DED Tunduru kwanini huu ubaguzi katika kulipa pesa za likizo?

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,173
6,157
Wiki iliyopita baadhi ya walimu walilipwa pesa zao za likizo baada ya nafikiri kulalamika humu jukwaani.

Pesa hizo wamelipwa baadhi ya walimu, tunauliza kwanini ubaguzi huu? Kwanini baadhi walipwe na wengine wasilipwe. Je ni kwasababu ya rushwa au kujuana? Mheshimiwa waziri Mchengerwa tunakuomba sana imulike hii halmashauri, maafisa utumishi ni wajeuri, wabaguzi, wamejaa kiburi na dharau.

Mbaya zaidi mkurugenzi ni kama hayupo. Mwaka juzi baadhi ya walimu walilipwa likizo zao mwaka jana(2023) mwezi wa tatu tena wakiwa wamekatwa zaidi ya nusu ya pesa walizoomba.

Hapa Tunduru Halmashauri kuna ubaguzi na uonevu mkubwa sana jambo ambalo ni nadra ktk halmashauri zingine nchini. Tunaomba msaada wako waziri wetu wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
 
Andolewe haraka kwa maslshi ya nchi.
Utaondoa Maded wote waHalmashauri zote.Kuhusu HRO hao utafikiri wameajiliwa kutoka tumbo Moja.Sijui Kozi za utumishi huko vyuoni wanafundisha dharau,majivuno na ujeuri,Kuhusu kulipa Kwa Makundi Halmashauri nyingi Wana michezo hiyo ukiuliza wanasema bajeti ndogo hata huyo Mchengerwa analijua.Hoja Yako ya kulipwa pungufu hili linaanzia Kwa Mkuu wa Idara SLO wengi wanajifanya wanafanya kazi Latra wanapunguza nauli wanaweka zile tu zilizoko kwenye mkeka wa Sumatra za vijijini huko wanafyeka,sijui ulilala Lodge fyeka n.k,lakini na nyie walimu ujanja mwingi Kuna Mabachela lakini kwenye Madai Wana vyeti vya ndoa, wengine hawana watoto na wanafahamika lakini utashangaa vyeti vya wategemezi kuwazidi wenye watoto.Mkuu pole utalipwa tu ni haki Yako lakini unaweza kwenda likizo nyingine na ya kwanza haukulipwa ni full malimbikizo ya madeni.
 
Wiki iliyopita baadhi ya walimu walilipwa pesa zao za likizo baada ya nafikiri kulalamika humu jukwaani.

Pesa hizo wamelipwa baadhi ya walimu, tunauliza kwanini ubaguzi huu? Kwanini baadhi walipwe na wengine wasilipwe. Je ni kwasababu ya rushwa au kujuana? Mheshimiwa waziri Mchengerwa tunakuomba sana imulike hii halmashauri, maafisa utumishi ni wajeuri, wabaguzi, wamejaa kiburi na dharau.

Mbaya zaidi mkurugenzi ni kama hayupo. Mwaka juzi baadhi ya walimu walilipwa likizo zao mwaka jana(2023) mwezi wa tatu tena wakiwa wamekatwa zaidi ya nusu ya pesa walizoomba.

Hapa Tunduru Halmashauri kuna ubaguzi na uonevu mkubwa sana jambo ambalo ni nadra ktk halmashauri zingine nchini. Tunaomba msaada wako waziri wetu wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
DAWA NI MOJA TU KUWASHITAKI KWA MUNGU KWA KUWALAANI MAKANISANI,MISIKITINI NA KUVUNJA CHUNGU HAKUNA NAMNA NASEMA HAKUNA NAMNA WASOMEENI VISOMO VIKALI NA VITAKATIFU
 
Wiki iliyopita baadhi ya walimu walilipwa pesa zao za likizo baada ya nafikiri kulalamika humu jukwaani.

Pesa hizo wamelipwa baadhi ya walimu, tunauliza kwanini ubaguzi huu? Kwanini baadhi walipwe na wengine wasilipwe. Je ni kwasababu ya rushwa au kujuana? Mheshimiwa waziri Mchengerwa tunakuomba sana imulike hii halmashauri, maafisa utumishi ni wajeuri, wabaguzi, wamejaa kiburi na dharau.

Mbaya zaidi mkurugenzi ni kama hayupo. Mwaka juzi baadhi ya walimu walilipwa likizo zao mwaka jana(2023) mwezi wa tatu tena wakiwa wamekatwa zaidi ya nusu ya pesa walizoomba.

Hapa Tunduru Halmashauri kuna ubaguzi na uonevu mkubwa sana jambo ambalo ni nadra ktk halmashauri zingine nchini. Tunaomba msaada wako waziri wetu wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Tatizo kubwa umoja wenu wa waalimu umetejwa na wanasiasa. Haya yasingekua yanatokea kama umoja huo ungekuwa na viongozi wenye nia ya dhati kuhudimia waalimu.
 
Hakuna mtu fisadi kama Chiza malando mkurungenzi wa Tunduru hili fisadi sana.
 
Back
Top Bottom