Mbunge Santiel Kirumba Aongoza Maadhimisho ya Mtoto Njiti Duniani, Agawa majiko ya Gesi, Aiomba Serikali Iongeze Likizo Mama Aliyejifungua Mtoto Njiti

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA AONGOZA MAADHIMISHO YA MTOTO NJITI DUNIANI, AGAWA MAJIKO YA GESI, AIOMBA SERIKALI IONGEZE LIKIZO MAMA ALIYEJIFUNGUA MTOTO NJITI

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba ameongoza Maadhimisho ya Mtoto Njiti duniani katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga huku akiiomba serikali iongeze likizo ya mama aliyejifungua na mtoto njiti.

Maadhimisho hayo ya siku ya Mtoto Njiti Duniani (Premature Day) yamefanyika katika kituo cha afya Bugarama Halmashauri ya Msalala ambapo siku ya kimataifa ya watoto njiti huadhimishwa tarehe 17 Novemba kila mwaka ulimwenguni kote kwa nia ya kuelimisha kuhusu kujifungua watoto njiti ambao hawajakomaa na kufikisha wiki 38 (miezi 9).

Maadhimisho hayo yameenda sanjari na kukutana na akina mama wajawazito na mama waliojifungua watoto njiti wanaonyonyesha kuwapa elimu ya kukaa na mtoto njiti sambamba na kugawa majiko ya gesi 50 kwa akina mama hao, watumishi wa afya katika kituo cha afya Bugarama na polisi Jamii.

"Tumegawa majiko ya gesi 50 kwa sekta ya afya inayohusika na mama na mtoto 15, wajawazito 15, akina mama wenye watoto njiti 15, majiko matano yalienda kwa askari polisi wanaohusika na masuala ya ukatili wa kijinsia kwa sababu mama akifanyiwa ukatili wa kijinsia anaweza kujifungua mtoto njiti." - Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba

"Tumewapongeza polisi jamii kwa kuweza kutupazia sauti na kuchukua hatua haraka. Watumishi wa afya pia tumewapa majiko kuwashukuru kwa mchango wao kwa jinsi wanavyowapigania watoto njiti" - Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba

Mhe. Santiel amesema kila mwaka watoto njiti 200,000 wanazaliwa na kutokana na changamoto ambazo watoto njiti wanapitia ni kundi ambalo limesahaulika kutunzwa hasa maeneo ya vijijini wazazi wamekuwa wakipoteza watoto wao kutokana na mazingira duni ya kushindwa kuwatunza.

"Serikali ikiwekeza kidogo tutaona matokeo makubwa, hawa watoto hasa maeneo ya vijijini wamekuwa wakifariki dunia kutokana na kwamba wazazi wao hawawezi kuwatunza, mtoto huyu anatakiwa akae kwenye kangaroo siku 90 tangu azaliwe. Kwa hiyo kwenye hilo unakuta mzazi anashindwa kumhudumia mtoto" - Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba

"Serikali imeanza kufundisha kwenye shule kwamba watoto njiti walelewe, pia Serikali imeweka huduma yam toto njiti kwenye bima, zamani haikuwepo. Kilichobakia ni huduma ya likizo ya uzazi ya mama aliyejifungua mtoto njiti kwa sababu akijifungua ana miezi sita itamtaka akae siku 90 ili mtoto aweze kutimia" - Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba

"Tunahitaji huyu mama aongezewe likizo ya uzazi na pia huyu mama apewe benefit anapokuwa katika kulea mtoto njiti kwa sababu kulea mtoto njiti ni gharama na inaweza kumfanya mwanamke arudi nyuma kiuchumi kutokana na kwamba anatumia muda mwingi kumwangalia mtoto zaidi kuliko kufanya shughuli za kumwingizia kipato" - Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba

Aidha, Mhe. Santiel Kirumba ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi kubwa inazofanya kuboresha sekta ya afya ambapo imeleta shilingi 157 na vifaa tiba na kujenga jengo la mtoto njiti katika mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) watoto Milioni 15 duniani huzaliwa kabla ya miezi 9 yaani njiti na hii imekuwa ikiongezeka siku hadi siku hali ambayo inatajwa kuchangia kwa wingi vifo vya watoto chini ya miaka mitano duniani. Kwa mujibu wa WHO kwa kila watoto 10 wanaozaliwa mmoja ni njiti.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.37(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.37(1).jpeg
    109.7 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.51(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.51(1).jpeg
    156.2 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.51.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.51.jpeg
    116.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.50(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.50(2).jpeg
    151.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.50.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.50.jpeg
    147 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.49(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.49(2).jpeg
    122.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.49(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.49(1).jpeg
    148.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.39(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.39(1).jpeg
    126.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.44(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.08.44(1).jpeg
    132.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.42.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.42.jpeg
    119.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.39.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.39.jpeg
    125.1 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.43(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.43(1).jpeg
    139.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.45.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-18 at 13.07.45.jpeg
    140.1 KB · Views: 3
Dah! Sikujua kama Kuna sikukuu ya Mtoto Njiti. Mwakani nitaiadhimisha maana ni Binti yangu ni Njiti. Happy Premature Day my daughter!!!
 
Back
Top Bottom