"A man should provide for his wife. PERIOD"

"A man should provide for his wife. PERIOD"

Nyie wanaume wadekezeni tu hao wake zenu. Siku mkifutwa kazi au kutangulia mbele za haki watoto wenu watawakumbuka sana maana life itawabadilikia in a month. Hata kama mkeo ni mama wa nyumbani familia itakuwa assured kama mama ni mtafutaji.
 
mwanajamiione mie kipato changu cha msimu, nikikosa najifanya mgonjwa nahudumiwa na mamaa lkn sasa kimbembe nakionaga, naambiwa maneno wewe, mara utasikia mwanaume suruari wewe, mwanaume sura wewe maana sura zetu za kiume kweli, makovu kote kote, na mwisho utasikia kile kicheko chenu kile cha bwana weee hapo ni kutoka kwa mpangaji mwenzangu akiwa anasikiliza taarabu "Utalijua jiji", nikizipata nakaribishwa acha utadhani mbunge vile.......
 
To my experience mwanamke mtafutaji anaheshimiwa sana na mmewe. Kwa hiyo hata siku moja hajawahi demand huduma ambayo ni nje ya uwezo wangu. Nikisema nje ya uwezo wangu nina maana including kuchoka. Mme wangu hana tabia za kiboss. But I do lots of works may be than many housewives. Mme wangu hafui nguo wala hapiki. Nampa heshima zote ambazo mwanaume wa kiafrika anapenda kupewa. Ila hana nyodo za kusema ooh sili alichopika h/girl si mtu wa masharti. Nikiwa nyumbani nafanya kazi nikiwa kazini anafanya H/girl that's obvious. Week days sipiki, week ends napika. Anataka nini tena zaidi ya hilo. Kwa ufupi siishi kwa masharti tunaishi kama lovers and equal partners.

Anyway wakati tunatafuta wenza maishani nadhani tunaangalia tunataka nini. What I have is what I needed. Napenda ku exercise some degree of independence and authority and my man has no problem with that and I knew he wont be a problem that's why I fell in love with him.

Hongera mamito kila mwanamke lazima ajishughulishe ,vipi kuhusu yale majukumu yetu tunayolalamikiwa kila siku unaweza vipi kucopy nayo hapo hapo ukitoka pasu na mzee kwenye majukumu mengine.
Unampa mwenza wako nafasi yake au ndo zile za stong na independent woman zinajitokeza kila mkikwaruzana mbona nahisi harufu ya ubabe kwenye post yako.
 
Oh Samahani ninamaanisha kuuliza hivi; baada ya kusoma majibu yako na ufafanuzi mzuri kwenye Imani, ndo nikaomba kujua
Bila samahani, una haki ya kujua na kukielewa kile ambacho unataka kukielewa.
1. Mtu (mwanaume) ambaye anatakiwa kuifuata Imani hii, akawa hayatimizi hayo uliyoyaainisha hapo juu, atatafsiriwaje?
Huyu mtu atakuwa anakwenda kinyume na haki za mke wake. Kisheria mke anapaswa kumshtaki kwenye vyombo vya sheria ili kupata haki yake.
2. Kuna wale wanaoshindwa kutimizia familia zao kwa sababu tu hali ya maisha haimruhusu (hana kazi au kazi yake ni kipato kidogo kukidhi mahitaji) na kuna wale wenye kipato lakini anaamua tu kutofanya kwa sababu anajua kuwa mkewe ana uwezo.
Kwa wale ambao kipato chao ni kidogo basi amesameheka na kama mke anao uwezo basi kibinadamu anapaswa kumsaidia mume wake katika kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha.

Na wale wenye uwezo lakini hawataki tu kwa jeuri watakuwa wanakwenda kinyume, kama hapo juu, nilivyo elezea.
 
Pheewww, Jazzakallah!...nimeisoma hiyo. Shukran.
Naomba tuliache hilo la imani nyingine, tusijeharibu topik ya mamaa hapa,
kuna atheists, hindus, sikhs, christians, rastafaris, pagans etc humu...

Haya, nasubiria umjibu Mwj1 nami nije na swali la nyongeza.
Naomba basi uni PM, maana nina kiu ya ilmu hii.
 
Mwanamme kumtimizia mwanamke mahitaji yake ya kila siku, bila kuzidi kipato chake, ndio sahihi. Lakini haitakiwi wanawake tubweteke kungoja kupewa tu. Inabidi na sisi tufanye kazi kwa bidii na tusiwe tegemezi kwa kila jambo letu.
Thats my girl... She is lovely
 
Maisha ni kusaidiana, nitasaidiana na mume wangu kwa hali na mali. Maisha ni kupanda na kushuka na daima nitapenda kuwa flexible kutokana na situation za maisha..

laa, sitojisikia raha mwanaume wangu kuhangaikia familia kwa kujinyima wakati na mimi nina salary halafu naitunza benki au kuwa mchoyo(mbinafsi).

Nitajitahidi pia kwa kila hali awe na azidi kuwa kichwa cha familia kwa kumheshimu na kumpa sapoti!..!
 
Bila samahani, una haki ya kujua na kukielewa kile ambacho unataka kukielewa.Huyu mtu atakuwa anakwenda kinyume na haki za mke wake. Kisheria mke anapaswa kumshtaki kwenye vyombo vya sheria ili kupata haki yake.Kwa wale ambao kipato chao ni kidogo basi amesameheka na kama mke anao uwezo basi kibinadamu anapaswa kumsaidia mume wake katika kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha.Na wale wenye uwezo lakini hawataki tu kwa jeuri watakuwa wanakwenda kinyume, kama hapo juu, nilivyo elezea.
Aksante ksana kaka kweli nimeelimika
 
Maisha ni kusaidiana, nitasaidiana na mume wangu kwa hali na mali. Maisha ni kupanda na kushuka na daima nitapenda kuwa flexible kutokana na situation za maisha..

laa, sitojisikia raha mwanaume wangu kuhangaikia familia kwa kujinyima wakati na mimi nina salary halafu naitunza benki au kuwa mchoyo(mbinafsi).

Nitajitahidi pia kwa kila hali awe na azidi kuwa kichwa cha familia kwa kumheshimu na kumpa sapoti!..!

Pheeeewwww,...BJ nice one...yaani hiki ni kiapo kabisa ambacho 'shemeji' anatakiwa a print, afanyie lamination na
kutundika ukutani.

Ubarikiwe sana.
 
Bila samahani, una haki ya kujua na kukielewa kile ambacho unataka kukielewa.
Huyu mtu atakuwa anakwenda kinyume na haki za mke wake. Kisheria mke anapaswa kumshtaki kwenye vyombo vya sheria ili kupata haki yake.
Kwa wale ambao kipato chao ni kidogo basi amesameheka na kama mke anao uwezo basi kibinadamu anapaswa kumsaidia mume wake katika kukabiliana na hali ngumu ya kimaisha.

Na wale wenye uwezo lakini hawataki tu kwa jeuri watakuwa wanakwenda kinyume, kama hapo juu, nilivyo elezea.

...lahaula, hapo nasikia harufu ya Ustawi wa Jamii! ...wale wakishakuamulia % ya Child and Maintenance benefit ujue imekula kwako mwanaume. Mwisho wa mwezi unakwenda kusaini "Nil Poix" Salary Slip!
 
Maisha ni kusaidiana, nitasaidiana na mume wangu kwa hali na mali. Maisha ni kupanda na kushuka na daima nitapenda kuwa flexible kutokana na situation za maisha..laa, sitojisikia raha mwanaume wangu kuhangaikia familia kwa kujinyima wakati na mimi nina salary halafu naitunza benki au kuwa mchoyo(mbinafsi).Nitajitahidi pia kwa kila hali awe na azidi kuwa kichwa cha familia kwa kumheshimu na kumpa sapoti!..!
BJ ubarikiwe Mwali na Mungu akutangulie katoka kuyatimiza yapasayo kutimizwa na mke mwema
 
...lahaula, hapo nasikia harufu ya Ustawi wa Jamii! ...wale wakishakuamulia % ya Child and Maintenance benefit ujue imekula kwako mwanaume. Mwisho wa mwezi unakwenda kusaini "Nil Poix" Salary Slip!
Kama uyataki hayo yakukute, basi timiza wajibu wako.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kama uyataki hayo yakukute, basi timiza wajibu wako.

XP, kuna mahala uligusia mke anaweza fidia pale penye mapungufu, lakini ukweli kwa Muongozo wa kidini na kiserikali
halazimiki kufanya hilo. Je,....ikitokezea hitilafu hiyo, ilhali mwanaume umekwama kabisa...nini suluhisho juu ya hilo?

mfano; watoto wamesimamishwa shule sababu ada imekosekana, kodi ya ngumba ishakushinda,
chakula ndani hakieleweki, nk...lakini wakati huo huo Mke anaenda kazini Asb, anarudi jioni, Jibu lake ni moja tu
"WEWE NDIYE BABA, TIMIZA WAJIBU WAKO.!"

pls dont mention kukopa,....nazungumzia alternatives 'zote' zimekauka.
 
mwanajamiione mie kipato changu cha msimu, nikikosa najifanya mgonjwa nahudumiwa na mamaa lkn sasa kimbembe nakionaga, naambiwa maneno wewe, mara utasikia mwanaume suruari wewe, mwanaume sura wewe maana sura zetu za kiume kweli, makovu kote kote, na mwisho utasikia kile kicheko chenu kile cha bwana weee hapo ni kutoka kwa mpangaji mwenzangu akiwa anasikiliza taarabu "Utalijua jiji", nikizipata nakaribishwa acha utadhani mbunge vile.......

Duh jamani huyo wifi naye mtata.........mwe ah kwa staili hiyo Magu sikusemi maana nlitaka nikugombeze kwa nini ukichacha husemi ukweli unadanganya but mh......I zip my lips!

Ah halafu hayo maneno mbona kama ni wanawake ndo wanayatumia sana kusimangia?! Sijawahisikia mwanaume akimsimanga mkewe kuwa ni golikipa ingawa hadithi hizi nshzisikia kitambo.
Mh mapenzi yaacheni yaitwe mapenzi yamejaa wingi wa viroja
 
XP, kuna mahala uligusia mke anaweza fidia pale penye mapungufu, lakini ukweli kwa Muongozo wa kidini na kiserikali
halazimiki kufanya hilo. Je,....ikitokezea hitilafu hiyo, ilhali mwanaume umekwama kabisa...nini suluhisho juu ya hilo?

mfano; watoto wamesimamishwa shule sababu ada imekosekana, kodi ya ngumba ishakushinda,
chakula ndani hakieleweki, nk...lakini wakati huo huo Mke anaenda kazini Asb, anarudi jioni, Jibu lake ni moja tu
"WEWE NDIYE BABA, TIMIZA WAJIBU WAKO.!"

pls dont mention kukopa,....nazungumzia alternatives 'zote' zimekauka.
Mbu, hivi kuna mwanamke jabari na mwenye moyo wa jiwe kiasi ya kuona watoto wake wa kuwazaa wakiteseka hali ya yeye uwezo anao wa kuwasaidia?

Hivi inawezekana kweli?

Hapo juu kwa muongozo wa serikali, sheria inasemaje? Ebu fanya rejea kwanza kwenye sheria ya serikali inasemaje.

...mmnhh, Mwj1 una habari muongozo huo wa kiimani unashabahiana sana na muongozo wa kiserikali (Sheria ya Ndoa Tanzania?) ....Bahati mbaya, kina mama wengi hawajui haki zao kisheria...

chunguza.

PART IV PROPERTY, RIGHTS, LIABILITIES AND STATUS (ss 56-68)​
63. Duty to maintain spouse​
Except where the parties are separated by agreement or by decree of the courtand subject to any subsisting order of the court–(a) it shall be the duty of every husband to maintain his wife or wives and to providethem with such accommodation, clothing and food as may be reasonable having regard to his means and station in life;
(b) it shall be the duty of every wife who has the means to do so, to provide insimilar manner for her husband if he is incapacitated, wholly or partially, from​
earning a livelihood by reason of mental or physical injury or ill-health.

Mwenzenu najisikia kuburudika tu leo............... hii ni special kwa MwanajamiiOne

Last edited by a moderator:
Duh jamani huyo wifi naye mtata.........mwe ah kwa staili hiyo Magu sikusemi maana nlitaka nikugombeze kwa nini ukichacha husemi ukweli unadanganya but mh......I zip my lips!

Ah halafu hayo maneno mbona kama ni wanawake ndo wanayatumia sana kusimangia?! Sijawahisikia mwanaume akimsimanga mkewe kuwa ni golikipa ingawa hadithi hizi nshzisikia kitambo.
Mh mapenzi yaacheni yaitwe mapenzi yamejaa wingi wa viroja

Unadhani anyesema hiyo nani? shoga ake mke wangu...kumbe nikichacha huwa wanaambizana......ujue pia kuoa wa dar sometimes kasheshe...
 
Nyie wanaume wadekezeni tu hao wake zenu. Siku mkifutwa kazi au kutangulia mbele za haki watoto wenu watawakumbuka sana maana life itawabadilikia in a month. Hata kama mkeo ni mama wa nyumbani familia itakuwa assured kama mama ni mtafutaji.

nyumba kubwa yaani mie huwa nasema namwuomba sana MUNGU anipe ufahamu pamoja na maarifa basi! maisha ya ndoa peke yako kwa kujifanya wajua ni magumu. Shangazi yangu mie alikuwa wa hivyo, nyumba ya shirika, watoto wawili wanasoma, kodi za umeme, maji n.k alikuwa hata hajui ni kiasi gani hulipwa........akiulizwa anasema mume wangu injinia......... (Utafikiri ni injinia pekee Tanzania!) mama mwisho wa mwezi ye anazungumzia akanunue Bazee la bei gani, lesi material ya aina gani maghorofani wamtambue! mama haya kushauri ....baba tufungue kigrosari basi mume wangu ah....ila kila jioni anatoka anakaa kwenye glosari ya shoga yake anampigia simu mjomba atamkuta hapo.....shughuli inaanza kunywa hadi sita usiku. Wanarudi............... wanakujatahamaki maghorofa yameuzwa, shirika limefilisika, injinia yuko juu ya mawe anabangaiza na kazi za wahindi,....kiwanja kilinunuliwa kisukulu enzi hizo mama akasema ni mbali sana, nani akae porini kikauzwa! .........................sasa wamepanga na mama anazikumbuka pesa za Bazee na Lace material.
 
Back
Top Bottom