Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
1,760
2,000
Na wewe pia huelewi umetumia muda mwingi kuandika Trumbo,kalazwe muhimbili halafu daktari akuandikie MRI scan ,kama utafanyiwa bure .Dawa hela vipimo hela bado unaiita universal health care system.You must be mad
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
8,539
2,000
Hayo makundi yaliyosamehewa kwa kifupi yanaonekana ni mzigo kwa serikali ya CCM. Wazee wengi 75+ wanasema wakiugua wanawahi hospitali, kwenye foleni wanatengwa wanaambiwa wasubiri. Mpaka wale wenye Bima waonwe wote hapo ni saa 8 mchana ndiyo unaandikiwa paracetamol hata kama unaharisha.
nimecheka km mazuri lol.
 

Themagufulianz

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
3,869
2,000
hicho ni kijiji cha ujamaa boss..

wako wangapi?

plus wanashamba lao la wizi congo...

Chunguza what you trying to call uelewa..
..una tatizo la uelewa.

..kutakuwa na bima ya afya kwa raia wote wa Tz.

..rwanda wana bima ya afya kwa raia wao, kwanini watanzania tushindwe?
 

Themagufulianz

JF-Expert Member
Apr 15, 2017
3,869
2,000
kwa heshima tu mkuu jina lako kubwa sana JF usijishushe....

population ya Rwanda ndogo sana
..una tatizo la uelewa.

..kutakuwa na bima ya afya kwa raia wote wa Tz.

..rwanda wana bima ya afya kwa raia wao, kwanini watanzania tushindwe?
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,200
2,000
We mleta mada ni mpumbavu. Kama tuna sera ya kutoa huduma za afya bure, kwanini kuna taasisi binafasi??

Ubure wa gharama ndio kielelezo ya kukosa ubora halo iliyopelekea kuwepo taasisi binafsi, bima na hata mjadala wenyewe!!
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,576
2,000
..UHC ipo kwa nchi kama Canada, Ujerumani, na kwa majirani zetu wa Rwanda.
Hizo ni UHCI siyo UHC. Wanaziita Universal Health Care Insurance. Ni mifuko ya bima ya afya inayomilikiwa na serikali zao kama hii ya kwetu ambayo sisi tunaiita National Health Insurance Fund. UHC ni mfumo, health insurances ni mojawapo tu wa mikakati ya kuwezesha mfumo huo. Canada hiyo UHCI ni free, maana yake serikali ya Canada inatenga fungu (vote) la serikali kwenye bajeti yake ambalo watoa huduma wote wa afya (wa binafsi na wa serikali) hurejeshewa gharama waliyotumia kuwahudumia wateja wao.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,576
2,000
..itanunuliwa at an affordable
Zinanunuliwa at realistic rate la sivyo bima hizo zitafilisika. Huwezi kwa mfano ukauziwa premium ya comprehensive insurance ya gari lako la thamani ya sh million 200 kwa shilingi laki moja (affordable) tu. Utakapopata ajali na gari lako likawa written off, huyo mmiliki wa hiyo bima yako atashindwa kuilipa la sivyo atafirisika.

Ndiyo maana kuna vifurushi mbali mbali kwenye hizo bima. Sasa hivi NHIF yetu inavifurushi kama vitano. Kutegemea na uwezo wa mteja kama vilivyo vifurushi vya mitandao ya simu . Kama ilivyo mtu anaweza kununua kifurushi cha kutuma sms tu, ndivyo ilivyo sasa kwa NHIF mtu anaweza kununua kifurushi cha tiba ya magonjwa basic (common) tu kwa gharama ndogo sana. Ukweli ni kuwa zaidi ya asilimia 80% ya wagonjwa wetu ni wa magonjwa basic tu.

Magonjwa yanayoongoza kwa vifo nchini kwetu ni: HIV (17%), Low respiratory tract infections (11%), malaria (7%), diarrhoea disease (6%), tuberculosis (5%), cancer (5%), magonjwa ya zinaa (3%), sepsis (2%). Haya yote yako covered kwenye kifurushi cha bei ndogo sana au yanatibiwa bure.
 

124 Ali

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
7,602
2,000
Huu ndio ubwege wa mtoa post!anaongea kama vile watu wwnye akili ni Mgufulu Lisu na yeye na kwamba magufuli na Lisu wanagombania kutudanganya au kutuambia ukweli ila hatuwaelewi na mtoa post ndio mkalimani wetu yeye anamuelewa Magufuli na anamuelewa Lisu na ana uwezo wa kutuelewesha wananchi!
Nikuambie tu shika adabu yako tuko mitaani tunajua tunachopitia kuhusiana na mambo ya bima wacha tipigie kura mfumo bora wa bima
 

Areus

Senior Member
Jul 27, 2016
168
250
Mleta mada, JARIBU kufanya Comparative heath care analysis kabla ya kuja hapa kuleta kinachoitwa bookish knowledge. Umemeza madesa lakni umeshindwa kutranslate into real situation

Watu wanataka huduma ya afya Bora,Sio Bora huduma ya afya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom