Ee mwumba wetu, umewaunganisha watu katika ndoa takatifu nami natumaini kupokea Sakramenti hiyo na kushirikiana na mwenzangu wa ndoa maisha yangu yote.
Kwa hiyo nakuomba ee Bwana unisaidie kuchagua kwa hekima, nipate mchumba mwema, safi na mwaminifu, nifuate zaidi uzuri wa roho kuliko wa uso...