maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,146
Barabara ya Kimara hadi Kibaha ilijengwa kwa kasi kubwa hadi tukasema shkamoo chama tawala. Oyaoya mara lakutokea likatokea na hapo ndio ikawa mwisho wa mwanzo wenye kasi. Miaka mitatu sasa hata street lights tu za solar wameshindwa kumalizia, mwendokasi wanaisoma namba kwenye foleni na barabara yao wanaiona ila hawana namna. Matumaini yanazidi kufa kila ukifika Kimara kuelekea ubungo baada ya kukutana na foleni kali kuanzia stop over, na unabaki unashangaa kivipi barabara 3 zinakua finyu tena kuelekea mjini. Anyway wabongo akili zishaanza kukaa sawa