Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni chama cha kiasiasa nchini Tanzania ambacho kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha katika miaka 1997 hadi 1979.
Mwaka 2000 CHADEMA hakikuwa na mgombea wa Urais. Mwaka 2005 mgombea wa CHADEMA Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.
Mwaka 2010 CHADEMA ilipata asilimia 27.1% na mgombea Urais wa chama Wilbroad Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.
Hata hivyo CHADEMA imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
Kupitia matangazo ya moja kwa moja yanayoendelea ya channel 10, imemuonesha aliyekuwa Katibu Kkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji akiingia ofisi hizo akiwa akiwa amevalia nguo za CHADEMA tayari kwa kuijiunga na CCM.
Anaeleza baada ya kutafakari kwa kina amebaini CHADEMA haina utayari wa kuleta...
Uchaguzi umekaribia, wale waliotuacha CCM wao wakamfuata mamvi, wakapata udiwani na ubunge, leo hii wameona uchaguzi umefika wanakuja kwa sharti kuwa wapewe nafasi ya kugombea. Je, sisi tulikipigani chama mmeamua kutuweka kando. Au ni mkakati wa CHADEMA kuja kivingine kuchukua kwa sura ya kuunga...
Kiukweli kitendawili cha nafasi ya mwenyekiti wa CHADEMA ni kigumu sana kukitegua.
Kwanini Mwenyekiti yuko madarakani kwa zaidi ya miaka 20, ndilo swali kuu!
Je, ni demokrasia, ubabe au udikteta?
Kwanini kila aliyetamani kuwa Mwenyekiti wa Chadema leo hii hayuko katika chama hicho chenye...
Baada ya aliyekuwa Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe kuhamia CCM inaelezwa kuwa madiwani wawili wa jimbo la Mtama watajiunga na CCM wakati wowote kuanzia sasa.
Taarifa zinadai kuwa huko Ndanda maelfu ya wana-Chadema wamerejesha kadi na bendera za chama hicho na wanasubiri kukabidhiwa kadi za CCM na...
Naibu waziri. wa Tamisemi Mwita Waitara amesema NEC ni Tume huru ya uchaguzi, watakaosusa wasuse lakini wengine watakula.
Source: Malumbano ya Hoja mubashara
Najiuliza tu maana tangia wamchukue Lazaro Nyalandu kutoka CCM hawa jamaa wa CHADEMA hawajapokea diwani wala Mbunge tena kutoka chama tofauti.
CCM wao karibia kila mwezi wanapokea madiwani kutoka vyama vya upinzani wanaojiunga nacho kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.
Je, CHADEMA kimepoteza...
Aliyekuwa mwenyekiti wa kanda ya Pwani na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA mzee Sumaye amesema mara kadhaa aliwashauri viongozi wenzake wapambane na CCM kwa hoja lakini walimpuuza.
Sumaye anasema CHADEMA wamejikita kushindana na polisi ambao kamwe hawatawaweza kwa kuwa askari wanatimiza majukumu...
Siasa za vyama vya upinzani ni zaidi ya Comedy! Siku zote walikuwa wakimtusi Dr Slaa kuwa alinunuliwa, alisaliti chama wakati muhimu na maneno kedekede ya kebehi, lakini mpaka jana mwenyezi Mungu alituonesha unafiki wa upinzani katika siasa zetu! Eti leo wanatuaminisha SUMAYE na LOWASA...
Mwenyekiti wa CUF Habari Prof Lipumba amesema wao wako tayari kushirikiana na vyama vingine vya upinzani kusimamisha mgombea mmoja wa urais.
Lipumba amesisitiza kuwa pamoja na yote hawatakuwa tayari kushirikiana na Chadema kama wanangojea makapi ya CCM waweze kupata mgombea.
Prof Lipumba...
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015, vyama vya upinzani hali yake ni mbaya sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Mpaka ninavyoandika hapa na kama hali ikiendelea hivi, Uchaguzi Mkuu wa 2020 upinzani utaambulia anguko kubwa na la aibu la kihistoria.
Ni anguko la kihistoria kwa sababu baada...
Habari!
Mimi napenda kuwauliza viongozi wa CHADEMA. Je, uamuzi wa haraka wa kuwapokea na kuwapa nafasi haraka viongozi hawa wanaolipwa na kulindwa na serikali mpaka kifo chao mliotoa wapi?
Kwanini mliwapa nafasi ndani ya CHADEMA haraka? Mliamini ikulu mtaingia kupitia hawa? Mlitaka kuongeza...
SUMAYE AREJEA RASMI CCM
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Februari 10, 2020 ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM)
Disemba 4, 2019 alitangaza kuachana na CHADEMA huku akidai alikosea kudhani kuna demokrasia ndani ya chama hicho.
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alijtoa CCM...
Msaanii Maarufu sana wa Filamu Nchini Tanzania Steve Nyerere ametangaza kumvua ubunge mchungaji Msigwa kwenye uchaguzi Mkuu utaofanyika mwishoni mwa mwaka huu, ametangaza kugombea jimbo la Iringa Mjini ili kulipa kisasi baada ya Mh Msigwa kumtaja bungeni kwa kuponda mipango ya Wizara ya mali...
Huu ni ukweli ulio wazi kwamba makamanda hawa wa zamani wa Chadema waliohamia CCM na kupewa shavu lakini bado kila siku wanaiota CHADEMA.
Na ndoto zao huwapeleka kwa Mbowe na Tundu Lisu respectively.
Niseme tu Dr Slaa na Juliana ni wanasiasa wa kweli unajua itikadi ni kama imani ya dini...
(Pichani kitabu kikianza kupatikana kwa Wabunge, Dodoma)
UPDATE:
Kuna watu wanaulizia jinsi ya kupata nakala ya kitabu cha "Nyuma ya Pazia" cha Balozi Dkt. Wilbrod Slaa. Sasa kinaweza kupatikana baadhi ya mikoa:
Mbeya Piga Simu: 0759829015
Arusha Piga Simu: 0716505921
Dodoma Piga Simu...
Hapa ndio mahali ambapo Nchi yetu na siasa zetu zilipofikia.
Tunamshukuru Mungu kwa kumlinda Mh Ibra dhidi ya wahalifu wanaolindwa ambao walimvamia alipotoka kwenye mgahawa kuelekea nyumbani kwake .
Mungu ibariki Chadema
=====
Ibrahim John Mwampwani diwani wa kata ya Isyesye Jijini Mbeya...
Nianze kwa kumpongeza sana Mh. Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA, kwa mambo mawili. Kwanza kitendo chake cha kuhudhuria sherehe za Uhuru mwezi Disemba, 2019 kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.
Pili kwa kitendo chake cha kumuandikia barua Mh. Dkt. John Pombe...
Vyama 12 vya upinzani nchini vimesema vitashiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu chini ya Tume ya uchaguzi iliyopo kwani wana imani nayo na pia wana imani na Rais Magufuli.
Makatibu wakuu wa vyama hivyo wakiongea na waandishi wa habari wamesema Mbowe na Chadema ni miongoni mwa waliosababisha...
Tumeshuhudia mara kadhaa mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani, hususan ya Chadema, ikizuiwa na Polisi, kwa maelezo kuwa kwa taarifa zao "walizozinusa" mikutano hiyo italeta machafuko na hivyo kusababisha hatari ya maafa.
Hata hivyo, mtumishi wa Mungu, anayejiita Mtume Boniface Mwamposa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.