Pakistan yamuita nyumbani balozi wake kutoka Iran na balozi wa Iran Pakistan alieko likizo Iran hatoruhusiwa kurudi kazini

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Pakistan imemuita nyumbani balozi wake alieko nchini Iran na pia imesema haitomruhusu balozi wa Iran alieko nchini Iran kwa likizo kutorudi Pakistan.

Uamuzi huo wa serikali ya Pakistani umetolewa baada ya jeshi la mapinduzi la Iran (IRG) kufanya mashambulizi ndani jimbo la Balochistan lililoko kusini magharibi mwa Pakistani na kuua watoto wawili.

Katika jimbo hilo la Balochistan wapo waasi wa kibalochi ambao wamekuwa wakidai uhuru wa jimbo hilo kutoka kwa Pakistan. Jimbo hilo la Balochistan pana mpaka ambao hutumiwa na nchi hizo mbili mpaka wenye urefu wa maili zipatazo 559.

Mapema jana Iran ilifanya mashambulizi ya kutumia makombora na ndege zisizo na rubani (UAVs) na kushambulia sehemu hiyo ambayo yaaminika kulikuwepo kundi la wapiganaji wa kiislam wa Jaish Al Adl ambaio ni wasuni.

Pakistani imelaani vikali mashambulizi hayo ambayo yafuatia mashambulizi mengine yalofanywa na IRG jumatatu, kaskazini mwa Iraq na nchini Syria.

Mashambulizi haya ya IRG yaelekea kuleta sintofahamu kubwa ndani ya mashariki ya kati ambapo vita kati ya Israeli na kundi la Hamas bado laendele huku siku 100 zikiwa zimepita.

Pakistan imelaani mashambulizi yalofanywa Balochistan na imesema kitendo hicho cha kuingia ndani ya anga lake ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa na kwamba Iran ijiandae na majibu.

Jeshi la Jordan nao leo hii limetoa taarifa kuwa sehemu ya majengo ya hospitali yake ya kijeshi iliyopo katika mji wa Khan Yunnis yameharibiwa kwa makombora ya Israeli yalokusudiwa kushambulia kambo ya Hamas ilokuwa imejificha sehemu hiyo.

Hali ya usalama katika mashariki ya kati imekuwa ni tata na vita kati ya mataifa mbalimbali huenda ikaenea kwa kasi.

Kwanini Iran yafanya mashambulizi haya wakati huu wa sasa?

Itakumbukwa kuwa baada ya mauaji ya mabomu yalofanywa na kundi la ISIS mapema mwezi januari mwaka huu ambao walikiri kuhusika nchini Iran katika mji wa Kerman, kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei alitoa onyo kwamba kutakuwepo na majibu makali kutoka kwa Iran.

ISIS walishambulia kwa bomu la kujitoa mhanga watu walokuwa waliadhimisha miaka mitatu ya kifo cha jasusi mbobezi Jenerali Qasem Soleimani ambae aliawa na mashambulizi ya Marekani na kuua watu 84. Hivyo Iran imeamua kutumia fursa hii kufanya mashambulizi yake Idlib nchini Syria ambako ndiko yalipo makazi ya kundi hilo.

Kundi la ISIS lasemekana ndo kundi la mwisho lilosalia linoikabili serikali ya raisi Assad ambae ni wa kabila la Shia. Kundi hili lipo chini ya ufadhili wa nchi za Magharibi na Marekani.

Hivyo mashambulizi yalofanywa na IRG yalilenga kuvunja miundombinu ya kundi hili pamoja na mashambulizi ya kaskazini mwa Iraq sehemu ya Kurdistan katika mji wa Irbil ambayo yalilenga kuvunja na kubomoa majengo na miundombinu ya majasusi wa Mossad.

Iran imedai kuwa kundi hili lina kazi ya kukusanya taarifa za kijasusi na kuzitoa kwa wahusika wanoshughulika nazo katika mashambuliz sehemu mbalimbali katika mashariki ya kati.
 
Wanapigana wao kwa wao wanamsingizia marekani
Mkuu, unganisha dots.

Hao wanoshambuliwa na Iran ni makundi ya wapiganaji ambao hufadhiliwa na .....

Makundi hayo wengi na Wasuni na ndo walioko kaskazini mwa Iraq na nchini Syria.

Ndo wanotumiwa kwa mashambulizi ndani ya Iran na sehemu zingine.

Hivyo Iran nao watumia Satelite ya ....... kufanya mashambuli hayo ambayo mengi ni "precise." yaani hayakosei.
 
Pakistan inalea vikundi vya kigaidi Iran ana haki ya kujilinda.
Watu wasahau kwamba huenda washirika wa Iran China na Russia waipatia taarifa za kijasusi za Satelite Iran na ndo maana hawakosei katika kutupa makombora yao.

Ndo maana China leo katoa kauli kwamba kuwe na utulivu kati ya Iran na Pakistan.

China hawajalaani mashambulizi hayo hivyo kutoa "indication" kwamba wana angalau some info.

Russia wao wapo busy na Ukraine lakini jicho moja lipo Middle East.

Mtu mmoja amwaga mboga mwingine amwaga ugali wa dona.
 
China huyu huyu anabomoa majumba ya ibada?
 
Kimeanza kunuka huko, Pakistan washachinja mtu

The senior IRGC officer who was reportedly assassinated near the Pakistan border

View: https://twitter.com/MOSSADil/status/1747660403545387137?t=xIYL6lKfymryUyaYdahljA&s=19
 
Watu wasahau kwamba huenda washirika wa Iran China na Russia waipatia taarifa za kijasusi za Satelite Iran na ndo maana hawakosei katika kutupa makombora yao.

Ndo maana China leo katoa kauli kwamba kuwe na utulivu kati ya Iran na Pakistan.

China hawajalaani mashambulizi hayo hivyo kutoa "indication" kwamba wana angalau some info.

Russia wao wapo busy na Ukraine lakini jicho moja lipo Middle East.

Mtu mmoja amwaga mboga mwingine amwaga ugali wa dona.
Shida ya lile eneo kila adui ni rafiki WA adui.
Pakistani adui WA India
India adui WA china
China rafiki WA Pakistani
Iran rafiki WA india
Pia Irani rafiki WA China
Russia rafiki WA India China na Iran.
Pia Pakistan rafiki WA USA na ndio alimpa Nuke
Russia akampa India Nuke. Ukumbuke pia India adui WA China ambae ni rafiki WA Russia
 
Back
Top Bottom