johnmashilatu
JF-Expert Member
- Sep 16, 2010
- 718
- 703
Habari wana Bodi,
Ninachokishuhudia katika mwenendo wa watendaji pamoja na hali ya sasa ya mfuko wa Bima yà Afya, inakatishà tamaa yà kwanini mfuko huu unawafanyia hivi wateja wake?
Kabla sijaendelea naomba niweke jambo moja sawa.. watumishi wa umma Tanzania tambueni kuwa ninyi sio Miungu watu ni watumishi wao mmpo hapo na hali mliyonayo inatokana na sisi kuwagharamikia ninyi. Hivyo basi haiingii akilini kuwaona waajiri wako" hamnazo".
Malengo ya kupitishwa kwa sheria ya Bima ya Afya kwa wote kwa hakika yanaweza yasifikiwe kutokana na taratibu na au watumishi wasiofaa wa Mfuko wa Bima ya Afya.
Mifano yangu itajikita katika Hospitali ya Bugando. Hapa kwenye jengo la Bima wahudumu wake nafikiri wasiokuwa na taaluma ya Afya, waliwataka ndugu warudi nyumbani kumleta mgonjwa ambaye yuko kwenye hali isiyoridhisha na kuhitaji usafiri wa tax ili wamuone kabla ya kumuona daktari ambaye kwa siku hiyo alikuwa anakwenda kuwasomea ndugu majibu ya vipimo alivyochukua.
Mfano mwingine unanihusu mimi. Mgonjwa wangu mwenye bima inayoitwa ya vifurushi alifanyiwa upasuaji hospitalini hapo. Kurudi kwa ajili ya klinik, kwa daktari aliyemfanyia upasuaji na kumpangia siku ya kurudi, tunaambiwa na wàsimamizi wa mfuko kuwa, haiwezekani mpaka muanzie hospitali ya chini iwapatie rufaa ya kwenda Bugando.
Mimi sio tabibu lakini jambo hili haliingii akilini. Siamini kwamba mgonjwa aliyepata matibabu hospitali kubwa anastahili kurudi nyuma ili apewe rufaa na hospitali ya chini kurudi hospitali kubwa.
Kimbembe ni kupata hiyo rufaa, haina tofauti na kuingia na kukutwa ukiwa na mnyama pori! Hospitali ya chini kwa hapa karibu ni Sekou Toure, hawa wako radhi wakuandikie uende Muhimbili lakini sio Bugando.
Mbilinge hizi na nyingine nyingi za watumishi na taratibu zisizofaa za bima ya Afya, zimenipelekea Juzi 23/11 kulipia gharama za matibabu licha ya kuwa mwanachama wa Timiza Afya.
Kwa msingi huu, uliojengwa na taratibu zisizofaa za mfuko wa Bima ya Afya, nina pata mashaka kama haiwezi kuwa kikwazo kwa Bima mpya.
Kwa sasa kuna mambo machache ya kufanya ili kuhakikisha taratibu hizi zina koma.
1. Katiba ya JMT inapiga marufuku vitendo vya ubaguzi wa aina yoyote. Tunakusudia kuiomba mahakama kutoa tafsiri ya kitendo cha watumishi wa umma kuruhusiwa kutibiwa popote ilhali watanzania wengine ambao kimsingi wanachangia zaidi kuliko hao wa umma, wakizuiliwa.
2. Kuishauri hospitali ya Bugando kuwa Bima ya Afya ni muwezeshaji wa huduma hivyo hawezi na hana mamlaka ya kuqapangia taratibu za kutoa huduma.
3. Mashirika na taasisi zisizokuwa za kiserikali, msiangalie tu kuhamashisha watu wajiunge na mifuko hii, angalieni pia utendaji wake.