Aache upotoshaji: Universal Health Care haimaanishi Bima ya Afya. 'Universal Health Care Coverage' kwa Tanzania tuko 100% tangia enzi za Mwl. Nyerere

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
3,576
2,000
Huyu mgombea kila kukicha anawapotosha wananchi kwa kuwaeleza mambo ambayo si sahihi. Anaongea mambo ambayo hayajui na hana utalaamu nayo. Hana wataalamu wa kumshauri ukweli wa kile anachokusudia kuwaeleza wananchi.

Moja ya upotoshaji anasema ni kuwa akichaguliwa atawaletea watanzania wote Universal health care. Ukimsikiliza utagundua kuwa kwake universal health care maana yake ni bima ya taifa ya afya kwa wote. Utagundua kuwa bima ya afya yataifa kwake ni NIHF tu. Hajui kuwa kuna bima zingine za afya za taifa kama CHF, TIKA, SHIB ya NSSF na kadhalika. Hajui kwamba kuna makampuni binafsi zaidi ya saba nchini yanayotoa bima ya afya. Hajui kwamba hadi sasa mzigo mkubwa wa gharama ya matibabu ya watanzania bado unabebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi kwa ujumla (government revenue)

Ukweli ni kwamba:
1.
Universal health care a.k.a universal health coverage (UHC) is a health care system in which all residents of a particular country are assured access to health care. The World Health Organization describes it as a situation where all citizens of a particular country can access health services without incurring financial hardship.

Maana yake ni kwamba UHC ni mfumo wa serikali unaohakikisha raia wake wote wanapata huduma za afya. UHC ni sera ya nchi na mfumo wake unatekelezwa kwa kuundiwa sheria kanuni na taratibu za utekelezaji.

2. Tangia enzi za Mwalimu Nyerere raia wote wa Tanzania walikuwa wanapata huduma za afya bila kulipa chochote. Gharama zote zilibebwa na serikali kupitia mapato yake ya kodi (TRA) na yasiyokuwa ya kodi (government revenues). Sisi tuliyaita matibabu ya bure. Hivyo universal health care coverage ilikuwa 100% kwa gharama ya serikali ya 100% kupitia bajeti yake ya wizara ya afya.

3. Kufikia miaka ya 1990s, kutokana na ongezeko la watu (population) na ongezeko la gharama za tiba kufuatana na teknolojia za kisasa za tiba zenye gharama kubwa, serikali yetu (kama zingine duniani) ilielemewa na mzigo huu wa kutoa huduma bure kwa wote.
Hivyo kwa sababu hizo lakini bila kuathiri universal health care policy, serikali ilibadilisha kidogo mfumo huo kwa kuanzisha utaratibu wa health cost sharing kwa wale wenye kauwezo. Kwa utaratibu huu mgonjwa alitakiwa kuchangia asilimia kidogo ya gharama ya matibabu yake. Gharama kubwa ilibebwa na serikali.

Kwa wale ambao hawana uwezo kabisa wa kuchangia serikali iliweka utaratibu wa kuwasamehe. Makundi yafuatayo hayakusika na utaratibu huu wa cost sharing (hadi sasa): Watoto wote walio chini ya miaka mitano, mama wajawazito, wenye umri unaozidi miaka sitini, wenye magonjwa ya kansa, kifua kikuu, HIV na magonjwa mengine sugu. Hawa bado serikali inabeba gharama zao za matibabu kupitia bajeti yake ya walipa kodi wote nchini. Pia kwa magonjwa ya dharura mtoa huduma analazimishwa kutoa huduma kwanza, masuala ya kiasi gani mgonjwa achangie ataulizwa baada ya kupona na kama hatakuwa na uwezo huo utaratibu wasamaha utafuata baada ya kupona.

