"A man should provide for his wife. PERIOD"

"A man should provide for his wife. PERIOD"

...my beliefs dearest darling,...

Mwanzo wa mapenzi, wengi wetu hufanya kosa la kuficha makucha kwa lengo la kutoonyesha mapungufu/misimamo yetu ili tusiwakwaze wale tunaowapenda. No wonder, baada ya miezi michache ya maisha ya pamoja, kucha zinapoanza kuota
utasikia maneno "zamani hukuwa hivyo!",..."siku hizi umebadilika!" etc...

Nilipoandika
naona shida kuacha moral values zangu, namaanisha inanibidi kuji adapt na moral values za Soulmate wangu
ili masikilizano yaimarishwe ndani ya nyumba. Tatizo ni pale personality zitapoanza ku clash...
mfano; mimi naamini una uhuru wa kujiamulia mambo fulani with the expectation unajua limits ya zuri na baya,
Lakini wewe kwa beliefs zako unaamini hapakuwa kosa kuzidisha uhuru zaidi ya uliopewa.

Iwapo Moral Values zangu zitakuwa compromised, zinanipelekea kwenye uncomfortable territories, jambo linaloniachia
machungu na maswali mengi kwanini sieleweki. Hoja ya Mkuu DC kuhusu kudumisha mila na desturi ili kuendelea kuwa mtawala, nimeichukulia kwamba inabidi nami nibadili hata kidogo mfumo wa maamuzi. Inabidi niwe muwazi zaidi nipate kueleweka nini ninachopenda, na nini nisichokipenda, na Consequenses zake ili mwenzangu nae aelewe.
Aksante umenielewesha vizuri sana nimekuelewa.
Very interesting!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Na mimi ndo ninavyojua, maisha ya mapenzi ni kushirikiana, kusikilizana, kuheshimiana, kujaliana tatizo letu wanawake tunapenda tujaliwe sisi tu, kushirikiana hatutaki, eti sio jukumu letu, nadhani mapenzi kwa baadhi ya wanawake yaangalia vitu sana

Umesema kweli shost saa ingine nasi tunachangia sana kwa hawa wababa kuwa hivi. Ninavyoamini mie huwa kuna mwanzo wa kila kitu...na inawezekana kabisa wakati wa mwanzo baba alikuwa anaprovide tena na vya ziada! Lakini baadhi yetu hufikia kuona kuwa ....nimemweka kiganjani.. tunabweteka miguu juu, hata kama unazo ukiambiwa mama chumvi imekwisha unajibu ..subiri baba enyu akirudi...huku unavaa kandambili zako mbio saluni!!

Kisha tena haya umeletewa, hata shukrani, neno aksante na sauti ya puani hakuna, ndio kwaaanza unamwangalia mume anaingia na kifurushi chake mpaka anakuletea hapo ulipokaa.na bado hunyooshi mkono ukapokea, unamnyooshea kidevu aweke juu ya meza. kisha wasubiriiii mpaka unagutuka ah nlisahau kumbe kuna kifurushi..haya tena ushakifungua umeona kilichomo hukukipenda waanza kitolea kasoro, ..oh ungeleta rangi ya samawati, kama ni dhahabu basi we unaropoka bora ungenunua kwa Kasmani ili mradi huonyeshi shukrani!..... wadhani kesho bwana atarudia kuleta?! Inaanza zawadi na mwisho matumizi .
 

LOL!...Rev. Masanilo...yaani hukumsoma DC, na wengineo wote na hoja zao nzito nzito
umeonelea u connect the dots kwa Moskwito tu?...ama Malaria haikubaliki! ha ha ha...
 

LOL!...Rev. Masanilo...yaani hukumsoma DC, na wengineo wote na hoja zao nzito nzito
umeonelea u connect the dots kwa Moskwito tu?...ama Malaria haikubaliki! ha ha ha...

