Ajali ya Meli: Serikali yetu na utata wa idadi ya abiria walioangamia

Yote hayo ni kwa sababu vodacom walidhamini miss tz siku ile, vinginevyo hali isingekua hivi. Kazi kulaumu na kujivua majukumu yake, SMZ bana
 
Mi nadhani ifike wakati jamani tuandamane tu hata sisi wana JF maana haya mambo yanaudhi sana aisee na sintoacha kuyalipua tu.

Serikali ama kwa makusudi ama kwa sababu zao wenyewe imetoa takwimu za uongo kabisa tena hata hawajafanya research kujua nani na nani kakumbwa na mkasa huo. Sioni mantiki ya kuwa na viongozi wa wilaya, vitongoji, kata, mitaa na hata vijimitaa kama kitu rahisi kama takwimu inakuwa issue ila kuiba hela za wavujajasho kunaratibiwa kwa umakini kabisa.

Kama kawaida yao wamekurupuka na kudai kuwa watu waliopatikana ni 816 tu yaani walio hai 619 na waliofariki 197, halafu wako na furaha kabisa na nasikia washaanza kuratibu u-vasco dagama tayari. Mimi nimeongea na chanzo changu huko Pemba leo na ifuatayo ni takwimu sahihi ambayo naapa kuisimamia na kuitetea kwa kuwa ni ukweli mtupu. Hawa chini ni waliopotea na ambao hawajulikani walipo;


  1. Wete District 1,141
  2. Micheweni District 337
  3. Chakechake District 141
  4. Mkoani 88
Jumla yao wanakuwa 1,1707.

Sasa naamini maneno ya Khalifa mbunge wa Gando Pemba kuwa meli ilikuwa na watu zaidi ya 2,000 (Raia Mwema 14/9/2011).

Aibu sana kwa serikali kukurupuka na vitakwimu vya uongouongo wakati watu wamepotelewa na ndugu zao.

Ndio maana hata baada ya miaka 50 ya uhuru tunabaki kuomba hata divers kutoka nchi tuliyokuwa nayo sambamba, yaani inafedhehesha eti na sisi tuna JWTZ yenye Nevi ila hao nevi kazi ni kuuramba mkanda na kutembea kwa madaha wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, kumbe hawana lolote aisee, aibu... Mkweree, aisee unatia aibu kabisa.
 
Mi nadhani ifike wakati jamani tuandamane tu hata sisi wana JF maana haya mambo yanaudhi sana aisee na sintoacha kuyalipua tu.

Serikali ama kwa makusudi ama kwa sababu zao wenyewe imetoa takwimu za uongo kabisa tena hata hawajafanya research kujua nani na nani kakumbwa na mkasa huo. Sioni mantiki ya kuwa na viongozi wa wilaya, vitongoji, kata, mitaa na hata vijimitaa kama kitu rahisi kama takwimu inakuwa issue ila kuiba hela za wavujajasho kunaratibiwa kwa umakini kabisa.

Kama kawaida yao wamekurupuka na kudai kuwa watu waliopatikana ni 816 tu yaani walio hai 619 na waliofariki 197, halafu wako na furaha kabisa na nasikia washaanza kuratibu u-vasco dagama tayari. Mimi nimeongea na chanzo changu huko Pemba leo na ifuatayo ni takwimu sahihi ambayo naapa kuisimamia na kuitetea kwa kuwa ni ukweli mtupu. Hawa chini ni waliopotea na ambao hawajulikani walipo;

1. Wete District 1,141
2. Micheweni District 337
3. Chakechake District 141
4. Mkoani 88
Jumla yao wanakuwa 1,1707.

Sasa naamini maneno ya Khalifa mbunge wa Gando Pemba kuwa meli ilikuwa na watu zaidi ya 2,000 (Raia Mwema 14/9/2011).

Aibu sana kwa serikali kukurupuka na vitakwimu vya uongouongo wakati watu wamepotelewa na ndugu zao.

Ndio maana hata baada ya miaka 50 ya uhuru tunabaki kuomba hata divers kutoka nchi tuliyokuwa nayo sambamba, yaani inafedhehesha eti na sisi tuna JWTZ yenye Nevi ila hao nevi kazi ni kuuramba mkanda na kutembea kwa madaha wakati wa maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika, kumbe hawana lolote aisee, aibu... Mkweree, aisee unatia aibu kabisa.

Tatizo la serikali yetu ni kukimbilia kuziba maovu yao ili tume yta kuchunguza ije na takwimu zilizo pishana kidogo na zao mbali na hilo mpaka leo sija weza kupata kujua jina la anaye milike Mv.Spice ni tunasikia takwimu kila kukicha ila mwenye meli hatajwi ili ndipo tuanze kujua wapi pakushika ili uchunguzi uwe huru na kufanya kazi yake.

JWTZ (Navy divers) wanajaifunza wapi kuogelea jamani? wajua serikali yetu ime relax sana na ndio maaana kile kitengo cha majanga mpaka matukio yatokee ndio utakisikia kina tangazwa kipindi hiki sija sikia hata wakikiongelea, Ni aibu sana kwa taifa changa kama hili halijipangi kabisa kwa miaka ijayo, hii miaka 50 ya uhuru ni ya majonzi tuuuu.

My Take;

Imefika wakati tudahi haki zetu kwa kuandamana tuuu period
 
Mpaka natuma thread hii sijui kama bado tetesi. Lakini nimedokezwa kuwa abiria 1,170 walikata tiketi, rekodi zaonesha. Watoto wasiolipa hawapo katika orodha, wazamiaji na waliopanda bure kiujamaa, wafanyakazi wa meli. Makadirio ya polisi kwa walio melini ni kati ya 1400 na 1500.


Hivi, hakuna mashindano ya ajali duniani kwenye olimpiki hv? Kila category tutatoka na medali km si dhahabu, fedha au shaba. Meli, mv bukoba na hii ya sasa zitawakilisha. Treni ile ajali ya dodoma. Bus, shengena la Tanga ambalo dereva aliliingiza kwenye maji zima zima abiria wakikenua meno.
 
Halafu politicians wanatwambia meli ilibeba watu 610, huu ni ujinga tu!
 
Ndugu za abiria waliokuwa wakizama na meli ya MV.SPICE walianza kupata taarifa mara meli ilipoanza kuingia katika dalili za wazi za kuzama,hiyo ilikuwa ni usiku wa saa saba.Meli ilipozama na kubaki watu wachache juu ya mgongo wa meli simu ziliendelea kupigwa na wahanga hao.

Hatimae meli ilizama na baadhi ya wahanga kudandia kwenye mlingoti wa meli huku wakiendelea kuomba msaada kwa majonzi kwamba muda wowote na wao wangezama hiyo ilikuwa ni baina ya saa 9 -10 alfajiri.Baada ya hapo hakukuwa na mawasiliano tena na watu hao.Simu baina ya ndugu ndizo ziliwaamsha watu wengi kote Tanzania.
Kwa maelezo ya waliookoka shughuli hasa za uokoaji zilianza asubuhi.Ni wazi kuwa kulikuwa na uzembe katika kila nyanja.Baadhi ya nyanja uzembe ulikofanyika ni kwenye mashirika ya simu.Jee hakuna kitu cha kuonesha ongezeko la watumiaji simu muda ambap si wa kawaida?.

Uzembe mkubwa itakuwa ulifanyika Zanzibar kwenyewe. Vyombo vya Usalama na wahusika wa bandari walikuwa wapi wakashindwa kuona hali ya meli tangu saa 12.30 jioni?.Ofisi ya kukutisha tiketi kwanini haikuwa na mawasiliano na wenzao wa Dar kuonesha kuwa hakukuwa na nafasi tena ya kupakia meli itakapofika Zanzibar.
Hali ya tukio iliendelea kuripotiwa kama lilivyokuwa mpaka pale serikali ya Jakaya Kikwete na vyombo vyote vya ulinzi ilipoamka na kuteka shughuli yote.Kuanzia hapo watu wakatakiwa kupata taarifa zilizoitwa sahihi kupitia vyombo vya habari vya serikali vilivyofanya kazi kubwa ya kupotosha idadi ya waliookolewa na maiti waliopatikana.

Wabunge na wawakilishi huko Pemba wanastahiki pongezi kwa kuweza kwa muda mfupi kupata takwimu za watu waliopanda kwenye meli hiyo na ambao mpaka sasa wanahesabiwa kwamba wamekufa.Kufuatia juhudi zao gazeti la Mwananchi lilmeandika.

MV Spice ilipakia abiria 3000
 
Mkuu wa wilaya wete Bw. Dadi amesema wilaya hiyo pekee imepoteza watu 1141 katika ajali ya meli ya mv spice. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar Maalim Seif Hamad. Huenda meli ile ilikuwa na abiria zaidi ya 3000 aliongeza Bw. Dadi.
 
kuna taarifa zinasema meli ilikuwa na watu 3000,hii serikali itasema nini kwa dunia?
 
MELI ya MV Spice Islanders iliyopata ajali mwishoni mwa wiki iliyopita na kusababisha vifo vya takriban watu 200 na majeruhi 619 ambao waliokopolewa, ilibeba abiria 3,000 wakati uwezo wake ni kubeba abiria 600 tu.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa idadi hiyo kubwa ya abiria, haijumuishi mizigo ambayo kiasi chake bado hakijajulikana.Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Dadi Fakhi Dadi alisema jana kuwa mkoa huo umepoteza watu 1,600 katika ajali hiyo, huku Wilaya ya Wete pekee ikiwa imepoteza watu 1,141.Dadi alisema hayo alipokuwa akizungumza mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.

“Wilaya ya Micheweni imepoteza watu 367, huku Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ikipoteza watu 27 na Wilaya ya Chakechake imepoteza watu 148,” alisema Dadi na kuongeza:

“Kwa idadi hiyo ikijumlishwa na idadi ya watu 619 waliosalimika katika ajali hiyo na wengine 204 waliotambuliwa na kuzikwa na wengine watano waliookotwa Mombasa, huenda meli ile ilikuwa na watu 3, 000,” alisema Dadi.

Kutokana na takwimu zinazoendelea kukusanywa, hadi sasa zaidi ya watu 2,000 hawajulikani walipo, mbali ya wale 198 walioopolewa na kuzikwa na wengine 619 walionusurika.

Wabunge wa CUF wajiandaa kuishtaki Serikali
Wakati Serikali ikiendelea kukusanya takwimu za waliokufa au kupotea kwenye ajali hiyo, baadhi ya wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), wamekuwa wakizunguka majimboni mwao kufanya tathmini kwa lengo la kuishtaki Serikali.

Mbunge wa Jimbo la Ziwani, Ahmed Juma Ngwali alisema anatafuta idadi kamili ya wananchi wake walioathirika kwa ajali hiyo ili afanye utaratibu wa kuishtaki Serikali kutokana na uzembe uliosababisha ajali hiyo.

“Tukishapata orodha kamili ya wananchi, nakwenda kutafuta orodha ya abiria waliokuwa kwenye meli, nalinganisha. Kwa wale waliokuwa na tiketi, nitasimamia walipwe bima zao na mmiliki wa meli. Wale waliozidi nitaishtaki Serikali kwa kuzembea,” alisema Ngwali.

Ngwali aliyekuwa akizunguka nyumba hadi nyumba kuorodhesha watu hao, alisema kwa kiasi kikubwa, Serikali ndiyo iliyofanya uzembe katika tukio hilo.

“Huu ni uzembe na ni lazima twende mahakamani. Ikiwa samaki wa Magufuli (Waziri wa Ujenzi), hadi leo wanasotesha watu mahakamani, itakuja kuwa watu?” alisema.

Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk alisema anakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni ili kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa tukio hilo.

“Inaonyesha Serikali haina takwimu sahihi, ndiyo maana sisi tumeamua kufanya tathmini ya kina,” alisema na kuongeza kuwa tathmini hiyo itamsaidia kuratibu misaada anayopata kutoka kwa mashirika mbalimbali kwa ajili ya watu walioathirika katika tukio hilo.

“Kwa mfano sasa Benki ya Watu wa Kenya (KCB) imetoa ahadi ya kusomesha watoto yatima waliofiwa na wazazi katika ajali hiyo. Lazima niwe na takwimu sahihi za kuwapa benki hiyo,” alisema Mbarouk.

Akizungumzia suala la Waziri Mkuu mbunge huyo alisema: “Sisi ni wasemaji wa wananchi siyo Serikali. Nina mpango wa kupeleka hoja binafsi Bungeni ili Waziri Mkuu awajibike.”

