uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Chief Kabikula

    GE2020 Siku Tano mgombea Urais wa CCM hafanyi kampeni, Kulikoni?

    Kimya kimetanda siku tano nzima mgombea urais wa CCM Hafanyi kampeni, hii mbona inaathiri ratiba yake alitakiwa awe Iringa hajaenda, hizi siku atazifidia vipi? Badala yake anasikika yuko Dodoma anakutana wakurugenzi? Vipi jamani upepo unamuendeaje? Nasikia anaandaa timu mpya baada ya Polepole na...
  2. K

    GE2020 Mgombea Urais kukutana na wasimamizi wa uchaguzi kipindi cha Kampeni inakubalika kisheria?

    Zipo taarifa za Mwenyekiti wa chama tawala kukutana na wakurugenzi Dodoma wakati kampeni zinaendelea huku Hawa wakiwa ndio wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo. Tume ya uchaguzi inazungumziaje hatua hii? Je Ni kweli mkutano huu upo au Ni propaganda za majukwaani tu? Serikali imekanusha...
  3. K

    Sheria ya uchaguzi inasemaje juu ya mawakala wa vyama vya siasa?

    Nawaombeni Ndugu zangu mnieleweshe juu ya Sheria ya Uchaguzi inasemaje juu ya mawakala ya Vyama vya Siasa kwenye vituo vya kupigia kura. Leo nimemuona mgombea fulani wa Chama fulani akisema kuwa hakitaeleweka kuhusu mawakala wao kama hawataapishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliwasimamie kwenye...
  4. Z

    Baada ya uchaguzi, Lissu jiandae kuunda chama chako

    Ndani ya CHADEMA ni kama hairuhusiwi kusikika kuliko Mbowe. Sasa naangalia meseji za sifa kwa Lissu, nikilinganisha na zile zilizokwishamwagwa kwa Mbowe wakati huu, ni wazi Jina la Lissu linatamkwa sana. Hapa JF mashabiki wa CHADEMA wanahaha kila kona. Kusema hivi simchongei Lissu kufukuzwa...
  5. J

    GE2020 Shibuda alia ukata unamfelisha kufanya kampeni, amtaka Rais Magufuli awatumbue wasimamizi wa Uchaguzi waliovurunda!

    Mgombea urais wa JMT kupitia upinzani mzee John Shibuda amesema vyama vingi vya upinzani vimekwama kuendelea na kampeni kwa sababu ya ukata. Kadhalika Shibuda amemtaka Rais Magufuli kuwatumbua wasimamizi wa uchaguzi waliovurunda wakati wa uteuzi wa wagombea ubunge na udiwani. Chanzo: ITV...
  6. kavulata

    Kuna maisha baada ya uchaguzi kupita, tuwekeni akiba ya maneno na vitendo

    Hata iweje maisha yataendelea baada uchaguzi kumalizika na bila kujali matokeo ya Uchaguzi yatakuwaje. Wadau wote wa uchaguzi, yaani Wanasiasa, wagombea, ofisi ya msajili, Tume ya Uchaguzi, Askari, wasimamizi wa uchaguzi, wahesabu kura, mawakala na wapigakura tukumbuke muda wote kuweka akiba ya...
  7. Prof Koboko

    GE2020 Sababu ni kwanini Rais Magufuli atashindwa sana uchaguzi huu

    Hili tumekua tukilisema sana humu mara nyingi. Sababu kubwa Rais Magufuli kushindwa na Wapinzani tena kwa kura nyingi sana ni Ugumu wa maisha aliousababisha yeye na serikali yake. Watu wote nchi nzima wanalia na maisha magumu mzee hasikii kabisa. Mzee amekimbilia kuanzisha miradi mikubwa...
  8. J

    Ernest Nyanda wa Star TV, mnapojadili Sheria za Uchaguzi waalike wanasheria mahiri. Usizoe tu wachambuzi wa mitaani, wanakufelisha!

    Kilichonishangaza leo katika mjadala wa Star tv Tuongee asubuhi, mada ikiwa " Muungano wa vyama vya siasa wakati wa uchaguzi " ni kwamba wageni wote wawili waliotambulishwa kama wanasheria wameshindwa kutupa tofauti kati ya Muungano na Ushirikiano. Wamesisitiza kuwa penye ushirikiano lazima...
  9. Miss Zomboko

    GE2020 Prof. Lipumba: Uchaguzi huu usiwe chanzo cha uvunjifu wa amani. Tume ya Uchaguzi itende haki

    Mgombea urais kwa tiketi ya CUF Prof. Ibrahimu Lipumba, amesema uchaguzi huu usiwe chanzo cha uvunjifu wa amani ya Tanzania. Lipumba ametoa kauli hiyo leo septemba 24, mwaka huu kwenye mkutano wake wa hadhara wa kuomba kura katika uwanja wa changalawe uliopo mjini Kayanga wilaya ya Karagwe...
  10. Lord Denning

    GE2020 Kwanini huu ndio Uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM?

    Amani iwe nanyi wadau Kama mada inavyojieleza hapo juu, hizi ndo sababu za Kwa nini Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ndo uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM? 1. Mwaka 2015 Chadema walikuwa na mgombea aliyependwa na watu Lowassa Ila hakuwa mgombea makini CCM waliweza kumchafua sana Lowassa kutokana na...
  11. J

    Mahakama ya Kisutu yaahirisha kesi za Tundu Lissu kupisha Uchaguzi Mkuu

    Mahakama ya Kisutu imeahirisha kesi mbili zinazomkabili Tundu Lissu hadi baada ya uchaguzi mkuu mwezi Novemba. Tundu Lissu anagombea urais wa JMT kupitia CHADEMA. Chanzo: ITV habari Maendeleo hayana vyama! ===== Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia kesi mbili zinazokabili Mgombea Urais...
  12. lembu

    Sheria inasemaje akifariki mgombea?

    Hivi akifariki mgombea wakati wa kampeni sheria inasemaje wadau? Chama kina ruksa ya kumuweka mwingine au ndio imetoka? Akifariki mgombea urais? Akifariki mgombea ubunge? Akifariki mgombea udiwani?
  13. desmond JJ

    GE2020 Tujikumbushe kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 28 Oktoba, 2020

    TUJIKUMBUSHE MAMBO MBALIMBALI KWA MUJIBU WA MIONGOZO YA NEC Wajibu wa Vyama vya siasa wakati huu wa kampeni ni kunadi sera kwa kuzingatia Sheria za Uchaguzi,Kanuni na Maadili ya Uchaguzi. Kama inavyoelekezwa katika kifungu cha 51 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha...
  14. P

    GE2020 Tuungane Kumwombea Tundu Lissu ili ashinde Uchaguzi hapo Oktoba 28

    Karata nyingine ya ushindi kwetu ni kuungana na kuomba ili mpenda haki na amani, mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu aweze kushinda kwa kishindo hapo Oktoba 28. Huu ni wito kwa watakatifu wote, wapenda haki, wapenda amani, wapenda usawa, na wapenda kweli kuungana na kumwombea Lissu...
  15. Q

    GE2020 Karata ya mwisho ya CCM ni kuahirisha uchaguzi na sio kuiba kura

    CCM ilianza mapema kutafuta kura, ilianza na mbinu ya kuzuia vyama vingine na wagombea wao kujitangaza akabaki Magufuli peke yake, ikaja na mbinu ya kununua wapinzani waliyoshauriwa na Polepole na KM Bashiru, CCM ikautumia uchaguzi wa serikali za Mitaa kuwahujumu wapinzani. CCM walijua wagombea...
  16. Subira the princess

    GE2020 Hizi si dalili njema kuelekea Oktoba 28

    Wasalaam, Kitendo cha tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoka haraka kukemea makusudio ya vyama vya upinzani kushirikiana katika uchaguzi huu ni cha kibaguzi hakikubaliki. Sababu iliotolewa na NEC ni dhaifu na ni dhahiri ni kuitetea CCM, eti wananchi watachanganyikiwa siku ya uchaguzi na eti...
  17. YEHODAYA

    GE2020 CHADEMA na ACT-Wazalendo wanadai uchaguzi wa haki wakati Wagombea Urais wao hawajawatendea haki

    CHADEMA kupitia vikao halali kabisa vya kikatiba walimteua mgombea urais wao wa Zanzibar. Lissu anahubiri haki lakini alipofika Zanzibar akaanza kumnadi Mgombea Urais wa ACT-Wazalendo. Haki ya Mgombea wake akaitupa kwenye dustbin. ACT-Wazalendo nayo inahubiri haki ikamteua Membe kuwa mgombea...
  18. Mystery

    Tetesi: Nafasi zote zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi za kusimamia Uchaguzi kushikwa na makada wa CCM!

    Zimetolewa hadharani kwa kila mtanzania mwenye sifa, aombe nafasi hizo za muda za kusimamia uchaguzi hapo October 28 mwaka huu, lakini taarifa za uhakika nilizozipata ni kuwa nafasi hizo muhimu, ambazo ni za watanzania wote, bila kujali itikadi zetu za kisiasa, hivi sasa hawa CCM, wamepanga...
Back
Top Bottom