Anasema mwaka 2008, akiwa Msaidizi wa Rais Kikwete, alikuwa ziarani Makete. Alikuwa anatumia gari na dereva wake wa Ikulu, aliyeazimwa kutoka Jeshini. Jioni moja, kuna document ya Rais alitaka aifanyie kazi na kumpelekee kesho yake saa 1:00 asubuhi. Akamwambia dereva amfuate saa 12:30 asubuhi...