Alieleza sababu za kutaka Waziri Mkuu awajibike kuwa ni pamoja na Serikali kupuuza swali lake alilouliza bungeni kuhusu usalama wa vyombo vya majini hadi sasa.

Kazi ya kuwaokoa walizama bado nguvu
Kazi ya uokoaji wa miili ya watu wanaosadikiwa kunasa ndani ya meli hiyo inaonekana kuwa ngumu baada ya wataalamu wa uokoaji kutoka Afrika Kusini kushindwa kuendelea na kazi kutokana na kina kirefu cha maji katika eneo hilo.

Tetesi za kushindikana kwa kazi hiyo zilianza kusikika jana kutoka kwa wavuvi ambao wamekuwa wakifanya kazi zao katika eneo hilo kwa kipindi kirefu huku. Wavuvi hao wanasema eneo hilo lina urefu wa zaidi ya mita 300 kutoka usawa wa bahari.

Mzamiaji kutoka eneo la Nungwi, Karim Abdallah alisema: “Hili eneo tunalifahamu lina kina kirefu sana unaweza kubeba kamba zinazojaza boti na ukifika eneo hilo na kutupa nanga haifiki chini, tulifahamu kwamba wataalamu hao hawawezi kufanya lolote katika eneo hilo.”

Kauli ya wavuvi hao ilionekana kuthibitishwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ambayo iliamua kuondoa mahema yaliyokuwa yamewekwa katika fukwe za Nungwi kwa ajili ya kuhifadhi miili ilinayopatikana.

Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Juma alisema wameamua kuanua mahema hayo kwa sababu uwezekano wa kupata miili iliyobaki ni mdogo.

“Tumelazimika kuondoa mahema hayo kwa sababu hali inavyoonekana ni wazi kuwa wataalamu hao wanaweza wakashindwa kupata miili ya watu wanaokisiwa kubaki katika eneo hilo” alisema Juma.

Hata hivyo, alipoulizwa juu ya hali ya waokoaji hao ambao bado wako katika eneo la tukio wakiongozwa na Kikosi cha Maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alisema: “Sina mamlaka ya kuzungumzia mazingira ya wataalamu hao isipokuwa taarifa nilizonazo kwa sasa ndizo hizo nilizowapa.”

Wataalamu hao walitakiwa kuanza kazi hiyo juzi lakini wakashindwa kuendelea na kazi hiyo kwa sababu ya hali ya bahari kuwa mbaya. Hata hivyo, walianza tena kazi hiyo leo ingawa si kwa kuingia baharini kutafuta waliokwama chini ya maji, bali kutafuta maiti zinazoelea katika maeneo mbalimbali ya Tanga, Mombasa, Unguja na Pemba.

Katika hatua nyingine mtu mmoja alinusurika jana baada ya kuwadhihaki hadharani watu waliokumbwa na mkasa huo wa ajali ya meli kwa kudai kwamba walistahili.

Mashuhuda waliokuwapo katika eneo hilo walidai kuwa sekunde chache baada ya kutamka maneno hayo, alivamiwa na watu waliokuwa eneo hilo lakini akafanikiwa kukimbilia katika duka la vitabu la Masomo na hatimaye kuokolewa na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiongozwa na Mkuu wa Polisi Kituo cha Malindi, Haji Mgoro.

Mkurugenzi wa duka hilo, Farouk Karim Karim alisema hatua ya mtu huyo kukimbilia dukani kwake ilihatarisha maisha yake baada ya umati watu kufunga mitaa yote inayozunguka Soko Kuu la Darajani ukimlazimisha kumtoa mtu huyo vinginevyo waingie kumtoa wenyewe.

“Kwa kweli mimi sikufahamu hata walipoanzia. Nilikuwa hapa dukani ghafla nikashtuka mtu anaingia ndani huku akisema nakufa, kabla hata sijamuuliza kilichomsibu umati watu ukawa umeshajazana dukani kwangu ndipo nilipolazimika kufunga mlango na kuwaita polisi,” alisema Karim.

Seif atoa mkono wa pole
Maalim Seif, jana aliongoza ujumbe wa viongozi wa Serikali kutoa pole kwa wafiwa waliopoteza ndugu na jamaa zao. Katika ziara hiyo, alifuatana Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalumu; Haji Faki Shaali na Machano Othman Said, Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Zainab Omar na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Said Ali Mbarouk.

