Progamu mtoto anazoweza kufanya wakati huu wa likizo ya mwisho wa mwaka

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Salaam Wazazi/Walezi

Kama mnavyojua vijana wetu wanakaribia kuanza likizo yao ya mwisho wa mwaka. Tuwapongeze kwa kuweza kupambana na masomo yao kwa kipindi chote mwaka huu. Shule huchosha akili, hasa hizi shule ya English Medium zimekuwa zikiwarundikia kazi wanafunzi hivyo kukosa muda wa kutosha kupumzika.

Hivyo ni vyema kuwapunguzia shinikizo la masomo kipindi hiki cha likizo ili waweze kujiandaa na mwaka wa masomo unaofuata.

Kipindi hiki cha likizo mtoto anakuwa na muda wa kutosha kubaki nyumbani, hivyo atatumia muda mwingi kuangalia vipindi mbalimbali katika luninga. Endapo atakosa usimamizi mzuri, atajikuta anaangalia vipindi visivyo na maadili hasa hizi nyimbo zetu za Bongo fleva ambazo kadri siku zinavyokwenda zinazidi kupoteza maadili.

Hivyo kama wazazi tuangalie namna bora ya kupendekeza programu nzuri ambazo mtoto anaweza kufanya kwa kipindi hiki cha likizo ili ziweze kumjenga kuliko kushinda nyumbani siku nzima bila chochote cha msingi.

Binafsi napendelea mwanangu kipindi hiki cha likizo nimpeleke kwenye hizo programu tatu
  • Mafunzo ya kuogelea
  • Sarakasi, na
  • Kupiga kinanda.
 
Mimi mtoto wangu kipindi cha likizo anabidi kukitumia katika kuendeleza kipaji chake cha Uandishi wa vitabu na mafunzo mbalimbali ya kufundisha katika semina hivyo atabidi amalizie kusoma kitabu cha Financial intelligence by Robert .
 
1. Anapenda kuimba, so atakuwa anaenda kufanya mazoezi.
2. Natamani ajifunze kupiga kinanda.
 
Mwanangu atatulia kwenye ofisi yake tu ya geto kwake na PC yake akigonga code na kujifunza proffesional speaking, goal nzima ni yeye kuja kupiga pesa za wazungu baadae i.e grants nk
 
Ngoj niendelee kusubili idea za watu huenda nami nikapata wazo wa kwangu afanye nini
 
Back
Top Bottom