Kwa Kauli hii ya RC wa Simiyu kuhusu Watu 22 Waliokufa Machimbo sioni sababu ya Serikali kuhangaika nao au watu kuwalilia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,649
109,040
"Baada ya Juzi Wachimbaji hawa Kuingia Chini Shimoni walikuta Madini ya Dhahabu ila kukaonekana kuwa hali ya Kule chini Kimazingira haikuwa Salama hivyo walivyopanda Juu na. Kuielezea kwa Wataalamu na Viongozi ilishauriwa wasubirie Kwanza ili Kuwatengenezea Mazingira mazuri ya Kiusalama Kwao kama Wakienda tena baadae na kukawekwa Askari wa Kulinda hilo Shimo na Eneo ila cha Kushangaza na Kusikitisha muda wa Usiku baada ya Askari hao kutoka hapo kurejea Makwao hawa Wachimbaji walikuja Kimya Kimya na Kuamua Kuingia huko Shimoni hatimaye wakakutwa na kilichowakuta na leo tunawaomboleza" amesema RC wa Simiyu.

Chanzo: U-FM Radio Asubuhi leo.

Hakuna ambaye hajui kuwa kwa sasa Maisha ni Magumu na huenda hata Mimi GENTAMYCINE nikawa na Maisha Magumu kuliko Wengine wanaojinasibu kila Siku ila hakuna Kitu ambacho nakiheshimu na nakifanya kila Uchao kama kuwa Makini na kufuata miongozo ya Kitaalamu na kutoka kwa Watalaamu.

Uhai na Usalama wangu ni muhimu kuliko Shida zangu nyingi na Tukuka za Kimaisha nilizonazo.

Yaani Ufe Kizembe halafu nikulilie? Thubutu na huyo siyo GENTAMYCINE labda Bujibuji Simba Nyamaume ndiyo anaweza kuwa na Huruma hiyo ya Kinafiki.

Maziko mema kwa Waliojitakia.
 
Sure kabisa mkuu.

Kuna watu watatetea kwa kusema eti kifo hakizuiliki. Kuna sababu zingine za kifo zinazuilika sana tu.

Siku zote huwa naona kuishi ni priority yangu ya kwanza, hasa nikifikiria wategemezi wangu wataishije nikifa/nikijikuta katika mazingira ambayo nami nakuwa mtegemezi, hivyo najitahidi sana kuziepuka hatari kadri ya uwezo wangu, nikifa ama kupata janga la kunigharimu basi iwe katika mazingira ambayo sina namna.

Kwanza ni ubinafsi. Jitu unakuta lina wake wawili na watoto 10 hata mahitaji ya shule tu ni ishu, kula yao inalitegemea kuanzia jumatatu hadi jumapili halafu linaingia kwenye ishu ambazo ni life threatening.

Ukishindwa kujithamini mwenyewe, wathamini basi hao wategemezi uliowajaza hapo kwako, ambao wala hata hawakukuandikia barua kukuomba uwalete hapo, ni tamaa zako tu. Always jiulize kama upo ila ni full tabu, je maisha yao yatakuwaje ukitoweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Baada ya Juzi Wachimbaji hawa Kuingia Chini Shimoni walikuta Madini ya Dhahabu ila kukaonekana kuwa hali ya Kule chini Kimazingira haikuwa Salama hivyo walivyopanda Juu na. Kuielezea kwa Wataalamu na Viongozi ilishauriwa wasubirie Kwanza ili Kuwatengenezea Mazingira mazuri ya Kiusalama Kwao kama Wakienda tena baadae na kukawekwa Askari wa Kulinda hilo Shimo na Eneo ila cha Kushangaza na Kusikitisha muda wa Usiku baada ya Askari hao kutoka hapo kurejea Makwao hawa Wachimbaji walikuja Kimya Kimya na Kuamua Kuingia huko Shimoni hatimaye wakakutwa na kilichowakuta na leo tunawaomboleza" amesema RC wa Simiyu.

Chanzo: U-FM Radio Asubuhi leo.

Hakuna ambaye hajui kuwa kwa sasa Maisha ni Magumu na huenda hata Mimi GENTAMYCINE nikawa na Maisha Magumu kuliko Wengine wanaojinasibu kila Siku ila hakuna Kitu ambacho nakiheshimu na nakifanya kila Uchao kama kuwa Makini na kufuata miongozo ya Kitaalamu na kutoka kwa Watalaamu.

Uhai na Usalama wangu ni muhimu kuliko Shida zangu nyingi na Tukuka za Kimaisha nilizonazo.

Yaani Ufe Kizembe halafu nikulilie? Thubutu na huyo siyo GENTAMYCINE labda Bujibuji Simba Nyamaume ndiyo anaweza kuwa na Huruma hiyo ya Kinafiki.

Maziko mema kwa Waliojitakia.
Mambo ya madini, ukiondoa "di" = majini; lakini pia Dhahabu ukibadili nafasi(interchange) ukaanza na "a" = adhabu.
1. Kwa nini askari waondoke? Ulinzi huwa ni 24hrs. au vp?
2. Inawezekana Wachimbaji walirubuniana /walidanganyana kuwa kuna wajanja wanaoingia usiku na kujizolea dhahabu. Kwa habari hiyo, Wahanga katika hili nao wakabweteka, na ili kuwahi, wakajipeleka nao huko ili wakajaribu bahati yao.
Dah! Wakapata lililowapata. Pole zao, Wapumzike kwa amani.
 
Njaa mbaya jmn
Sawa; lakini bado hao hata kama ni marehemu au bado wapo hai huko chini wanayo HAKI yao kama binadamu wengine ya kuokolewa au kuzikwa kwa heshima stahiki i.e. huyo RC asitumie lugha aliyotumia kwani hata yeye na sisi wote ni marehemu watarajiwa. Ajali haishabikiwi hata siku moja.
 
Unaongea bila kujua uhalisia wa maisha.

Usimlilie mtu kisa Nini? Wewe Huwa unatii kila unaloelekezwa?

Popoma!!
 
Sawa; lakini bado hao hata kama ni marehemu au bado wapo hai huko chini wanayo HAKI yao kama binadamu wengine ya kuokolewa au kuzikwa kwa heshima stahiki i.e. huyo RC asitumie lugha aliyotumia kwani hata yeye na sisi wote ni marehemu watarajiwa. Ajali haishabikiwi hata siku moja.
Ni sahihi mkuu tuwaombee tu watu wa Simiyu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom