Walimu wanaojitolea kufundisha kipindi cha likizo wapongezwe, wazazi msisite kuchangia chochote

Nobunaga

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,169
4,986
Nimefungua huu uzi baada ya kuona "dokezo" hili lililopostiwa hapa JF...


Nipo hapa kupinga hili dokezo kwa nguvu zote kwa sababu haliendani na uhalisia wa elimu ya mtanzania wa st kayumba.

Kama kuna ambaye hafahamu, shule za kata zinazofanya vizuri huwa kuna "nguvu ya ziada" inatumika. Mojawapo ni hii ya kuwabakisha wanafunzi wa madarasa yenye mitihani ya taifa kwa mwaka husika, na hasa hasa concentration huwa inaelekezwa kwenye masomo makuu (core subjects).

Tuition siyo jambo geni kwa nchi yetu. Kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma st kayumba, na kama mzazi anajitambua hawezi kumuacha mtoto wake kipindi cha likizo akae tu bila kupata vipindi vya ziada.

Wengi wetu tumetoboa kwa kusoma st kayumba, lakini bila kujiongeza hakika sahau kutoboa kimasomo.

Na kwa wasiojua, habari za elimu bure is just a political stunt, ila kwa ground mambo ni tofauti sana, wazazi inabidi wajue kujiongeza kwa kuwapa walimu motisha ili wapate motisha zaidi wa kufundisha mpaka kipindi cha likizo.

Kuna ambao watauliza mbona private wanaweza, wanawezaje? Jibu ni ratiba za private schools ziko tofauti sana. Mfano wakati kidato cha tano wanafungua mwezi July kwa ratiba ya kawaida, private wao wanakuwa wameshaanza masomo toka mwezi April au May.

Hivyo nitoe rai kwa wazazi wenzangu wanaosomesha st kayumba, mkiona walimu wamejitolea kufundisha kipindi cha likizo, tunapaswa kuwapongeza na kuwapa motisha kwa kuwawezesha kwa chochote kitu. Hatupaswi kuwavunja mioyo kwani lengo lao ni zuri.

Niwaombe rai jf administrators muondoe hilo dokezo kwani kiuhalisia linabomoa badala ya kujenga. Aliyelileta huenda hajui uhalisia wa maisha ya shule za kata.
 
Usimpinge , wewe unataka kila mtu asome?

Utapata wapi shamba boy na ma-beki 3?

Wakati matajiri viongozi wa Serikali wa wizara na ikulu watoto wao wapo Kifungilo Girls, , St Fransi -Mbeya , Livingstone Seminary Tanga, St Meriogoreth na St Dominic savio ambazo hakuna likizo na ada ya mwaka inalipwa na ya twisheni na wanapewa likizo tarehe 21-12-2023 kwa wiki moja mpaka january 2-1-2024 ,watoto wa maskini wanapinga shilingi elfu 10 kwa mwezi mtoto asome.
Sasa basi nawashauri maskini tuandamane, tusilazimishwe kusoma, watoto wakae holiday, Matajiri hawapendi watoto wao ndio maana wanawaacha wakae na mapadri na masista.
 
St. Kayumba tuition ni jambo lisiloepukika, lazima upige MAPINDI uwe full nondo.

R.i.p comissioner..
MOUDY PHYSICS
Apumzike kwa amani, kupitia MAPINDI yake fizikia ikawa ni uwanja wa nyumbani.
Shule nisingepata fizikia ya kiwango kile.
 
Eiiiishhhhh maokoto tunayataka ila walimu nanyi muache viranga.....acheni watoto wapumzike. Bora hata likizo ya july hii ya december????? Ntamnyonga mwalimu kwa kutumia tai aloivaa
 
Back
Top Bottom