Kama stress za mapenzi zingekuwa zinaua ungekufa mwaka gani?

Eti kama hizi stress za mapenzi zingekuwa zinaua wewe ungekuwa marehemu tangu mwaka gani?

Aah yaani mimi ningekufa mwaka jana yaani ningekuwa sasa hivi nimebaki mifupa ila Alhamdulillah hazijaniua zimenifanya tu kuwa sugu.
Kwa wanaume stress za mapenzi hazina nafasi kubwa maana ni wepesi kuvuta chombo kipya kuziba pengo.

Kinachowaponza wanawake ni kusubiri atongozwe badala ya kuchukua hatua chap
 
ningekufa enzi Niko kidato chatatu.kunademu nilikuwa nampenda hadi tukikutana siwezi kufumbua mdomo kumwambia nabaki kama kunamtu amenishika mdomo nisweze kuufumbua daa

nikienda kutesti kwawingine mambo safikabisa nikienda kwake nashikwa nakigugumizi kizito
basi usiku silali namuwaza tuu nikiona mtumwingine kasimamanae natamani alzi ipasuke kwawivu

chakushukuru alihama mtaaule nakwenda mkoa mwingine ndio nikapona mdogo mdogo.

hadi leo bado sijaona mwanamke wakunichanganya kwakweli.

sasa hivi nikikosa kuingiza kiasichangu chapesa kila siku ndio silali kwamawazo.
 
Ahh wapiii. Ya nini usumbuke? Nyenzo hizo si nyingi tuuuu! Ikizengua,tupilia mbali. Hakikisha hutoi hela kabla hujaosha.
 
Mwaka huu tarehe 1 mwezi wa saba alinitikisia kiberiti ila nilimuonyesha maamuzi magumu hadi akaanza kulia ye mwenyewe akasema sijawahi kukutana na mwanaume mwenye roho ngumu kama wewe , sahiv kaanza tena kunitafuta ila nimemkazia sitaki hata kumuona asije akanifanyia jaribio lingine la kuniua
 
Desemba mwaka huu nagonga miaka 77. Nilifikiri kwamba nimeshamalizana na hizi hekaheka za mapenzi. Aaaa wapi bwana. Kumbe ni kweli hayanaga mwongozo. Yaani nimekuja kubananishwa na kibinti cha Kisukuma kimatani matani tu hivi najiona kabisa na akili zangu kamili....

Ni siteresi 24/7 na sioni hata dalili za kujinasua yaani. Kweli hujafa hujaumbika wallahi!

Ila nitatoboa tu 💪💪💪💪
 
Eti kama hizi stress za mapenzi zingekuwa zinaua wewe ungekuwa marehemu tangu mwaka gani?

Aah yaani mimi ningekufa mwaka jana yaani ningekuwa sasa hivi nimebaki mifupa ila Alhamdulillah hazijaniua zimenifanya tu kuwa sugu.
Mwanaume unakuwaje na stress za mapenzi ?

Stress za mapenzi ndiyo nini? Zinakuwaje ?
 
Desemba mwaka huu nagonga miaka 77. Nilifikiri kwamba nimeshamalizana na hizi hekaheka za mapenzi. Aaaa wapi bwana. Kumbe ni kweli hayanaga mwongozo. Yaani nimekuja kubananishwa na kibinti cha Kisukuma kimatani matani tu hivi najiona kabisa na akili zangu kamili....

Ni siteresi 24/7 na sioni hata dalili za kujinasua yaani. Kweli hujafa hujaumbika wallahi!

Ila nitatoboa tu 💪💪💪💪
mzee wangu polee sana kumbe wasukuma nao sio haba.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom