Likizo time tuliporudi vijijini,watoto wenzetu walielekea Paris,London, Washington DC waliambiwa nanyi pia mna haki ya kuishi hapa

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Wakati wa likizo miaka ya 1980 tulipokuwa watoto,ilikuwa ni utamaduni kwenda kuwasalimu bibi na babu,yalikuwa ni malezi bora yenye baraka pale babu na bibi wanapokushika mkono kukubariki na kukutakia yote yaliyo mema,wakati tukirudi kijijini, watoto wa waliofanikiwa walipelekwa kutembea Paris,Ufaransa,London,UK, Washington DC,Marekani walipofika uko wazazi wao waliwaambia nanyi pia mna haki ya kuishi huku duniani,sio kule kijijini tulipotoka,miaka thelathini mbele watoto hao tayari wamekuwa wenyeji uko Paris,london na Washington na leo hii wananunua nyumba palm Jumeirah Dubai kwa bilioni 25.

Wakati wazazi wetu wanatufundisha kuwa na kiasi na kuridhika na kile kidogo tunachopata,watu waliofanikiwa wanafundisha watoto wao kwamba kila kilichopo duniani ni haki yao kukipata na kukimiliki,ndio maana mtu anaweza kuja kuchukua Mali yako ya halali na kusema ya kwake sababu amekuona tu unaishi kijamaa umeridhika na kidogo ulichonacho,ila yeye hajaridhika anataka kuchukua hata kidogo ulichonacho,Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere aliuita huu ni ukupe,unyonyaji,ubepari na ukabaila.Tuliolelewa na malezi ya Mwalimu tuliofundishwa kuridhika na tulivyonavyo tunabaki tunajiuliza mbona watu awa wamefanikiwa lakini bado hawaridhiki,kumbe wakati sisi tunafundishwa pesa haiwezi kununua furaha,watu waliofanikiwa waliwafundisha watoto wao kuzitafuta pesa ndiyo waseme ni kweli pesa hainunui furaha,na wazazi wao walihakikisha watoto wanaingia kwenye mifumo yote ya kiuchumi.

Je ni kweli tulifanywa kuwa wanyonge katika ulimwengu wa kibepari tukaendelea kuishi kijamaa!? Wenzetu waliofanikiwa wanawaandaa watoto wao kuwa ngangari Ili waweze kwenda na ulimwengu wa sasa,hawakuwafundisha watoto wao kuridhika,hivi sasa mambo mazuri yote wanafaidi wao waliofanikiwa,wanasafiri kwa ndege,sisi kusafiri kwa ndege labda tulipiwe na ofisi,au tushinde bahati nasibu,na kukipanda tunavyopiga picha na kuzisambaza mitandaoni kila mtu aone,huu ni unyonge,wenzetu waliofanikiwa wanalala hotel nzuri za nyota tano,sisi tunalala kwenye nyumba za wageni ndala tofauti wakiweka zinafanana utaiba,tulifundishwa kuridhika,Wakati tukifundishwa kufanya kazi kama watumwa ili tuishi kama wafalme, wenzetu waliofanikiwa wanawafundisha watoto wao mjini akili nguvu peleka shamba.

Nimalizie kwa kusema kwamba tuwafundishe watoto wetu maisha ya uhalisia,kwanza wawe makini kwa kila jambo ni sawa tupo msituni na Simba anatuwinda,tuwafundishe watoto wetu wajue fursa kwamba kwenye matatizo kuna ulaji,sisi tulioridhika hatuoni huo ulaji,ikinyesha mvua tunaona tope,mafuriko tunaona kifo, waliofanikiwa wakiona mvua wanaona pesa,wakati sisi tunafundishwa walimwengu ni wabaya, waliofanikiwa wanafundisha watoto wao walimwengu ni fursa na mtaji mkubwa hasa ukimkuta mtu aliyeridhika na malezi ya kijamaa,bado hatujachelewa wakati kitoto cha mchina kikiletwa Kariakoo kuuza duka la mashuka,taulo na pazia sisi hatujui nini cha kuuza!? wakati mchina akideposit milioni mia tano kila siku benki sisi tunaomba kazi ya kufagia na kuwapangia mabelo yao ya nguo,kwa nini hatukugundua mwanzo kuwa Watanzania wanahitaji sana chandarua,mashuka,taulo na mapazia,tuamke sasa, tuwafundishe watoto wetu fursa zilizojaa hapa Tanzania.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in International business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.
 
Asante kwa ushauri, kweli dunia ni mapambano, hakuna anahaki mwingine, ni vita ya kusaka fursa, ukishindwa kufiti kwenye mfumo huo wa mapambano tayari unakuwa nje ya mfumo automatically unakuwa masikini, ndo maana tunaambiwa tujiajili , hawakwambia namna ya kupata mtaji,unaambiwa kiakili tu, ambaye nakwambia jiajili yaye amesajiliwa na wameshatengeneza mazingira ya ndugu zake kuajiliwa.
 
Asante kwa ushauri, kweli dunia ni mapambano, hakuna anahaki mwingine, ni vita ya kusaka fursa, ukishindwa kufiti kwenye mfumo huo wa mapambano tayari unakuwa nje ya mfumo automatically unakuwa masikini, ndo maana tunaambiwa tujiajili , hawakwambia namna ya kupata mtaji,unaambiwa kiakili tu, ambaye nakwambia jiajili yaye amesajiliwa na wameshatengeneza mazingira ya ndugu zake kuajiliwa.
Sasa mnanichanganya

Tujiajiri au tuajiriwe??

Ukweli ni kuwa fundisha mwanao biashara
 
Mkuu ungesema tu.

Watu wanaoiba pesa za Watanzania ni kupigwa risasi au kupotezwa.

Hizo habari za watoto kwenda Paris au New York hazituhusu sana.

Majizi haitakiwi kuuliza sijui umeridhika ama nini.

Ni chuma tu au life imprisonment.

Tusipofanya hivyo watanzania wataendelea kushikwa mat*ko.
 
Mkiwa wote wafanya biashara, biahara zenu mtamuuzia nani?
Haiwezekani wote kuwa wafanyibiashara ingawa dunia inayofuata ni business oriented

Kama huna business skills yajayo yatawatoa jasho
 
Back
Top Bottom