Uchaguzi 2020 Namna ya kudhibiti uwepo wa vituo hewa/bubu vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu - 2020

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,535
Ndugu zangu wana JF;

CCM wamejiapiza kuwa John Pombe Magufuli ni lazima ashinde tu uchaguzi huu wa mwaka huu either by hooks or by crooks..

Wagombea wa CCM katika ngazi zote ikiwemo ya Urais, kwa utaratibu wa kawaida kama wakiachwa hivi hivi bila kusaidiwa kushinda kwa njia haramu za wizi wa kura, kwa hakika kabisa ni wachache sana wana uwezo wa kushinda katikati ya ushindani huu..

Kwa upande wa Urais, Magufuli hawezi kushinda kabisa, kabisa, kabisa..

Hili kila mtu anajua, wao CCM wanajua, wapambe wao kwenye mitandao kina Bia yetu, Nawatafuna, USSR, elitwege na wengine wanajua na Magufuli mwenyewe anajua kuwa hawezi kushinda bila kutenda dhambi ya wizi..!

SASA WANAFANYAJE ILI KUSHINDA?

1. Wanatengeneza karatasi za kupigia kura za ziada. Zinatiwa tick (√) kwa Magufuli. Zinakuwa kura zisizo halali..

Tetesi zinasema kuwa kuna karatasi za kura za namna hii zaidi 5,000,000 zimeandaliwa na kusambazwa nchi nzima..!!

2. Kutengeneza au kuandaa vitu vya kupigia kura visivyo rasmi maarufu kama hewa au feki. Lengo la vituo hivi ni kupitishia hizo kura zisizo halali ili ziwe halali sawa na zingine zitakazopigwa na wapiga kura rasmi..

3. Kuandaa wapiga kura wasio rasmi (ghost voters) na mbinu za kuwaingiza vutuoni kupiga kura zitaandaliwa na kusimamiwa kikamilifu. Ndiyo kuna sehemu zingine wanafunzi wa shule za sekondari walishawekwa tayari..

4. Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ambao karibu 95% ni watumishi umma i.e walimu, manesi, maafisa ugani, watendaji vijiji/mitaa nk kupewa maelekezo maalumu kuwezesha kufanikisha zoezi hili muhimu la "kumshindisha John Pombe Magufuli" awe Rais tena..

Hawa watumishi, wameambiwa na kutishiwa kuwa kama kituo atakachosimamia itaonekana Tundu Lissu (CHADEMA) ameongoza kura kumzidi John Pombe (CCM), basi ajihesabu hana ama amejifukuzisha kazi..!!

NINI KIFANYIKE KUDHIBITI/KUPAMBANA NA HUJUMA NA MIKAKATI YA WIZI HUU WA KURA?

Ni rahisi sana..

Ni kuihamasisha NGUVU YA UMMA kuamka na kulinda HAKI YAO, MAAMUZI YAO..

Ni kuhakikisha wananchi wanajengewa awareness miongoni mwao ili wawe tayari kwa mapambano kulinda maamuzi yao..

Hata hivyo, hizi ni njia za jumla (universal) za kupambana na uhalifu huu dhidi ya demokrasia na uhuru wa watu wa kuchagua..

1. Kila mgombea wa udiwani (katika kata yake) na ubunge (katika jimbo lake) ahakikishe kuwa, ana orodha ya vituo halali vyote vya kupigia kura vilivyotolewa na kuidhinishwa na Tume ya uchaguzi pamoja na code number zake..

2. Kila mgombea ahakiki uwepo wa vituo hivyo kimoja baada ya kingine katika kata yake...

3. Kila mgombea udiwani na ubunge awe na orodha ya NEC ya vituo vyote vya kupigia kura katika kata ama jimbo lake siku ya majumuisho ya kura katani (kwa udiwani) au kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo - makao makuu ya halmashauri husika (kwa ubunge na Urais)..

4. Kila mgombea udiwani ama ubunge awe makini sana hatua kwa hatua siku ya majumuisho ya kura pale katani au kwa DED kwa sababu kitakuwa kinatajwa kituo kimoja baada ya kingine na idadi ya kura kwa kila mgombea..

Ikitokea anataja kituo cha kupigia kura ambacho hakiko kwenye orodha uliyonayo wewe iliyotolewa na NEC, moja kwa moja mnamkamata pale pale hadi athibitishe uhalali wa kituo hicho na kwanini hakipo kwenye orodha halali ya NEC..

5. Kila mgombea udiwani au ubunge ahakikishe kuwa kila kituo cha kupigia kura katika kata ama jimbo lake kuna wakala aggressive asiyeyumbishwa. Na ahakikishe kuwa anapata nakala ya fomu ya matokeo ya kura za kituo (udiwani, ubunge na Urais) kama ushahidi..

6. Kila mgombea udiwani na ubunge ahakikishe anazo na anaenda na fomu zote za matokeo ya kura kwa kila kituo siku ya majumuisho ya kura kwa msimamizi wa uchaguzi katani (udiwani) au jimbo (ubunge)..

Kama haya yatazingatiwa, wezi watadhibitiwa na washindi halali wa uchaguzi wa mwaka huu watatangazwa tu..!!
 
Kama kweli Kuna mpango wa kuinginza kura hewa wakukamilisha zoezi Hilo wajipange maana sidhani Kama ukikamatwa na wananchi utabaki salama maana naona kwenye jamii watu wanahasira Sana, Jana tu nikiwa kwenye daladala ilianza Kama utani watu wawili wakitaniana mmoja upande wa ccm mmoja upande chadema ghafla haukua utani Tena manusla wa ccm atandikwe makofi na abiria na konda akaingilia Kati kwamba hataki siasa kwenye gari lake.

So huu mwaka watu Wana hasira Sana , Wasimamizi wa vituo ,Kama ni mwalim n.k usijitoe ufaham,kisa eti utaachishwa kazi ,uhai muhim kuliko kazi msikubali ujinga ambao waweza kuwaletea madhara makubwa Bora kujitoa Hali sio nzuri wananchi Wana hasira Sana,

Kama kunampango wa kuchelewesha mawakala wa upinzani ,sisi tuko mitaani nyie mpo ofisin ila muelewe mpango huu ni hatari Yani mnaenda chomoa betri kwenye tank la mafuta, sisi tuna sema ,Sasa mkiziba masikio,sawa tutalia wote ,na tutapata shida wote ,hakuna aliesalama tz kwanza
 
Safari mtaandika vitabu naona mnaandika insha yakeyale ya 2015 ohhh tumeibiwa kura ukiambiwa onyesha hata kituo kimoja ukichoibiwa kura kipi mkabaki mnatoa mimacho tu

Sasa mko vituo hewa!!! Viko wapi hamonyeshi lakini kelele kibao

Mumeshaona mnashindwa mnahaha
Safari hii kipigo mtakachopata upinzani sanduku la kura muandae kabisa madaktari wa pressure sababu lazima ziwapande na wengine mzimie
 
Ktk mapambano haupaswi kumdharau adui yako hata km mbinu zake zote unazijua kwa sabab inawezekana Kuna mengine huyajui,waliotuletea democrasia ndio haohao wanaosisitiza kura Ni siri ya mpigaj tunapaswa kujua inawezekana mtu ambaye unayeamin yupo upande A akampigia kura upande ambao huwez utarajia ktk huu mchezo hakuna neno lazima tunaangaliaga uwezekano hususan kwa upinzan.
 
Mkuu upo sawa kabisa na Mungu akwamishe mbinu zote ovu! Sasa hapo juu umeeleza njia mbili za wizi wa kura zilizoandaliwa na mashetani wa demokrasia yetu kuwa ni;

1.Ni zile kura zaidi ya 5 milion zitakazopenyezwa kupitia vituo hewa.

2.Wanafunzi wa Sekondari wameshaandaliwa kuingizwa kupiga kura za CCM.

Sasa hapo juu umeonyesha mbinu na njia za kuthibiti hiyo mbinu ya kwanza tu ya vituo hewa! Vipi na hawa wanafunzi ambao wamepewa umri wa wazee wa mwaka 1949 au 1953, wathibitiwe vipi?

Maana kama wataruhusiwa kuingia kupiga kura vituoni, hata mgombea akienda kwenye majumuisho bado hesabu itabaki palepale!
Je tuzuie vipi mamluki hao wasifanye uharamia huo?? Mie nafikiri jambo ni moja tu kuzuia uchaguzi usifanyike, mpaka dosari hizo zote ziondolewe!
 
Ndugu zangu Vituo hewa vimetapakaa Nchi nzima vimevizidi hata Vituo vya Petroli ijiandae mapema kuvivumbua
 
Jamaa unaandika uwongo mwepesi sana,hata ushahidi ukuweka!!.

Alafu ujaeleza kwenye majumuisho ya kura za udiwani,Ubunge na Urais hizo kura za vituo hewa zitapenyezwaje,ilhali mawakala wakuu wa majumuisho wana nakala za matokeo za kila kituo cha kupigia kura na Ballot box zipo mbele yao wanaziona huku majumisho yakiendelea.
 
Kama kweli Kuna mpango wa kuinginza kura hewa wakukamilisha zoezi Hilo wajipange maana sidhani Kama ukikamatwa na wananchi utabaki salama maana naona kwenye jamii watu wanahasira Sana, Jana tu nikiwa kwenye daladala ilianza Kama utani watu wawili wakitaniana mmoja upande wa ccm mmoja upande chadema ghafla haukua utani Tena manusla wa ccm atandikwe makofi na abiria na konda akaingilia Kati kwamba hataki siasa kwenye gari lake
So huu mwaka watu Wana hasira Sana ,
Wasimamizi wa vituo ,Kama ni mwalim n.k usijitoe ufaham,kisa eti utaachishwa kazi ,uhai muhim kuliko kazi msikubali ujinga ambao waweza kuwaletea madhara makubwa Bora kujitoa Hali sio nzuri wananchi Wana hasira Sana,
Kama kunampango wa kuchelewesha mawakala wa upinzani ,sisi tuko mitaani nyie mpo ofisin ila muelewe mpango huu ni hatari Yani mnaenda chomoa betri kwenye tank la mafuta, sisi tuna sema ,Sasa mkiziba masikio,sawa tutalia wote ,na tutapata shida wote ,hakuna aliesalama tz kwanza

Umesema vyema kabisaa watu wanahasira na ile roho ya WoGa hamna.

Nimeshuhudia maeneo Mengi watu wanasubiri polisi walianzishe watu wajibu mapigo.

Nashauri CCM waibe Kura kistaarabu sio kuiba wazi wazi italeta machafuko.
 
Ndugu zangu wana JF;

CCM wamejiapiza kuwa John Pombe Magufuli ni lazima ashinde tu uchaguzi huu wa mwaka huu either by hooks or by crooks..

Wagombea wa CCM katika ngazi zote ikiwemo ya Urais, kwa utaratibu wa kawaida kama wakiachwa hivi hivi bila kusaidiwa kushinda kwa njia haramu za wizi wa kura, kwa hakika kabisa ni wachache sana wana uwezo wa kushinda katikati ya ushindani huu..

Kwa upande wa Urais, Magufuli hawezi kushinda kabisa, kabisa, kabisa..

Hili kila mtu anajua, wao CCM wanajua, wapambe wao kwenye mitandao kina Bia yetu, Nawatafuna, USSR, elitwege na wengine wanajua na Magufuli mwenyewe anajua kuwa hawezi kushinda bila kutenda dhambi ya wizi..!

SASA WANAFANYAJE ILI KUSHINDA?

1. Wanatengeneza karatasi za kupigia kura za ziada. Zinatiwa tick (√) kwa Magufuli. Zinakuwa kura zisizo halali..

Tetesi zinasema kuwa kuna karatasi za kura za namna hii zaidi 5,000,000 zimeandaliwa na kusambazwa nchi nzima..!!

2. Kutengeneza au kuandaa vitu vya kupigia kura visivyo rasmi maarufu kama hewa au feki. Lengo la vituo hivi ni kupitishia hizo kura zisizo halali ili ziwe halali sawa na zingine zitakazopigwa na wapiga kura rasmi..

3. Kuandaa wapiga kura wasio rasmi (ghost voters) na mbinu za kuwaingiza vutuoni kupiga kura zitaandaliwa na kusimamiwa kikamilifu. Ndiyo kuna sehemu zingine wanafunzi wa shule za sekondari walishawekwa tayari..

4. Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura ambao karibu 95% ni watumishi umma i.e walimu, manesi, maafisa ugani, watendaji vijiji/mitaa nk kupewa maelekezo maalumu kuwezesha kufanikisha zoezi hili muhimu la "kumshindisha John Pombe Magufuli" awe Rais tena..

Hawa watumishi, wameambiwa na kutishiwa kuwa kama kituo atakachosimamia itaonekana Tundu Lissu (CHADEMA) ameongoza kura kumzidi John Pombe (CCM), basi ajihesabu hana ama amejifukuzisha kazi..!!

NINI KIFANYIKE KUDHIBITI/KUPAMBANA NA HUJUMA NA MIKAKATI YA WIZI HUU WA KURA?

Ni rahisi sana..

Ni kuihamasisha NGUVU YA UMMA kuamka na kulinda HAKI YAO, MAAMUZI YAO..

Ni kuhakikisha wananchi wanajengewa awareness miongoni mwao ili wawe tayari kwa mapambano kulinda maamuzi yao..

Hata hivyo, hizi ni njia za jumla (universal) za kupambana na uhalifu huu dhidi ya demokrasia na uhuru wa watu wa kuchagua..

1. Kila mgombea wa udiwani (katika kata take) na ubunge (katika jimbo lake) ana orodha ya vituo vyote vya kupigia kura vilivyotolewa na kuidhinishwa na Tume ya uchaguzi pamoja na code number zake..

2. Kila mgombea ahakiki uwepo wa vituo hivyo kimoja baada ya kingine katika kata yake...

3. Kila mgombea udiwani na ubunge awe na orodha ya NEC ya vituo vyote vya kupigia kura katika kata ama jimbo lake siku ya majumuisho ya kura katani (kwa udiwani) au kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo - makao makuu ya halmashauri husika (kwa ubunge na Urais)..

4. Kila mgombea udiwani ama ubunge awe makini sana hatua kwa hatua siku ya majumuisho ya kura pale katani au kwa DED kwa sababu kitakuwa kinatajwa kituo kimoja baada ya kingine na idadi ya kura kwa kila mgombea..

Ikitokea anataja kituo cha kupigia kura ambacho hakiko kwenye orodha uliyonayo wewe iliyotolewa na NEC, moja kwa moja mnamkamata pale pale hadi athibitishe uhalali wa kituo hicho na kwanini hakipo kwenye orodha halali ya NEC..

5. Kila mgombea udiwani au ubunge ahakikishe kuwa kila kituo cha kupigia kura katika kata ama jimbo lake kuna wakala aggressive asiyeyumbishwa. Na ahakikishe kuwa anapata nakala ya fomu ya matokeo ya kura za kituo (udiwani, ubunge na Urais) kama ushahidi..

6. Kila mgombea udiwani na ubunge ahakikishe anazo na anaenda na fomu zote za matokeo ya kura kwa kila kituo siku ya majumuisho ya kura kwa msimamizi wa uchaguzi katani (udiwani) au jimbo (ubunge)..

Kama haya yatazingatiwa, wezi watadhibitiwa na washindi halali wa uchaguzi wa mwaka huu watatangazwa tu..!!
Yaani hizi nguvu ungetumia kuhamasisha wapiga kura, kutangaza Sera za chama chako, mngeweza hata kupata asilimia 3 ya kura zote!
 
Back
Top Bottom