peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 16,602
- 27,378
Usalama wa abiria awamu ya sita barabarani ni 0%
Raia wengi wa Tanzania wana akili ndogo ndio maana hata wakiwa kwenye gari hawaoni tofauti ya mwendokasi wa hatari na speed ya kawaida, hawana habari kabisa na usalama wao safarini.So sad,nawaombea marehemu wapumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka waungane na familia zao.
Madereve wetu kuweni makini barabarani mwaka 2016 niligombana na mmoja wa maderva tulikuwa tunatoka dar kwenda Mwanza,tumefika shinyanga dereva akawa anaendesha gari kwa spidi Kali sana nikamfata nikamgombeza vizuri alielewa Cha ajabu abiria wenzangu walikuwa wanaona kawaida tu ile spidi.Madereva badilikeni familia zanapata shida sana kuwapoteza wapendwa wao,tuwe makini.
Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutaterejea.Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.
Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi
Chanzo cha ajali ikiwa ni mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza
Updates
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66 na 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================
View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875
View attachment 3641983
View attachment 3641876
Hakuna awama nchi usalama wa barabara umewahi kuwa na afadhali, awamu ya jiwe kulikuwa na ajali nyingi tu mbaya sana.Usalama wa abiria awamu ya sita barabarani ni 0%
Sahihi bila njia nne watu wataendelea kufa sana kwa ajali katika hizi barabara zetu za njia mbili kadri gari zinavyoongezeka.Haraka bila sababu ,kujiona kwamba wao ndio kipaumbele kwenye barabara hiyo ni shida kubwa. Njia nne ndio suluhisho kwa aina ya madereva wetu.
1. Barabara nyembamba 2. Madereva wazembe 3. Mwendo kasiIfikie hatua tuseme yatosha sasa ajali kila leo enzi za mwenda zake ajali zilipungua sana ila huyu mama sijui ana jini mnywa damu
Kwa uhakika wa 100%, akitokea kiongozi mzuri, akatumia fedha zote zinazotumika kwa matumizi ya kifahari na ufisadi, mikoa yote itaunganishwa kwa barabara nne.Sahihi bila njia nne watu wataendelea kufa sana kwa ajali katika hizi barabara zetu za njia mbili kadri gari zinavyoongezeka.
Katika hekaheka za kujiweka salama upande wao, madereva wanalengesha angle wanaposimama makonda. Muda huo urafiki haupo ni suala la usalama binafsi.Hatari Sana, Ajali za mabasi zinapotezaga sana matingo/kondakta.