Hapana Kaka mimi husoma maandishi magumu Ukutani.....!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kweli kabisa Mbu. Mimi nafanya kazi tena ya maana tu kwa nini niwe tegemezi 100%. Kwenye familia yangu wote ni watafutaji na pesa si yangu wala ya mume wangu, ni yetu sote. Kwa hiyo mimi hapa naona kama watu wanaongea kichina tu. Yes wazazi wetu walitegemea baba kuwa ni provider kwa kuwa those days wamama walikuwa wanakaa nyumbani kufanya kazi za home. Sasa mimi na elimu yangu na kazi yangu nzuri bado nitegemee mume anihudumie. Well as a woman I love receiving gifts and of course I do. Ila gharama za maisha ni zetu sote and am proud that I can contribute a lot to making my family enjoy modern life.



...mimi maswali yangu manne iwapo mwanaume anastahiki ku 'provide for his wife'

1. kwa kiwango gani?...kwa kila kitu? au kwa yaliyo makuu i.e Nyumba, Chakula, Mavazi, na Matibabu.
2. kwa muda gani? mume akiwa mzima au ugonjwa, mume akiwa kijana au mzee
3. mwanamke abakie (full-time) mama wa nyumbani? ...kwakuwa pesa yake haihitajiki, ruksa alee watoto tu?
4. kipato chake (mke) kitafsiriwe vipi?

...nachelea tafsiri ya maamuzi haya 'compared' na mila, desturi na tamaduni za makabila/utaifa.
Kwetu 'Mwambao' yanawezekana sana haya. Mke anashinda ndani kulea watoto, kujifukiza udi nk...
'Unyamwezini' mume na mke wote wanapiga matuta!...Sijui kule kwa 'Wakurya' kukoje...!
 

LOL!...Rev. Masanilo...yaani hukumsoma DC, na wengineo wote na hoja zao nzito nzito
umeonelea u connect the dots kwa Moskwito tu?...ama Malaria haikubaliki! ha ha ha...
Mchungaji amekonsentreti na posts zako wakati mi niko busy na signecha ya mjukuu mtiifu.

......
.
Said I loved you but I lied, This is more than what I fee Inside
 
Ndiyo nashangaa. Na hii inanifanya niamini wasemao wanawake wengi ni selfish.

hivi mapenzi ni nini, na ndoa ni nini, mbona wanawake wenzangu mna element za utegemezi jamani, yaani pesa yako ni yako peke yako, ya mwenzio ya wote,halafu unasema unampenda, hivi kwenye mapenzi kuna mtu anatakiwa amgharimie mwenzie au sijui maana ya mapenzi
 
Mchungaji amekonsentreti na posts zako wakati mi niko busy na signecha ya mjukuu mtiifu.

......
.
Said I loved you but I lied, This is more than what I fee Inside
.......Mh Babu hebu acha hizo wewe ni wa kushtushwa hapa wakati mahari ulishakula na kusahau?! Bora Mchungaji akishangaa ntaelewa! Mwone vile
 
Mchungaji amekonsentreti na posts zako wakati mi niko busy na signecha ya mjukuu mtiifu.

......
.
Said I loved you but I lied, This is more than what I fee Inside

...hivi wewe Babu!, ....hiyo fee uliyoiainisha hapo maana yake ada? mahari? mchango? au?....
halafu,....nikishatoa mahari, makazi, malazi, chakula, mavazi, na matakataka mengine,...kisha huyu mjukuu wako
aka 'laaziz chokileti wa moyoni mwangu' anambie eti watoto tisa wanatosha, pataeleweka kweli?

Itabidi anizalie timu nzima mahari yangu na gharama zirudi!

 
katelero;2217899]hivi mapenzi ni nini, na ndoa ni nini, mbona wanawake wenzangu mna element za utegemezi jamani, yaani pesa yako ni yako peke yako, ya mwenzio ya wote,halafu unasema unampenda, hivi kwenye mapenzi kuna mtu anatakiwa amgharimie mwenzie au sijui maana ya mapenzi

Mkuu unaweza badili hili jina lako?

Kila nikiwaza Katelero narekebisha Jiografia ya suruali yangu. Niombi tu......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom