi hii bana kila kitu siasa

TUNACHOKIONGELEA HAPA mkuu ni ile hali ya kuguswa na matatizo yaliyowakumba wenzako,hata kama umefurahia tatizo kutokea basi onyesha hisia zako kwa wafiwa kuwa nawe limekugusa,kuliko kuendelea kupiga miziki na ngoma kana kwamba kilichotokea wewe hakikuhusu,
hicho kilicho washangaza watu

je waweza kufunguwa sauti ya redio hadi mwisho wakati jirani yako kafiwa na kuna watu kibao wamelala matanga ktk msiba huo?
 
Huyu muungwa najibu pia

"@JMakamba: Siku ya msiba, CCM ilizindua kampeni kwa shamra Igunga, Ligi Kuu iliendelea, mabaa yalijaa, but kuna watu wamekomalia shughuli ya vichupi!"
Vodacom ni wadhamini tu, waandaaji na wamiliki wa milele wa shindano ni akina Lundenga na agency yao
 
Hebu hapa tuzungumze hali halisi ya hili suala kwa mujibu wa utaratibu mwenye mamlaka ya kusimamisha shindano alikuwani Lundenga na kamati yake while vodacom yy ni mtu wa kuambia tu mamlaka ya shindano yapo ktk kampuni ya Lundenga vodacom ni Mdhamini tu alikwisha toa pesa toka mwanzo wa mashindano ya wilaya huko!trademark tu ya shindano ndo inayoleta shida!hebu tuwe waelewa ktk hili limeshatokea dats all tujipange vp!mbn ccm hailaumiwi?????
 
Kama hawa watu sio wanafki, basi natarajia kusikia wakiisusia CCM maana Benjamini Mkapa alifanya uzinduzi wa kampeni siku ya jumamosi Igun ga huku wakiwa na taarifa za maafa hayo.
Huu ni unafki ambao kamwe siwezi kuunga mkono, ni mpumbavu pekee unaweza kumnasa kwenye ujinga huu.
 
huu msiba kwa kweli haueleweki kila mtu/kiongozi
yeyote anatoa pole kwa wazanzibar kama vile watanzania bara
hawakuwepo kwenye meli hiyo basi kwa mantiki hiyo basi
shindano hili kufanyika ni sahihi kabisa.
 
Katika hali hiyo Vodacom wangefanyaje ingawaje wanaushawishi lakini waandaaji wameamua hivyo
Kwangu mimi Ligo Agency ya Lundenga ni waganga njaa tu wanao subiri tukio moja tu kwa mwaka wapige hela ya kutakata hivyo kuwaambia wasogeze mbele kutakako pelekea kupata hasara kwao ni ngumu, na wao ndio wakulaumiwa haswa.

Vodacom ni wezi tu lakini katika hili japo hawawezi kukwepa lawama
Mkuu sasa tuko pamoja (kwa kuzingatia uzito wa sentensi zako niloziwekea bold) ila kwa kweli lazima kwa kila muungwana akubaliane na hoja iliyo wazi ya kuwa uzembe wa SMZ kupitia mamlaka zinazohusika kwa kuruhusu Meli iondoke ikiwa imepitiliza ujazo.
 
tuwasusie na ccm kwa kuzindua kampeni jioni wakati habari zilipatikana alfajiri,wangeonyesha kuguswa hata kwa kuacha kupika pilao.
vodacom hawana makosa kwani wao ni wadhamini tu na hawana kauli kwenye mashindano,lundenga ni kada wa siku nyingi wa ccm.
na nyie wazanzibar acheni mambo ya kususa.
 
Kuvuja kwa pakacha nafuu ya... Vodacom uchuneni tu si wamekataa msaada, lakini nawahakikishieni kesho na kesho kutwa hao hao waliokataa msaada watakuja kuomba msaada ama udhamini wa shughuli nyingine, serikali hizi zilivyo matonya wa kutupa watajileta. Worry not mabepari wa vodacom
 