Hivyo hata baada ya kuanzisha cost sharing mfumo ulihakikisha universal health care kwa raia wote kwa serikali kubeba most of the cost. Ingawa kiwango cha hii cost sharing ya mgonjwa imekuwa ikiongezwa kidogo kidogo lakini hadi sasa burden kubwa bado inaendelea kubebwa na serikali. Kwa mfano gharama ya operesheni ya Caesarian Section huko Amerika ni USD 18,000 ambayo ni sawa na takribani Tsh 40 million lakini sisi hapa cost anayopaswa kuchangia mgonjwa haizidi Tshs 150,000/ na kama ni ya uzazi ni bure na kama hana uwezo anasamehewa au analipa kidogo ya hiyo. Inayobaki serikali inabeba kuhakikisha hakuna raia wake atakayekufa kwa kukosa uwezo wa kulipia gharama hizo. Hence 100% universal health coverage.

Dhana na chimbuko la bima za afya (Evolution of other health care financing in Tanzania):
Ili kurahisisha na kupunguza buguza/ changamoto ulipwaji wa hizo cost sharing kwa upande wa mgonjwa serikali iliunda bima za afya za taifa (public owned health insurance schemes:

1. The National Insuranse Health Fund (NIHF) ilianzishwa mwaka 1999 (Act of Parliament No. 8 of 199 -CAP 395 RE 2002) kwa ajili kwa waajiriwa wa serikali - government workers. Kila mwajirwa wa serikali alilazimika kukatwa 3% ya mshahara wake kila mwezi na serikali kutoa kiasi hicho hicho kutoka vyanzo vyake vingine vya mapato hivyo kupata 6% ya mshahara na kuuweka kwenye huo mfuko wa bima wa taifa. Mchango huo unamuwezesha mtumishi huyo pamoja na mwenza wake, watoto wao wasiozidi 4 wenye umri usiozidi miaka 18 na wazazi wake wawili - jumla watu sita kupata matibabu kwa gharama ya mfuko huo wa NIHF.

NB: - Waajiri na waajiriwa binafsi hawalazimiki kisheria kwa sasa kujiunga na mfuko huu. Ni wa hiari kwao.
- hulipa Shs 50,000 tu kwa mwaka kuwa wanachama wa mfuko huu.

2. Community Health Fund (CHF): Walengwa hasa wa mfuko huu ni wakazi wa vijijini. Ni mfuko wa hiari. Kila kaya hulipa Sh 10,000 tu kwa mwaka ambayo huwezesha mkuu wa kaya pamoja na watoto wao wote wenye umri chini ya miaka 18 kupata matinabu kwenye ngazi ya zahanati, kituo cha afya hadi hospitali ya wilaya bila mchango mwingine.

3. TIKA (Tiba kwa Kadi): Huu unafanana na ule wa CHF, tofauti hapa ni kaya zilizo mjini.

4. SHIB - ni Social health insurance benefit ulio chini ya National Social Scurity Fund (NSSF).

Ukiacha hizo mifuko aina 4 za bima za afya za kitaifa pia yapo makampuni zaidi ya saba yanayoendesha private health insuranses eg AAR, Strategy etc. Pia bima za maisha zinazotolewa na bima za kawaida huwa zina health insurance.

Mgombea huyo anapaswa kujua basics hizi badala ya kujifanya much know na kuanza kupotosha wananchi kwamba wataletewa UHC kutoka ubelgiji. Hiyo Obamacare haifiki ya kwetu kwa ubora na kwa coverage. UHC coverage ya kwetu bado ni 100%. Hakuna anayekosa matibabu au kufa kwa sababu hana pesa. Nchi zingine haziko hivyo.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,634
2,000
Hayo makundi yaliyosamehewa kwa kifupi yanaonekana ni mzigo kwa serikali ya CCM. Wazee wengi 75+ wanasema wakiugua wanawahi hospitali, kwenye foleni wanatengwa wanaambiwa wasubiri. Mpaka wale wenye Bima waonwe wote hapo ni saa 8 mchana ndiyo unaandikiwa paracetamol hata kama unaharisha.
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
832
1,000
Unaweza kuwa unajua kuelezea hivyo vitu vizuri sana lakini ile maana halisi huijui au unajaribu kupiga siasa. shida hapa ni kila mwananchi kupata huduma za afya kwa urahisi kabisa au bure kabisa. hayo uliyoelezea yanawezekana kwa watz wote leo?!? ni asilimia chache tu wana bima za afya tena wengi wao ni waajiriwa kwenye mfumo rasmi nao bado wanalalamika hiyo bima haitumiki kwa magonjwa yote. tuache politiki tufikirie kwa kujenga nchi
 

Incredible

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,022
2,000
Mimi ni Mtanzania ninaye ishi Canada. Universal Health care ni bima ya afya ambayo kila mkazi anapewa na serikali. Kwa miaka ambayo nimeiishi Canada, sijawi lipia matibabu wala familia yangu kulipia matibabu. Kusema ukweli gharama za elimu na matibabu ni cost za serikali. Tena kwa watoto gharama za elimu ni free mpaka school bus za kuwapeleka mashuleni na kuwarudisha. Nakuwekea maelezo hapo chini usome na nakuwekea na link yake.

Healthcare in Canada is delivered through the provincial and territorial systems of publicly funded health care, informally called Medicare.[1][2] It is guided by the provisions of the Canada Health Act of 1984,[3] and is universal.[4] Universal access to publicly funded health services is often considered by Canadians as a "fundamental value that ensures national health care insurance for everyone wherever they live in the country.

link;

Healthcare in Canada - Wikipedia
 

yanga2000

Senior Member
Sep 13, 2013
109
225
Universal health coverage is defined as ensuring that all people have access to needed health services (including prevention, promotion, treatment, rehabilitation and palliation) of sufficient quality to be effective while also ensuring that the use of these services does not expose the user the financial hardship.


For a community or country to achieve universal health coverage, several factors must be in place including: A strong, efficient, well-run health system that meets priority health needs through people-centred integrated care by: ... detecting health conditions early; having the capacity to treat disease; and.The guide aims to share specific tools to help you call on policy and decision makers to focus on improving any and all of the three pillars of Healthy systems for universal health coverage - a joint vision for healthy lives (joint vision): service delivery, health financing and governance.


Usijifanye unajua kumbe huna lolote....
 

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
286
1,000
Na: Mh Tundu Lissu

Pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii hazitajenga kiwanda chochote. Ni siasa tu. Pesa za mifuko ya hifadhi ya umma sio pesa za serikali, ni pesa za wafanyakazi. Zinatokana na makato yao ya mishahara. Serikali imekuwa inatumia pesa hizi kama zake, wakati sio zake. Pesa hizo zimetumika kujenga UDOM kwa makubaliano kwamba serikali hii ingerudisha pesa hizo kwa mifuko hiyo. Haijarudisha hata senti moja. Pesa hizo zimejenga jengo la Usalama wa Taifa OysterBay Dar.

Serikali haijarudisha hata senti moja kwa mifuko ilikochota pesa hizo. Pesa za mifuko zimejenga jengo la Machinga Complex Ilala Dar na nyumba za polisi Kurasini Dar. Serikali haijarudisha hata senti moja. Ndizo zilizojenga Daraja la Mwalimu Nyerere Kigamboni. You can rest assured haitarudi hata senti moja.

Ukweli, kama alivyosema CAG kwenye mojawapo ya taarifa zake za mwaka, mifuko ya hifadhi ya jamii ina hali mbaya ya kifedha. Hii ndio sababu wenye mamlaka wanataka kuondoa fao la kujitoa. Wameigeuza mifuko ya hifadhi ya jamii kuwa shamba la bibi mpaka mifuko inakaribia kufilisika. Sasa wanataka kuficha uchafu huu kwa blangeti la uzalendo uchwara. Wafanyakazi wa Tanzania wakikubali udanganyifu huu wataliwa kama ambavyo pesa zao zimeliwa kwenye miradi niliyoitaja.

Suala sio tuache siasa. Hatuwezi kuacha siasa. Suala ni tuache siasa za aina gani. Hawa wanasiasa wanaojivika uzalendo uchwara kuhusu hela za wafanyakazi wao wenyewe wametengenezewa utaratibu maalum ambapo wanakatwa na NSSF halafu baada ya kumaliza ubunge wanarudishiwa pesa zao.

Hawasubiri wafikishe miaka sitini ndipo wapate mafao yao ya kujitoa. Halafu wanawahubiria wafanyakazi wasubiri miaka sitini ndipo wapate mafao yao. Wana ndimi mbili kama za nyoka. Wafanyakazi wa Tanzania amkeni, hamna chochote cha kupoteza isipokuwa minyororo yenu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom