Uchaguzi 2020 Je, wajua kura yako inaweza kuamliwa na msimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata au Jimbo endapo itaonekana ina mgogoro na kuhesabika kuwa ni halali?

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,682
3,065
Tunapoelekea mwishoni mwishoni kuelekea uchaguzi mkuu hapo tarehe 28.10.2020
Ni bora tujikimbushe namna ya upigaji kura wetu.
Kazi yetu kubwa sisi wapiga kura ni kwenda kuwapigia kura wagombea tuliowakubali kwa sera zao binafsi,chama chao na Ilani zao zitakavyotekelezwa kwa miaka 5 mingine.

Basi nawaomba kuwambusha wapiga kura wenzangu
Alama hizi za upigaji kura zitahesabika moja kwa moja bil kutiliwa shaka yoyote.
Alama no:
1.(✔) halali
2.(✖) itahesabika halali
3.()✔ itahesabika halali
4.()✖itahesabika halali
Kura hizo zitakubaliwa kuwa ni halali.

Kura yenye utata.
Kura ambayo itakuwa na mgorogo ni ile mpiga kura ambayo atapiga tick kwa wagombea wawili au zaidi ya wawili ila msimamiz wa uchaguz(kata au jimbo) anao uwezo wa kuamua kwamba lengo la mpiga alitaka kumpigia nani ?
Mfano umetick kwa Lisu lakini ikapitiliza hadi kwa Hashimu Rungwe basi msimamizi ataamua kura yako ulilenga kwa mgombea yupi ilianzia wapi ataamua kuwa ni halali na ihesabike kuwa ni ya mgombea flani.

Kwa nini hii inaweza kutokea .
Hii inaweza kutoa endapo msimamizi wa ktuo pamoja na mawakala watashindwa kuafikiana kuwa kura hiyo ilimlenga nani ,msimamizi wa kituo atamplekea msimamizi wa uchaguzi ngazi ya kata ,akikishindwa kuamua atamplekea wa ngazi ya jimbo na ndo atakuwa mwamuzi wa mwisho kufanya uamuzi.

Aidha mpiga kura anaweza kurudia kupiga kura pale anapoona ameharibu kabla hajaitumbukiza kwenye sanduku la kura.

Tuwe makini sana katika upigaji kura wetu.
Ahsanteni sana.
Tukachague viongozi tuanaowataka huku tukiwaomba NEC kutenda HAKI na kusimamia sheria.

Aidha tuwaombe wafuasi wetu wasiende na Matokeo.
Kwangu mimi nitampigia mpenda HAKI ,mpenda AMANI mfuata SHERIA ,mleta KATIBA MPYA.
Ahsanteni.
 
Mambo ya Kisheria kama haya huambatana na kunukuu Vifungu vya Sheria tofauti na hapo ni Porojo na Soga za Vijiweni
 
Uchaguzi uliopita mazwazwa ya Edlow yaliaribu kura nyingi sana,yanaweka tiki vizuri kabisa kwa mamvi ama mgombe anaemtaka,alafu kwa JPM au mgombea wa CCM anamkata uso kwakuweka X au anamtoboa macho.
 
1603355296705.png
 
Mambo ya Kisheria kama haya huambatana na kunukuu Vifungu vya Sheria tofauti na hapo ni Porojo na Soga za Vijiweni
Hadi moderator kuruhusu uzi huu ambao ni nyeti na mhimu kwa umma amejidhihirisha kuwa ni kweli.
Ukitaka vifungu tafuta kitabu cha mwongozo wa uchaguzi wa wasimamiz wa Uchaguzi.
 
Back
Top Bottom