Uchaguzi 2020 Waraka maalum kwa wananchi kabla ya Uchaguzi

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,457
1,442
Ninawiwa kuandika waraka wangu binafsi kwa waTanzania kuhusu umuhimu wa kupiga kura na kuchagua mgombea ngazi zote kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo:
1. Binafsi mimi nitapiga kura lakini nimetafakari na kuamua kumpigia kura mgombea mwenye kujitambua na anayejali maslahi ya wananchi na nchi kwa ujumla
2. Mgombea asiye na harufu zozote za rushwa, ufisadi na ambaye hata kwenye jamii ni mwadilifu
3. Mgombea mwenye utashi wa kisiasa kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wake bila ubaguzi na nikiunganishi cha makundi yote
4. Chama Chenye Uongozi imara na kinachoweza kutuongoza kwa kulinda umoja, amani na tulivu endelevu tulionano kama taifa
5. Chama chenye historia ilyotukuka na sera nzuri na mipango inayotekelezeka

Wananchi tumebakiza siku 7 za kujitafakari mengi yamesemwa wakati wa kampeni na kila mgombea ni juu yetu kuchuja sera,mipango na maelezo yote yaliyotolewa. Hivyo yatupaswa tuwe makini kipindi cha miaka mitano ni kirefu kosa moja linaweza kutugharimu. Sisi ni taifa huru lenye kujitambua Mungu atuongoze kutupa hekima kuchagua anayetufaa ili taifa hili liendelee kustawi.TUCHUJE NA KUAFAKARI BILA JAZBA AU MIHEMKO ILI TUPATE VIONGOZI BORA NA SIYO BORA VIONGOZI.

Kuhusu Wagombea ninashauri wakubaliane na matokeo ili mradi iwapo hakubaliani sheria za nchi zifuatwe katika kuipata haki yao. Aidha, Tume na Wasimamizi wa Uchaguzi wanaaswa watende HAKI ili kuondoa sintafamu na uvunjivu wa amani na vyombo vya Dola visimamie kwa kuzingatia sheria na kwa weledi na Mataifa ya nje yasiingilie uchaguzi ili ufanyike kwa kuzingatia sheria, matakwa desturi na katiba ya nchi.MUNGU IBARIKI TANZANIA!Moderators uzi huu ni muhimu kwa umma kama kumbusho kablaya uchaguzi usomwe na kila mtu bila kuzngatia itikadi.
 
Back
Top Bottom