ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

Viongozi siyo wananchi bwashee?
Kuna rafiki angu mpemba nafanya nae kazi huku wakati wa uchaguzi alirudi kwao zanzibar kupiga kura. Nilimwambia maneno kama uliyoyasema ww kuwa mpinzani wa kweli TZ ni Lissu hivyo nilimwambia relax inabidi ktk siasa za Tz kwa vyama pinzani uwe umejiandaa kisaikolojia vinginevyo yanaweza kutokea mambo ya kuumiza kama haya.

Alichonijibu sio kuunda serikali ya umoja bali kwanini viongozi wao wa ACT hawa kuwashirikisha wananchi wanachama wa ACT wa kawaida wangesikia maoni yao ingekuwa jambo la busara hiki ndio kinachomuuma na kumkera kutowahusisha wao
 
ACT wazalendo wapi misimamo yenu sasa..
Zitto fanya mikutano ya kisiasa achana na hizi mambo
Jenga msingi mashinani, hamna watu huku bara hamna mashabiki wala wafuasi wala wanachama mmepoteza

Hao wa wazanzibar walikuwa wa CUF sasa mnarudia kosa la CUF
Weka mikakati ya kuvuna wanachama toka CCM
Ukiendelea utabebwa na upepo toka kwa wenzako
 
Wala sitaki kujua, ila wakosee tu watambue uwepo wa hao wahuni bungeni. Itakapofika wakati wa uchaguzi wawaombe wanaccm wajitokeze kuwaunga mkono, lakini kura zetu wasisahau rasmi. Sasa hivi wenye maamuzi ni sisi wapiga kura, na sio wao. Na uwezo wa kushawishi watu wasipige kura tunao.
Kwa 100% cdm hawawezi kuingia kwenye huo mtego wa tamaa ya fisi
 
Kimsingi pamoja na kejeli zitakazoelekezwa na watu juu ya uamuzi huu kwa chama cha ACT Wazalendo mimi naona wametumia busara iliyopitiliza. Kwa mujibu wa Ado walitakiwa wachague jambo moja kati ya mawili, kuamua maamuzi mabaya au kuamua maamuzi mabaya zaidi.

Ninaamini mzee maalim anaijua zanzibar na anajua zanzibar inahitaji nini, ni maamuzi ya kikomavu sana.
Hapo ACT walichotazama ni maslahi binafsi ya viongozi wa chama chao na siyo maslahi ya watanzania
 
Zito alisha saliti CHADEMA enzi hizo, kutaka uenyekiti wa Mbowe, si mtu wa kumwamini. Kwa hili mimi sioni ajabu maana Zito ana historia ya usaliti!
Zitto ni state agent hilo lipo wazi na tumesema sana hapa jukwaani,Zitto yeye anachohitaji ni kuhakikisha ccm haikwamishwi na wapinzani
 
Siasa siasani. Katu huwezi kula cha mtu ukawa huru kumshitaki.

Naomba wanasiasa mjue gharama mnayotulipisha wananchi kuuwawa, kufungwa, kusota rumande, kujeruhiwa na kutiwa ulemavu alafu nyie kilahisi tu mnatoa sababu zisizokua na mashiko.

Mmetufunza , tumeelimika na katu tunawaomba msije kutulaghai tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom