Nilitoa mahari mwaka jana mwezi Desemba. Lakini mpaka leo sijafuata jiko langu

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Ndo hivyo wakurugenzi.

Mwaka jana nilikuwa na nia kabisa ya kitaka kuoa kutokana na upole, unyenyekevu, heshima na adabu aliyokuwa nayo huyo binti licha ya uzuri na rangi yake

Mahari yenyewe haikuwa kubwa kiasi hicho, ni 300k tu. Niliitoa kiutani utani nikisindikizwa na ndugu pamoja na marafiki wenye hulka ambao wao tayari wamekwisha oa. Ndoa ilitakiwa iwe mwishoni mwa Januari. Lakini katikati ya Januari, mke mpya wa jirani yangu alimmwagia mumewe maji ya moto baada ya purukushani zilizotokea jioni hiyo. Chanzo eti ni fumanizi la kwenye simu

Baada ya hapo nilianza kupata tetesi za etu wanawake wapole na wakimya huwa wanatunza vinyongo, lakini siku wakiripuka, wanaweza kukuua huku wanacheka. Jumlisha zile kataa kataa ndoa za humu jukwaani na matukio kedekede. Hiyo siku sikulala usiku, nikaanza kutafakari namna ambavyo ninaenda kujitwisha mzigo mzito wa kumiliki kiumbe ambacho kimeumbwa na Mungu kwa akili na udongo mwingi sana, nikajikuta naona naingilia majukumu yasiyonihusu, nikaanza kukwepa

Nilitamani maneno na matarajio ya ndugu, jamaa na marafiki yapotee vinywani mwao lakini wapi. Ndugu wengine wenye shobo walinunua maandalizi madogo madogo bila kumsahau Mjomba Bwena ambaye alinunua tairi la gari ili aje anikabidhi kama zawadi kwenye harusi yangu ili nikamilishe vifaa vingine liwe gari kamili

Baada ya hapo nilisingizia kuwa nahitaji kusoma IT kwa ajili ya kazi zangu binafsi ili wanipatie muda. Nikahama hata pale nilipokuwepo. Siku nilipomuonesha dada yangu mahali nilipohamia, nikawa nimeyabananga. Wakwe wakaanza kutengeneza misururu. Sasa hivi wananisumbua eti nioe ili mdogo wake na mke wangu mtarajiwa aolewe maake keshapata bwana

Nimejaribu kuzungumza nao kwa mafumbo kuwaeleza kuwa sina wazo la kuoa, kama ni issue ya mahari mimi nishasamehe, lakini ndio kwanza wanatafsiri eti "Wiki ijayo mambo yatakuwa mwemwere mwemwere

Nifanye nini kuukimbia huu msala ndugu zanguni?
 
Aisee kuna ndugu yetu alitoa mahari ya 2m+, mwanamke wake akaanza kuleta jeuri, mara anafanya mambo ya ajabu, jamaa machale yakamcheza, akaamua kuchomoa waya, akawaambia mahari ameisamehe, haoi. Aisee hawakuamini upande wa mwanamke, sasahivi anaendelea na maisha yake full kujimwaga.
 
Ndo hivyo wakurugenzi.

Mwaka jana nilikuwa na nia kabisa ya kitaka kuoa kutokana na upole, unyenyekevu, heshima na adabu aliyokuwa nayo huyo binti licha ya uzuri na rangi yake

Mahari yenyewe haikuwa kubwa kiasi hicho, ni 300k tu. Niliitoa kiutani utani nikisindikizwa na ndugu pamoja na marafiki wenye hurka ambao wao tayari wamekwisha oa. Ndoa ilitakiwa iwe mwishoni mwa Januari. Lakini katikati ya Januari, mke mpya wa jirani yangu alimmwagia mumewe maji ya moto baada ya purukushani zilizotokea jioni hiyo. Chanzo eti ni fumanizi la kwenye simu

Baada ya hapo nilianza kupata tetesi za etu wanawake wapole na wakimya huwa wanatunza vinyongo, lakini siku wakiripuka, wanaweza kukuua huku wanacheka. Jumlisha zile kataa kataa ndoa za humu jukwaani na matukio kedekede. Hiyo siku sikulala usiku, nikaanza kutafakari namna ambavyo ninaenda kujitwisha mzigo mzito wa kumiliki kiumbe ambacho kimeumbwa na Mungu kwa akili na udongo mwingi sana, nikajikuta naona naingilia majukumu yasiyonihusu, nikaanza kukwepa

Nilitamani maneno na matarajio ya ndugu, jamaa na marafiki yapotee vinywani mwao lakini wapi. Ndugu wengine wenye shobo walinunua maandalizi madogo madogo bila kumsahau Mjomba Bwena ambaye alinunua tairi la gari ili aje anikabidhi kama zawadi kwenye harusi yangu ili nikamilishe vifaa vingine liwe gari kamili

Baada ya hapo nilisingizia kuwa nahitaji kusoma IT kwa ajili ya kazi zangu binafsi ili wanipatie muda. Nikahama hata pale nilipokuwepo. Siku nilipomuonesha dada yangu mahali nilipohamia, nikawa nimeyabananga. Wakwe wakaanza kutengeneza misururu. Sasa hivi wananisumbua eti nioe ili mdogo wake na mke wangu mtarajiwa aolewe maake keshapata bwana

Nimejaribu kuzungumza nao kwa mafumbo kuwaeleza kuwa sina wazo la kuoa, kama ni issue ya mahari mimi nishasamehe, lakini ndio kwanza wanatafsiri eti "Wiki ijayo mambo yatakuwa mwemwere mwemwere

Nifanye nini kuukimbia huu msala ndugu zanguni?
Hiyo mahari ya laki tatu 300,000 utakuwa umeoa binti wa mikoa ya pwani! Jiandae na ngoma za mdundiko na vigodoro
 
Pole kwa muolewaji yani unabadilisha maamuzi yako kisa ndoa ya jirani na maneno ya kataa ndoa za jf, hao kataa ndoa wa jf una uhakika awajaoa mkuu.
 
Hahahaaa maji ya moro yanayolainisha viazi ndio yanafanya yai liwe gumu

Ww bado mtoto sanaaa, kuna wenzio walijinga na ukimwi kila mwanamke lazima apime ndio apige show lkn akaumwa na kipindu pindu asubui na jioni akafa, akazikwa na masispaa bila maiti yake kuombewa dua ya mwisho.

Ikiwa bint hana shida yeyote owa kwa maana wakati huu nia bora sana kwako kuliko wakayi unaokuja ambao haujui utakuwa nani na wapi. Acha kuowa kwa sbabu bint au familia ya upande wa kikeni kuna changamoto lkn kama hakuna owa kaka.
 
Unaogopa hata Bado hujakaa naye

Wewe sema tu umepata mwingine

Na wazi tu kuwa umeghaili kuoa wakupige faini
Umsake huyo unayemuona anafaa
 
Pole kwa muolewaji yani unabadilisha maamuzi yako kisa ndoa ya jirani na maneno ya kataa ndoa za jf, hao kataa ndoa wa jf una uhakika awajaoa mkuu.
Kwahiyo unataka kutusingizia kwamba tumeoa?. Anachotakiwa kufanya ni kuwafungulia nyuzi za kataa ndoa ukweni wajue sababu halisi na waone cha kufanya juu ya mtoto wao
 
Back
Top Bottom