Akizungumza na ndugu na jamaa wa marehemu hao katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu, Mkoani na baadaye Uwanja wa Gombani katika Mkoa wa Kusini Pemba, Maalim Seif aliwataka wakazi wa Zanzibar, kuvuta subira kwa kuwa msiba huo ni wa taifa zima na ni mipango ya Mungu.

Alisema Serikali inaamini kuwa kulikuwa na uzembe katika tukio hilo ndiyo maana imeamua kuunda tume huru ambayo itafanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo.Alisema Serikali haitasita kumchukulia hatua mtendaji yeyote atakayebainika kuhusika katika uzembe uliosababisha ajali hiyo.Akiwa Mkoa wa kusini Pemba, Maalim Seif ametoa mkono wa pole na ubani kwa familia zaidi ya 112.



SOURCE: Mwananchi newspaper today September 15th 2011
 
Hili suala la idadi halisi ya abiria waliokuwa katika meli iliyopata ajali litabakia kitendawili na MUNGU ANISAMEHE JIBU LAKE SAHAHIHI HALITOPATIKANA. Nasema hivyo pamoja na kutokuwa mtaalamu wa masuala ya baharini lakini kwa uelewa wangu mdogo, ajali kutokea kwenye MKONDO BAHARI WA NUNGWI inamaanisha miili mingi itakuwa imekokwotwa na mkondo bahari na kutokuwa pale meli ilipozama.

Pia hata hiyo miili ya waliopoteza maisha kwa kuzama na mlei hiyo; naamini miili hiyo mingi itakuwa imeharibika kiasi cha kutoweza kuokolewa na kutambulika (achana na siasa za Mhh Rais za kutumia DNA kutambua waliofariki).

Kwa ufupi hii ni moja ya matukio yatakayobakia ya kihistoria katika Tanzania yatakayotusuta kizazi chetu kwa karne zijazo kuhusu uzembe wetu katika kutekeleza majukumu yetu na uwajibikaji kwa ujumla
 
Asante sana ndugu.. Nimeipenda habari hii na nimeisoma kwa kina. Hapa kuna maswali ya kujiuliza sana. Ila yote tumwachie mola.
 
Asante sana ndugu.. Nimeipenda habari hii na nimeisoma kwa kina. Hapa kuna maswali ya kujiuliza sana. Ila yote tumwachie mola.
<br />
<br />
Kadri muda unavyokwenda ndivyo msiba unavyozidi kuwa mkubwa!
 
Wanaotangaza idadi ya abiria 210 wanapotosha Watanzania maana huyu mkuu wa wilaya ndiye yuko on a ground ambapo analazimika kueleza kile kinachoonekana.
Kwa maana hiyo tunaweza sasa kuona jinsi mamlaka zetu zisivyoweza kuaminika tena na zinapoteza credibility mbele ya wananchi. Hivi ndivyo wanatupa takwimu kila siku na hatuoni mabadiliko na hii inathibitisha kuwa zinakuwa sio sahihi kama hili suala la MV Spice Island!
Tukijifunza kuongea UKWELI (japo unamiza sana wakati mwingine) ndipo tu nchi itaanza kwenda mbele mbali na hapo tutabakia kudumaa kimawazo kama tulivyo sasa!
Poleni sana wafiwa.
Mkuu wa wilaya wete Bw. Dadi amesema wilaya hiyo pekee imepoteza watu 1141 katika ajali ya meli ya mv spice. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makamu wa kwanza wa rais wa zanzibar Maalim Seif Hamad. Huenda meli ile ilikuwa na abiria zaidi ya 3000 aliongeza Bw. Dadi.
 
Ingekuwa ni amri yangu ningesha weka watu wote ndani wanaohusika na uendeshaji pamoja na mmiliki wa meli hio tangu day one halafu kesi baadae. Sasa hivi utasikia tume inaundwa ili posho zitafunwe kisawawa wakati wahusika wakuu wakitembea scot-free. Hii itapita kama ile ajali ya MV Bukoba na ingine tena itatokea hapo baadae. Mxxxxxiii, ama kweli Tanzania imejaa vichwa vya wendawazimu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom