Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Ajali ya basi la Isamilo na Libanika, alfajiri ya leo

Watoto wangu jamani" then kishindo Kikubwa...Konda hakuumia
Dah inaumiza sana Jamani, jamaa alipenda sana watoto wake Hadi pumzi ya mwisho kwenye hatari kubwa anakumbuka watoto wake.
dereva mwenyewe licha ya kuwa kafariki lakini pia amekatika vibaya Sana, dereva Kipindi anaiona ajali hii hapa alisikika Tu akisema "Watoto wangu jamani" then kishindo Kikubwa...Konda hakuumia
 
Hawa wapumbavu wa mabasi wamezoea kuovateki wanapojisikia, wakitukuta sisi waendesha bebi woka tunawapisha njia,wakikutana wemyewe au na Lori haya ndio matokeo yake. Na wakifanya upumbavu wao kuna abiria wanachekelea tu kama mazuzu.
Siku moja nipo kwenye basi dereva wa basi hilo alifanya kitu cha kijinga sana ilibaki nusu tu kama sio kulivamia roli basi alikuwa anatumwaga wote huwezi amini kuna bwege mmoja nyuma huko aliropoka mwaga moto baba ipe ipe, hapo ndio niliamini kweli uchawi upo
 
Hawa maoondakta wangekuwa wanawekewa siti yao mbali na huo mlango, hata kama dereva kapoteza maisha utaona hapo ajali imeelemea upande mwingine maana yake ni kwamba alijaribu kujinusuru akapeleka kwa Kondakta.

Pale mbele ni hatari sana hata madereva wa akiba kwa maaafa marefu hawathubutu kukaa pale. Wanachukua kigodoro na kulala kwenye korido au kama siti zipo wanaenda zao kujilaza mwisho kabisa.

Makonda hawashtuki hilo
Hii ni kweli karibuni hapa gari ya baraka ambayo ikiendeshwa na dereva wa akiba iliacha barabara ikaenda kugonga nyumba pale kiwalala saa 10 alfajiri na ikawagonga watu wawili mke na mume waliokalala mule ndani ya nyumba na wakafarik palepale pamoja na dereva nae....ila dereva mkuu yeye alikaa nyuma kabisa kule
 
Haya mapumbavu hata ukiwa Bagamoyo road kule Bunju,Boko yana vurugu kweli kujidai yana haraka wakati tayari wako Dar. Kuwachekea Hawa wapumbavu ndio sababu wanaua ndugu zetu kizembe.
Kweli hususani usiku huwa yanatembea kweli kweli yaani....
 
Shubamiit tatizo la pili ni baadhi ya abiria 70% wanapenda speed kwenye safari...nyie abiria pia ni tatizo.
 
Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.

Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi

Chanzo cha ajali ikiwa ni mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza

Updates 1
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66 na 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================

Updates 2
=========================
Dereva nambari 2 wa basi la Isamilo akamatwa na anashikiliwa na jeshi la polisi Dodoma
Ikumbukwe huyu dereva ndiye "aliyesababisha" ajali kisha kukimbia akiwa na majeraha
=========================

View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875
View attachment 3641983
View attachment 3641876
Pole sana kwa wahanga wa ajali
NAFIKIRI CHANZO CHA AJALI SIO MWENDO KASI (SIKU HIZI MABASI YA USIKU YANATEMBEA 80kms)
BALI UZEMBE WA DEREVA KUPITA GARI JINGINE KWENYE KONA BILA KUCHUKUA TAHADHARI YOYOTE

Watu wamezoea wakisha sikia ajali, wanasema ni mwendokasi. Kimsingi mwendokasi huwa sio chanzo cha ajali. Chanzo cha ajali nikutokufuata sheria na taratibu za barabarani na ndio sababu magari yakaruhusiwa kuwa na speed hadi 240kms
 
Pole sana kwa wahanga wa ajali
NAFIKIRI CHANZO CHA AJALI SIO MWENDO KASI (SIKU HIZI MABASI YA USIKU YANATEMBEA 80kms)
BALI UZEMBE WA DEREVA KUPITA GARI JINGINE KWENYE KONA BILA KUCHUKUA TAHADHARI YOYOTE.....
Yeah!! Upo sahihi mkuu,, mtu unaovertake vipi kwenye kona kali au mlima
 
Ajali mbaya za basi la Isamilo linalofanya safari zake Mwanza-Dar kugongana uso kwa uso na basi la Libanika (Dar-Mwanza) iliyotokea alfajiri ya leo, kijiji cha Msembeta, kata ya Nala, wilaya ya Dodoma, mkoa wa Dodoma.

Kumekuwa na ripoti za vifo kadhaa na majeruhi wengi

Chanzo cha ajali ikiwa ni mwendokasi wa basi la Isamilo (linatoka Mwanza kwenda Dar) , ku overtake lori kwenye mlima na likiwa kwenye kona kali, kulivamia basi la Libanika lililokuwa linatoka Dar kwenda Mwanza

Updates 1
=========================
Wamefariki watu 9 ikiwemo dereva, makondakta na abiria
Jumla ya majeruhi ni 66 na 9 kati yao wameripotiwa kuwa katika hali mbaya na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
==========================

Updates 2
=========================
Dereva nambari 2 wa basi la Isamilo akamatwa na anashikiliwa na jeshi la polisi Dodoma
Ikumbukwe huyu dereva ndiye "aliyesababisha" ajali kisha kukimbia akiwa na majeraha
=========================

View attachment 3641954
View attachment 3641874View attachment 3641875
View attachment 3641983
View attachment 3641876
Nimejifunza kitu, usithubutu kukaa siti za mbele Upande wa abiria. Bora ukae Upande wa Dereva lakini Siri za kati kati
 
Mbaya sana ajali za mabasi nyingi wanaosababisha ni hao madereva kwa kutaka kuyapita magari mengine bila hata kuwa na uhakika kama atamaliza salama wanaua abiria kizembe sana ukiwa na safari unawaza na vichwa vya madereva ni kama vina mafuta ya taa kichwani..
Madereva wanaendesha kwa mazoea, hawachukui tahadhari kabisaa.
 
Sidhani kama kuna dereva wa bus huwa anazingatia sheria, hawa jamaa huwa wana overtake hadi kwenye zile kona za barabara ya Dom- Iringa.

Tena haoni mbele.
Jamaa wajinga sana! Na hivi vitu viko wazi kabisa! Sijui kwa nini wanakuwa wajinga hivyo?
 
Mkuu, mi sitetei kitu chochote kinacholea uzembe wa madereva. Halafu sio tu kufanya mtihani, sheria ziwe Kali kiasi kwamba anaetaka kufanya uzembe anajiuliza mara 100. Halafu teknolojia itumike, trafiki hawezi kuwepo kila mahali, ila teknolojia inaweza kuwepo kila mahali, ukiovertake kijinga tu adhabu inakusubiri. Bado usalama wa barabarani sisi tunatania
Wewe ndyo ungetakiaa uwe bungeni, hawa matabulasa sjui wanafanya nini huko
 
Hawa maoondakta wangekuwa wanawekewa siti yao mbali na huo mlango, hata kama dereva kapoteza maisha utaona hapo ajali imeelemea upande mwingine maana yake ni kwamba alijaribu kujinusuru akapeleka kwa Kondakta.

Pale mbele ni hatari sana hata madereva wa akiba kwa maaafa marefu hawathubutu kukaa pale. Wanachukua kigodoro na kulala kwenye korido au kama siti zipo wanaenda zao kujilaza mwisho kabisa.

Makonda hawashtuki hilo
😅😅😅 unajua ukishakuwa dereva unajua hali ilivo, mimi ni dereva kuna namna nakuelewa, road life sio easy.
 
Hii ni kweli karibuni hapa gari ya baraka ambayo ikiendeshwa na dereva wa akiba iliacha barabara ikaenda kugonga nyumba pale kiwalala saa 10 alfajiri na ikawagonga watu wawili mke na mume waliokalala mule ndani ya nyumba na wakafarik palepale pamoja na dereva nae....ila dereva mkuu yeye alikaa nyuma kabisa kule
Akae mbele labda hajitaki, anajua lazima mwenzake angepeleka kushoto na hata ingekuwa yeye angefanya hivyo
 
Back
Top Bottom