Kuna mdada mmoja aliolewa na jamaa mmoja handsome ana kazi yake na mkewe ana kazi yake, ila mkewe anapata mshahara mkubwa zaidi ya mkewe, dada wa watu alikuwa anajitahidi kuhudumia family including him, kwa kila kitu, jamaa akabweteka kabisa, mwisho wa siku akaanza kutembea na msichana wa jirani yao yaani alikuwa anakaa kwao, basi yule kaka akatafuta chumba na sebule akamweka yule dada, jamani mngemwona huyo dada wa nje alivo mbaya, mngeshangaa,mkewe mzuri maskini, yule mwanaume si akaanza kulala huko kwa mwanamke mara siku moja mara mbili, mpaka navyoandika hapa huyo mke bado anapata tabu na dhiki ya uke wenza, ila kipato anacho, sasa ukimwona hata huwezi jua kama ana pesa, kakonda kwa mawazo,kwa mimi ninavyowaza, mwanaume akikosa pa kuzitumia pesa zake anaweza fanya mambo ya ajabu sana, kama haya pia.hii ni story nayoijua na ni ya kweli.kwa hiyo wadada wenzangu kuweni makini sana na mambo kama haya