Naibu Waziri Mkuu, Dk Doto Biteko ametangaza kufuta likizo kwa watumishi wote wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) akiwataka wote wawe kazini kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme.
Amesema hakuna mtumishi wa Tanesco atatakiwa kwenda likizo wakati huu wa changamoto ya mgawo wa umeme...