Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Ajali ya Meli: SMZ yakataa misaada ya VODACOM

Hatimae kilio cha wengi kimesikika kwani ule msaada uliotolewa na Vodacom kwa wale wahanga wa kuzama kwa meli Zanzibar umekataliwa

kwani pale watu wa Jamhuri ya muungano wakilia na maafa yaliyo wakuta hawa wenzetu kutoka SA Walikuwa wakisheherekea miss Tanzania

hongera serikali ya zanzibar

habari hii ni kutoka redio ujerumani kiswahili
 
How old is Mdondoaji by the way na huo umri wake unatusaidia vipi kwenye VODAKOM ya Rostam Azizi kudharau mila na desturi za Mtanzania kunapotokea msiba na hasa wa kitaifa hivi???????????

Wewe tunakufahamu sana afisa uhusiano wa VODAKOM lakini ukumbuke kabla ya Vodakom na kazi wanayokupa wewe ni Tanzania kwanza; ikuume Mtanzania mwenzako anapopoteza maisha halafu mwekezaji aanayenufaika na uwepo wa Wa-Tanzania kujiamulia kushiriki mambo mazuri lakini katika kipindi kisicho mwafaka.

Vile vile nakusikitikia kwamba kadiri unavyotafuta kupambana na Wa-Tanzania wote na kutafuta tuonekane kana kwamba ni WAJINGA kwenye malalamiko yetu dhidi ya taasisi mbalimbali zilizotukera sana, hivyo ndivyo unavyoendelea kuiweka VODAKOM pabaya zaidi. Sijui kwamba unalionaje hilo???

Be your age!
 
vodacom hawakustahili kufanya miss tz wakati huu.wangepostpone to next week ingewajengea heshima na uungwana
 
kwakweli maana ni janga la kitaifa lilikuwa
 
Kwa kweli waandaaji wa Miss Tanzania na sponsors walipaswa kuonyesha utu wao. Hata kama wasingeahirisha shindano, wangefanya kitu cha kuonyesha kuwa wameguswa na ajali ile, hata kwa kufanya shindano bila burudani
 
Siungi mkono hata kidogo, serikali inajikosha!. Nawashauri wazanzibari kwa kutumia uzalendo huuhuu wakatae misaada yote ya SMZ kwani SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kichakavu kikabeba abiria?, SMZ ilikuwa wapi hadi chombo kikaongezwa urefu na mafundi mchundo?!, smz ilikuwa wapi hadi chombo kika-overload?!- who's better: a private donor or serikali irresponsible?!. Sitaingamkono hili hatasiku moja-ni kujisafisha @ the expense ya kumkera muhisani. Onyo kwa wazanzibari na watanzania wenzangu- hakuna jema kutoka kwa mafisadi wa madaraka.
 
Hivi leo serikali ndio inauwezo wa kukataa msaada kwa kigezo hicho?
Upuuzi wangekuwa makini kwanza wao kwa kuhakikisha meli ile inasafiri kwa masharti husika yaliopelekea ajali lakini watu wasamehe hawakuisusia serikali kwa uzembe wao, leo wanafanya hivyo kuwahamisha watu kutoka katika uzembe wao na uonekana ubaya wa Vodacom.
Vodacom ni wadhamini tu wa shindano lile ingawa nao wanakasehemu kao lakini waliopanga kama wameamua au wameona kuhairisha ni kusababisha hasara unategemea Vodacom wangefanya nini?.
Nchi hii bana kila kitu siasa
 
Hatudanganyiki, bora mtulie mnatuzidisha hasira kwa kujifanya kuhamishia hasira zetu kwingine. Mmetumia pesa nyingi sana kuosha nyota yenu kupitia vyombo vya habari. Mnaingia hasara tu na kuzidisha hasira za wananchi. Vodacom is inhuman
 
Pole sana ndugu yangu SMZ ndio inhuman no one, ndio ambayo ipo reponsible kwa yaliyotokea.
Leo hii yenyewe ndio ya kwanza kuhukumu wasio husika kwa kigezo cha kijinga
 
Hivi leo serikali ndio inauwezo wa kukataa msaada kwa kigezo hicho?
Upuuzi wangekuwa makini kwanza wao kwa kuhakikisha meli ile inasafiri kwa masharti husika yaliopelekea ajali lakini watu wasamehe hawakuisusia serikali kwa uzembe wao, leo wanafanya hivyo kuwahamisha watu kutoka katika uzembe wao na uonekana ubaya wa Vodacom.
Vodacom ni wadhamini tu wa shindano lile ingawa nao wanakasehemu kao lakini waliopanga kama wameamua au wameona kuhairisha ni kusababisha hasara unategemea Vodacom wangefanya nini?.
Nchi hii bana kila kitu siasa

Ajali ni ajali tuu, hata uchukue tahadhari gani kama it is to happen it will happen tuu ila we do our best kuchukua tahadhari zote ajali zisitokee.

Lakini ndugu yako anapopata janga au ajali ni bora ukamkarimu/kumliwaza na sio kusheherekea au kutamashika.

Unavyosema eti vodacom walikwepa hasara ina maana wameona hasara ni bora kuliko utu, au una maanisha kuwa wanathamini sana pesa kuliko ukarimu, mbona wenzao wametoka sehemu mbalimbali kwenda zanzibar kusaidia kwani wao hawapati hasara/gharama?

Think twice and more as u can!

Kwa hili Vodacom wamechemka.
 
Kila mtu anajua kwamba serikali imefanya uzembe kusababisha ajali na kuchelewa kuokoa watu.
Kila mtu anajua Vodacom walisherehekea msiba ule na kutuonesha dunia mzima live namna wanasherehekea msiba

Kusema serikali nao Wana makosa hakuifanyi Vodacom kuwa haikufanya kosa. Kila mmoja awajibike kwa kosa lake, Huo ndio uungwana na ndicho kitakachowanusuru.
 
SMZ isuse na misaada toka CCM kwa sababu wakati wengine tunaomboleza, mwenyekiti wao mstaafu alikuwa anazindua kampeni ya Ubunge Igunga.....
 
Ajali ni ajali tuu, hata uchukue tahadhari gani kama it is to happen it will happen tuu ila we do our best kuchukua tahadhari zote ajali zisitokee.

Lakini ndugu yako anapopata janga au ajali ni bora ukamkarimu/kumliwaza na sio kusheherekea au kutamashika.

Unavyosema eti vodacom walikwepa hasara ina maana wameona hasara ni bora kuliko utu, au una maanisha kuwa wanathamini sana pesa kuliko ukarimu, mbona wenzao wametoka sehemu mbalimbali kwenda zanzibar kusaidia kwani wao hawapati hasara/gharama?

Think twice and more as u can!

Kwa hili Vodacom wamechemka.
Mkuu sijasema Vodacom walikwepa hasara, nimesema Vodaco ni wadhamini tu wa lile shindano, Ligo Agency ya lundenga ndio wamiliki na waandaaji wa lile shindano, walipewa pesa na Vodacom na waliisha fanya kilakitu, so kwa madai yao kuhairisha ilikuwa ni hasara kubwa.
Katika hali hiyo Vodacom wangefanyaje ingawaje wanaushawishi lakini waandaaji wameamua hivyo
Kwangu mimi Ligo Agency ya Lundenga ni waganga njaa tu wanao subiri tukio moja tu kwa mwaka wapige hela ya kutakata hivyo kuwaambia wasogeze mbele kutakako pelekea kupata hasara kwao ni ngumu, na wao ndio wakulaumiwa haswa.
Kinacho nikera mimi ni kukataa misaada ya Vodacom, inakuwa kama mfano ingecheza mechi ya ligi kuu badala ya kuilaumu TFF uanze kulaumu mdhamini wa ligi kwanini karuhusu mechi ichezwe.
Vodacom ni wezi tu lakini katika hili japo hawawezi kukwepa lawama lakini si kufikia kukataa misaada yao as if hao walio kataa ni watakatifu saana kumbe wao ndi chanzo cha haya yote.
Na wamefanya hayo ili sasa tusiona udhaifu wao tuona unyama wa Vodacom
 
Ndo mana siwasikii kabisa kwenye tuki hili la wahanga...duh kazi kwerkwer
 
Kwa hili la Vodacom, siwezi kuwalaumu Wazanzibar msiba ni wakwao wana haki ya kukataa hiyo misaada ya kinafiki
 
Back
Top Bottom