Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Taifa wa CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji ajiunga na CCM

Nov 27, 2019
35
145

0DB5509E-EFCD-4967-B132-3BBB23C92622.jpeg

Kupitia matangazo ya moja kwa moja yanayoendelea ya channel 10, imemuonesha aliyekuwa Katibu Kkuu wa CHADEMA, Dkt. Mashinji akiingia ofisi hizo akiwa akiwa amevalia nguo za CHADEMA tayari kwa kuijiunga na CCM.

Anaeleza baada ya kutafakari kwa kina amebaini CHADEMA haina utayari wa kuleta maendeleo kwa wananchi tofauti na CCM ambayo imejizatiti.

Ameeleza CHADEMA inatumia muda mwingi kulumbana badala ya kuleta maendeleo wananchi, anaamini CCM ni chama sahihi ambacho kinaweza kumlea na kutoa mchango wake kwa Taifa.

Amemuomba mwenyekiti wa CCM Taifa. Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI kumpokea yuko tayari kwa ajili ya kulitumikia Taifa.

======

DKT MASHINJI ATIMKIA CCM!! Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji leo Februari 18 amefika ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi Lumumba jijini Dar es Salaam na kuomba kwa Mwenyekiti wa CCM taifa nafasi ya kujiunga na chama hicho.

A667BA65-B1E7-4DA6-8FC6-00CA5E23F215.jpeg

Zaidi, soma:
1). Dr. Mashinji Kuunga Mkono Utekelezaji wa Ilani ya CCM
2). Katibu Mkuu wa CHADEMA, Mashinji akanusha taarifa kuhusu kuhamia CCM
3). Lini Tulia Ackson alikuwa mwana CCM, na je lini Vicent Mashinji alikuwa mwana CHADEMA?
4). Ushauri wa bure: Dkt. Mashinji hamia CCM
5). Dkt. Vincent Mashinji: Viongozi tumeondoka kila mmoja na siri kubwa kichwani

WASIFU WAKE KWA UFUPI.

JINA: Dr.Vincent Mashingi

UMRI: Miaka 47
KABILA: Msukuma

TAALUMA: Daktari bingwa wa binadamu (MMED) na Daktari wa Falsafa (PhD).
ELIMU:

1981 - 1987 Elimu ya Msingi (Shule ya msingi Iligamba)

1988 - 1992 Elimu ya Sekondari (St.Pius seminary)

1992 - 1994 A-Level PCB (Mzumbe High School).

1995 - 2001 Chuo Kikuu cha Makerere (Degree ya Udaktari MD)

2003 - 2005 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Shahada ya pili - udaktari bingwa (MMED Anaesthesiology).

2004 - 2004 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Astashahada ya Utafiti)

2008 - 2010 Evin School of Management (Shahada ya Uzamili (Masters) ya Public Relations (CSR)

2007 - 2010 Blekinge Institute of Technology (Shahada ya pili (Masters) ya Usimamizi wa biashara, MBA)

2010-2010
University of Carlifonia - Anderson School (Stashahada ya Management Development)

2008 - 2008 University of Maryland School of Medicine (Astashahada Human Virology)

2010 - 2016 Chuo Kikuu Huria Tanzania (Shahada ya uzamivu (PHD) ya Uongozi.
UZOEFU WA KITAALUMA,

2001 2002, Daktari wa mazoezi - Intern doctor (Hospitali ya taifa Muhimbili).

2002 - 2003, Mtafiti wa kujitegemea (Freelance Researcher).

2003 - 2005, Daktari (Hospitali ya Taifa Muhimbili)

2005 - 2006, Daktari bingwa (Hospitali ya Regency).

2006 - 2008, Msimamizi wa mradi (Shirika la kimataifa la afya IMA World Health)

2008 - 2016, Mshauri wa tiba (TB and HIV), Shirika la afya la Kimataifa la IMA WorldHealth.

Ana degree 1, Masters 3, Certificate 2, Diploma 1 na PhD 1.

Machi 13 2016, Dk Vincent Mashinji alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Chadema akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Willibrod Slaa aliyeachana na chama hicho siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuuwa 2015.

Dk Mashinji alikuwa katibu mkuu wa nne wa Chadema tangu chama hicho kianzishwe maka 1992 baada ya Bob Makani, Dk Walid Aman Kabourou na Dk Slaa.

Alitumikia Chadema hadi Dec 19, 2019 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na John John Mnyika.
 
Tayari katangaza kuhamia CCM muda huu tuu
Kupitia matangazo ya moja kwa moja yanayoendelea ya channel 10, imemuonesha aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema Dk Mashinji akiingia ofisi hizo akiwa akiwa amevalia nguo za chadema tayari kwa kuijiunga na CCM.

Anaeleza baada ya kutafakari kwa kina amebaini CHADEMA haina utayari wa kuleta maendeleo kwa wananchi tofauti na CCM ambayo imejizatiti.
 
45 Reactions
Reply
Back
Top Bottom