uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. K

    Dkt. Fomunyo aitaja Tanzania kama miongoni mwa nchi ambayo demokrasia yake imeteteleka

    Dkt. Christopher Fomunyoh, ambaye ni Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa shirika la National Democratic Institute (NDI) ambalo linafanya kazi kusaidia na kuimarisha taasisi za kidemokrasia ulimwenguni kupitia ushiriki wa raia, uwazi na uwajibikaji serikalini, ameelezea hali ya kudhorota na kurudi...
  2. funaku

    GE2020 Ubalozi wetu nchini Marekani utoe tamko kwa ajili ya mwenendo wa Uchaguzi Marekani

    Ni muhimu ubalozi wa Tanzania Nchini marekani ukatuwakilisha vyema kwa kutoa tamko rasmi la jinsi mwenendo wa uchaguzi unavyoendelea nchini Marekani. Ni muhimu kuwaasa wagombea urais huko marekani kuacha kutupiana maneno bali wanadi sera zao.
  3. lee Vladimir cleef

    Tanzania mabingwa wa kutetea Haki nchi za nie na kulinda Amani. Na Uchaguzi uwe huru, uwazi na haki

    Tangu tupate Uhuru na tangu zama za Mwalimu Nyerere Tanzania ilijitoa kupigania Haki kwa nchi zote zilizokua zikionewa hapa duniani. Sio tu nchi kuonewa bali hata jamii yoyote kuonewa Tanzania iliitetea jamii hiyo. Sio tu nchi na au jamii, bali pia hata mtu binafsi alipokua akionewa huko kwao...
  4. T

    GE2020 Uchaguzi huru na haki unaanzia kwenye kampeni, Polisi TZ pamoja na NEC, anzeni kumshughulikia mgombea urais kupitia CCM

    Uchaguzi huru na wa haki unaanzia kipindi cha kampeni, lakini tunaona uoendeleo wa wazi kwa CCM. Mgombea wake Magufuli kila anapopita anaomba kura kwa vitisho lakini hakuna anayehoji iwe ni NEC ama Polisi. CCM imeshirikiana na vyama vingine lakini hakuna aliyewakemea ila ikitokea upinzani...
  5. D

    GE2020 John Magufuli wa CCM anakiuka sheria ya maadili ya uchaguzi waziwazi. Naziomba jumuiya za kimataifa zimchukulie hatua kali sana

    Mimi ni muumini wa usawa kwenye uchaguzi. Tumeshuhudia huko duniani mamlaka zikiingia kwenye uchaguzi mkuu huku wakijitahidi kuweka usawa. Kwa Tanzania mwaka huu tumefeli na tunajichafua kwelikweli. Sasa basi, kabla taifa zima halijachafuliwa kutokana na huu upuuzi anaoleta mgombea aa CCM...
  6. desmond JJ

    GE2020 Uchaguzi utakuwa wa haki na uwazi – NEC

    Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Uchaguzi utakaofanyika Tarehe 28 Oktoba, 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye kuzingatia uwazi kwa mujibu wa sheria. Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mstaafu Mhe. Mbarouk S. Mbarouk alipokuwa akihutubia Mkutano wa Wadau na Asasi...
  7. S

    GE2020 Uchaguzi huu hatutaki kusikia sera, tunahitaji mwendo mdundo wa kuing'oa CCM

    Wacha CCM wazungumzie sera mpaka washikwe na presha, huku upinzani ni kampeni za kuisaga CCM na kuonyesha uovu wake wote na hawastahili kuongezwa hata dakika moja. Waende mitaani na sera zao za ajabu ajabu wanampigia mbuzi gitaa, wananchi walio wengi tumechoka na sera na mikakati hio hio kila...
  8. beth

    Uchaguzi wa Marekani 2020: Vatican yamkatalia Mike Pompeo kuonana na Papa Francis

    Vatican imemkatalia waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo kuonana na Papa Francis. Kiongozi huyo wa juu wa Kanisa Katoliki ameelezwa kuwa hawapokei wanasiasa wakati wa kipindi cha uchaguzi. Hatua hiyo inaongeza hali ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kauli ya Bwana Pompeo kuhusu China...
  9. Q

    GE2020 Lushoto, Tanga: Wananchi wamkataa na kumfukuza mgombea wa CCM, Shabani Shekilindi (Boznia)

    Sasa ni dhahiri kwamba hali ya wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya urais hadi udiwani ni ngumu. Inasemekana huyu ni mgombea ubunge wa CCM jimbo la Lushoto Mjini Bosnia amekataliwa wazi wazi bila chenga na wakazi wa jimbo lake. ====== Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shabani...
  10. L

    Mapendekezo ya Tume ya Uchaguzi kwa Tume ya Katiba

    Wakati Tume ya Katiba ya judge Warioba ikikusanya maoni ya wadau mbalimbali nchini, Tume ya Uchaguzi iliweka wazi kwamba haipo huru na ikashauri ipewe uhuru wake ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na kuweza endesha chaguzi ambazo zitakuwa free, fair and credible. Rasimu ya katiba mpya...
  11. S

    Kwanini Polisi wanawapiga mabomu wananchi, katika msimu huu wa hekaheka za uchaguzi?

    Kwa kweli msimu huu wa uchaguzi ni kama sherehe katika nchi ,kwa wananchi wengi kujichagulia kiongozi wao kutoka chama kitakachobahatika kupaa kura nyingi kihalali au kimipango. Sasa inakuwaje polisi wanaonekana kubeba upande mmoja kwa visingizio vya kijinga sana,hata Afande wao mkubwa nafikiri...
  12. D

    GE2020 Vurugu zilizoanza kuibuka Uchaguzi Mkuu: Balozi mpya wa Marekani nchini Tanzania atema cheche

    Haya bwana msome mwenyewe alichonena hapa.
  13. This is...

    Tuweke uwanja sawa wa kampeni. Mambo ambayo Dkt. Magufuli na wapambe wake wamefanya yanayokiuka maadili ya Uchaguzi na NEC wako kimya..

    Tumemsikia Mkurugenzi wa NEC akitoa tuhuma dhidi ya mgombea urais wa chadema kwamba anakiuka maadili ya uchaguzi, lakini hatujamsikia akiongelea upande wa pili wa Dkt. Magufuli. Sisi kama wananchi tumeshuhudia matendo yanayokiuka maadili ya uchaguzi yanayofanywa na Dkt. Magufuli kwa uchache...
  14. kavulata

    Tume ya Uchaguzi ifanye nini ionekane ipo huru?

    Wapo wanaodhani kuwa Tume haiko huru na Kuna wanaoamini iko huru. Wale wasioamini kuwa Tume iko huru kipi Tume ifanye ili ionekane iko huru?
  15. Kibanga Ampiga Mkoloni

    GE2020 Ujue Muundo na Mamlaka ya Kamati na kamati ya Rufaa ya Maadili ya Uchaguzi

    Kwa mujibu wa GAZETI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA la Tarehe 5 Juni, 2020 SEHEMU YA TANO Ukururasa wa 14. Angalia Kiambatisho. 5.2.2 Kamati ya Kitaifa Itakuwa na mamlaka ya kusikiliza malalamiko ya ukiukwaji wa maadili kwenye uchaguzi wa Rais na Rufaa kutoka Kamati ya Jimbo. Kamati...
  16. B

    One love wimbo wa Bob Marley ndio ulionikuna kwenye Uchaguzi huu, Lissu alifikiria nini?

    Wakuu huu wimbo Tundu Lissu alijifikiria nini kwenda nao katika kampeni? Kiukweli umenigusa sana hasa hiyo mistari niliyobold ina maana kubwa sana. Tundu una akili sana na napenda unavyojua kuucheza. One love One heart Let's get together and feel alright (hear the children crying) One love...
  17. K

    GE2020 Tume ya Uchaguzi (NEC): Tundu Lissu amepelekewa barua ya kuitwa na Kamati ya Maadili

    Kwa huu mtihani kabambe ambao jopo la watendaji wa Tume wakiongozwa na Majaji wenye weredi wa kutosha kushindwa kutafsri kanuni za uchaguzi na hatimaye Tindu lissu kuibuka kidedea kwa kuwapa darasa ambalo limekuwa funzo kwa Tume na kwa wagombea wengine. Hii ni dhahili tosha kwamba huyu jamaa...
  18. Erythrocyte

    Dar es Salaam: Gharama za kujifungua ni Tshs 75,000. Uchaguzi huu unakupa nafasi ya kukataa uharamia huu

    Wajawazito wanaojifungulia kwenye Hospitali ya Rufaa ya Temeke , wale wanaojifungua kwa njia ya kawaida inawalazimu kulipia pesa taslimu ya kitanzania shilingi elfu 75 kama gharama ya kuzaa , Wale wanaojifungua kwa njia ya upasuaji wanapaswa kulipa zaidi ya Tsh laki 2 na yaweza hata kufika...
  19. B

    GE2020 NEC yatangaza Nchi na Taasisi zilizoruhusiwa kuwa watazamaji (Observors) wa Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

    29 September 2020 Arusha, Tanzania Source: video : Global online TV TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia kwa mkurugenzi wake, Dkt Willson Mahera, leo Septemba 29, wamezungumza na wanahabari na ili kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mnamo Oktoba 28...
  20. OLS

    GE2020 NEC wanavyoajiri Wasaidizi wa Uchaguzi wanatambuaje wanayemuajiri sio mshabiki wa chama cha siasa?

    Waungwana katika kupambana tunajua zikitokea fursa huwa tunazichangamkia kwa nguvu sana. Kila mwaka wa uchaguzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi huwa inatoa nafasi za kazi za muda mfupi ili kusaidia shughuli za uchaguzi. Ni wazi kuwa kwa miaka mingi kazi hizi zimekuwa zikiwa njia sahihi ya walimu...
Back
Top Bottom