Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Mbaya sana ajali za mabasi nyingi wanaosababisha ni hao madereva kwa kutaka kuyapita magari mengine bila hata kuwa na uhakika kama atamaliza salama wanaua abiria kizembe sana ukiwa na safari unawaza na vichwa vya madereva ni kama vina mafuta ya taa kichwani..
 
Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.

Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi

Chanzo cha ajali ikiwa na mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza

Updates
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66, 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================

View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875View attachment 3641876
 
Kukaidi sheria kutateketeza sana ndugu zetu hao watu waliofariki wana watu wangapi nyuma yao daah.

Tangu mwaka huu uanze kila mtu ninayemjua amepoteza rafiki au ndugu kwa ajali, Boda boda zimeongoza

Tatizo ni moja tu, kupuuza SHERIA ZA BARABARANI .

Tuwe makini jamani madereva na wasafiri, na hapa Dar Boda boda ni hatari kuliko Kulala na mtu mwenye HIV
 
Haraka bila sababu ,kujiona kwamba wao ndio kipaumbele kwenye barabara hiyo ni shida kubwa. Njia nne ndio suluhisho kwa aina ya madereva wetu.
Haya mapumbavu hata ukiwa Bagamoyo road kule Bunju,Boko yana vurugu kweli kujidai yana haraka wakati tayari wako Dar. Kuwachekea Hawa wapumbavu ndio sababu wanaua ndugu zetu kizembe.
 
Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.

Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi

Chanzo cha ajali ikiwa ni mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza

Updates
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66 na 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================

View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875
View attachment 3641983
View attachment 3641876
Yote hii ni shauri ya kutozingatia taaluma ya udereva. Una-overtake vipi kwenye mlima na uko mwendo kasi? Dereva lipungukiwa maarifa ya udereva! Ajali zinazotokana na ubovu wa gari ni chache mno, nyingi ni hizi za kusababishwa na binadamu.
 
Hata juzi hapo kuna basi la Manyara limegongana uso Kwa uso na Lori, Kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba watu sita walifariki, watu wamekatika vibaya Sana and probably kuna zaidi watakaokufa maana Ile basi ni kama imekatika hivi....

Yani Ile trailer imekwenda kukata upande wa dereva kama kisu shwaa ikapita na wale waliokaa kulia, dereva mwenyewe licha ya kuwa kafariki lakini pia amekatika vibaya Sana, dereva Kipindi anaiona ajali hii hapa alisikika Tu akisema "Watoto wangu jamani" then kishindo Kikubwa...Konda hakuumia kabisa mzimaaa maana nasikia konda alivyoona Hapa kama kuna ajali basi akakimbilia kurudi nyuma ndio Pona Yake.

Mwenye Lori ndio mwenye Tatizo ame overtake reckless....
 
Back
Top Bottom