Hatimae kilio cha wengi kimesikika kwani ule msaada uliotolewa na Vodacom kwa wale wahanga wa kuzama kwa meli Zanzibar umekataliwa

kwani pale watu wa Jamhuri ya muungano wakilia na maafa yaliyo wakuta hawa wenzetu kutoka SA Walikuwa wakisheherekea miss Tanzania

hongera serikali ya zanzibar

habari hii ni kutoka redio ujerumani kiswahili

I reserve my comments
 
Siungi mkono hata kidogo, serikali inajikosha!. Nawashauri wazanzibari kwa kutumia uzalendo huuhuu wakatae misaada yote ya SMZ kwani SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kichakavu kikabeba abiria?, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikaongezwa urefu na mafundi mchundo?!, smz ilikuwa wapi hadi chombo kika-overload?!- who's better: a private donor or serikali irresponsible?!. Sitaingamkono hili hatasiku moja-ni kujisafisha @ the expense ya kumkera muhisani. Onyo kwa wazanzibari na watanzania wenzangu- hakuna jema kutoka kwa mafisadi wa madaraka.

Hii SMZ inayozungumziwa bado ipo?? kwani baada ya ile ndoa na wale jamaa mwengine bado inajulikana kama SMZ?? hebu nijuzeni naona kizunguzungu
 
Hongera SMZ, Hongera Zanzibar na Hongera sana waZnz kwa msimamo wenu.

Hakika hio msaada ulikuwa ni kejeli kwenu kwani wao hawakuona kabisa umuhimu wa majonzi yenu na taifa kijumla. Kwao wao ilikuwa bora ni kuendelea na burdani zao na kukwepa gharama.

Mimi nashauri Znz na SMZ ni vizuri mkaenda mbali zaidi kwa kuifungia kabisa Vodacom isi operate Znz ili kutoa fundisho kwa wengine wenye dharau na kibri kama Hao.

Nazidi kujiuliza kama maafa yale angetokea ukerewe au hata Mafia, wangeendelea na miss Tz?
 
huu msiba kwa kweli haueleweki kila mtu/kiongozi
yeyote anatoa pole kwa wazanzibar kama vile watanzania bara
hawakuwepo kwenye meli hiyo basi kwa mantiki hiyo basi
shindano hili kufanyika ni sahihi kabisa.
unaona mkuu hilo ndo tatizo sasa!
 
Hongera SMZ, Hongera Zanzibar na Hongera sana waZnz kwa msimamo wenu.

Hakika hio msaada ulikuwa ni kejeli kwenu kwani wao hawakuona kabisa umuhimu wa majonzi yenu na taifa kijumla. Kwao wao ilikuwa bora ni kuendelea na burdani zao na kukwepa gharama.

Mimi nashauri Znz na SMZ ni vizuri mkaenda mbali zaidi kwa kuifungia kabisa Vodacom isi operate Znz ili kutoa fundisho kwa wengine wenye dharau na kibri kama Hao.

Nazidi kujiuliza kama maafa yale angetokea ukerewe au hata Mafia, wangeendelea na miss Tz?

mhhhhhm
 
Asalamelekum amiii kwani Vodacom wamefanyaje hadi muwazuie huko amii, na SMZ nayo si muikatae kwa uzembe wake shekh wangu
 
Hizo fedha za msaada pengine ndo zingelitumika baada ya kuahirisha hiyo show kufidia baadhi ya gharama. sasa iweje waogope kuingia gharama then wanatumia gharama kinafki kuwaliwaza wahanga. t<span style="color:#ff0000;">hat is right but its not ok!</span> mchekea ujinga haachi mpaka yamkute. tutakuja kumbushana tu wakati huo. wazanzibar walishaonekana wapumbavu sana wanapotetea mambo ila mwishowe hata nyinyi werevu mnaunga mkono. kwa Mungu si kwa mzungu. Mungu atupe uhai tuyaone!
 
Wakubwa kwa hili la Vodacom kwa kweli halikuwa la busara. Lakini ni aibu kwa Serikali kuifanya vodacom kuwa Bangusilo (Mbuzi wa kafara) kwa uzembe wake yenyewe!!! Yenyewe ndiyo ilikua katika nafasi ya kuzuia janga hilo lisitokee!!! Leo hii PM anasema Serikali itajifunza kutoka katika janga hilo... huo si upuuzi jamani??!!! Kama hawakujifunza kwa lile la MV Bukoba.... mpaka waje kujifunza si tutakua tumekwisha wote??!!
 
Back
Top Bottom