Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Barabara yetu ya kwenda mikoani ipo kama ulimi, kila siku nchi inakopa na pesa hazieleweki zinafanyiwa Nini? Katika vitu Bora katika nchi ipo barabara , inatakiwa iwe Pana na kubwa
 
Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.

Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi

Chanzo cha ajali ikiwa ni mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza

Updates 1
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66 na 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================

Updates 2
=========================
Dereva nambari 2 wa basi la Isamilo akamatwa na anashikiliwa na jeshi la polisi Dodoma
Ikumbukwe huyu dereva ndiye "aliyesababisha" ajali kisha kukimbia akiwa na majeraha
=========================

View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875
View attachment 3641983
View attachment 3641876
Madereva wa mabasi yote wachunguzwe,hiyo ajali inavyoonekana speed ilikuwa ni zaidi ya 80 km/h ambayo imependekezwa kwa mabasi,kufanyike uchunguzi wakina pia kwa mabasi mengine kuna kila uwezekano vidhibiti mwendo kuwa vimechezewa...
 
Haya mapumbavu hata ukiwa Bagamoyo road kule Bunju,Boko yana vurugu kweli kujidai yana haraka wakati tayari wako Dar. Kuwachekea Hawa wapumbavu ndio sababu wanaua ndugu zetu kizembe.
Barabara funyi sana kutoka tegeta kibaoni mpaka unamaliza bunju b sokoni karibu na mapinga kuna wingi wa magari ila hao dereva basi ni changamoto sana, walitamani kuwa wao barabarani.
 
Akae mbele labda hajitaki, anajua lazima mwenzake angepeleka kushoto na hata ingekuwa yeye angefanya hivyo
images.jpeg
 
Kuna haja ya serikali Kuja na njia mbili zinazoenda na kurudi Katika barabara kuu za kuelekea mikoani ili kupunguza haya matukio ya ajali za kikatili
 
Hao wote wamefanyishwa mitihani na kuthibitishwa huko LATRA na pia ku-renew leseni zao waliombwa vyeti vya taaluma ya udereva kutoka VETA.

Bila kusahau hayo mabasi yamekaguliwa polisi yana sticker ya Wiki ya nenda kwa usalama.

Uzembe unadhibitiwaje?

Hua wanawachekea, wanapo ONA wana overtake barabarani sehemu isiyo ruhusiwa.

Inatakiwa mtu kama huyu anafutiwa leseni, Aende kua fundi mchundo.

Huwezi beba watu 50+ halafu uendeshe kizembe namna hyo.
 
Haya mapumbavu hata ukiwa Bagamoyo road kule Bunju,Boko yana vurugu kweli kujidai yana haraka wakati tayari wako Dar. Kuwachekea Hawa wapumbavu ndio sababu wanaua ndugu zetu kizembe.

Walitakiwa wawe wanafutiwa leseni.

Kupiga faini tu haitoshi.
 
Haraka bila sababu ,kujiona kwamba wao ndio kipaumbele kwenye barabara hiyo ni shida kubwa. Njia nne ndio suluhisho kwa aina ya madereva wetu.
Kujenga barabara ya lami njia mbili ni kukatili na kuendelea kupoteza nguvu kazi ya taifa.
 
hapana, davoo #2 (gen z flani) ndiye alikuwa nyuma ya usukani
mzee alikuwa kasimama tayari kupokea kijiti chuma ikifika Nala kulisha
Kuna bus nipo hapa,staff wanazungumzia huyu davoo alivyopenda watoto wake 💔
 
Back
Top Bottom