Cape Verde; Wanafunzi 25 wafariki kwa ajali

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
383
Reaction score
866
Watu 25 wamefariki dunia, wengi wao wakiwa watoto na vijana, baada ya basi lililokuwa limebeba abiria waliokwenda katika ziara kuanguka kwenye korongo katika Kisiwa cha Fogo, nchini Cape Verde.

Ajali hiyo ilitokea Jumamosi jioni katika eneo la milimani kaskazini mwa Fogo, ambapo basi hilo lilitoka nje ya barabara na kutumbukia kwenye korongo lenye kina cha takriban mita 30.

Miongoni mwa waliofariki ni dereva wa basi hilo, huku abiria wengine kadhaa wakijeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya São Francisco de Assis kwa ajili ya matibabu.

Taarifa zinaeleza kuwa wengi wa waliokuwa ndani ya basi walikuwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari. Safari hiyo haikuandaliwa rasmi na shule, bali ilikuwa ikiandaliwa na dereva huyo kila mwaka.

Shughuli za uokoaji zilikuwa ngumu kutokana na eneo la ajali kuwa la miinuko, lenye miamba na lisilofikika kwa urahisi. Mamlaka zinaendelea kuchunguza chanzo cha ajali hiyo, huku baadhi ya majeruhi wakielezwa kuwa katika hali mbaya.
1788762972568.png
 
View attachment 3664967
Ajali kubwa hii,
 
Inasikitisha sana ,madereva wengi huwa wanamatatizo ya afya ya akili ,mambo ya kutafuta pesa ya Boss daily ni kama wanawake na kausha damu...huwa akili hazifanyi kazi ukichanganya akiwa road lazima awaingize mtaroni.
 
Back
Top Bottom