Unyama: Diwani wa CHADEMA Mbeya Mjini anusurika kuuawa na watu wasiojulikana, apigwa panga la utosi, hakuna uchunguzi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,448
215,243
1580993993632.png

Hapa ndio mahali ambapo Nchi yetu na siasa zetu zilipofikia.

Tunamshukuru Mungu kwa kumlinda Mh Ibra dhidi ya wahalifu wanaolindwa ambao walimvamia alipotoka kwenye mgahawa kuelekea nyumbani kwake .

Mungu ibariki Chadema

=====

Ibrahim John Mwampwani diwani wa kata ya Isyesye Jijini Mbeya, amevamiwa saa nne na watu wanne wenye Mapanga na kukatwa sehemu za kichwani. Ameshonwa nyuzi 6, Alikuwa anatoka kwenye Shughuli zake za biashara.
 
POLE SANA.
Kauli za viongozi wa chama tawala na serikali ndizo zinazotufikisha hapa.

Kilichopo ni mtu kufanya alanaloliweza yeye mwenyewe kujikinga/kujilinda. Tukitegemea hii serikali itusaidie kwenye mambo yenye harufu ya siasa hasa ukiwa mpinzani wa CCM, hautapata msaada toka serikalini.
 
sisi kama polisi bado tunaendelea na uchunguzi, tukishathibitisha wahusika/muhusika watapelekwa mahakamani.
by~ OCD Mbeya mjini
 
Pole zake ila inawezekana wasiwe hao unao wadhania

Mbeya kwa sasa vibaka wengi sana

Wapo wanaoa pigwa ila kwa kuwa sauti yao haifiki kwenu kama ilivyo kwa viongozi wetu
 
amevamiwa na kupigwa panga kwa sababu ni diwani wa Chadema , hilo ndio kosa lake
watanzania mnakoelekea siyo kuzuri kwa kuzani kuwa viongozi wa chadema ni malaika hawana makosa katika jamii huyu kapigwa panga lakini kabla hata ya uchunguzi unakuja na uzi kuwa ccm ndiyo wamempiga je unauhakika gani? je kama alikuwa na visasi na watu wengine utajuaje acheni ujinga mnaotaka kuujaza kwa watu yatawarudia nyienyie je alikuwa kwenye kutano wa siasa? unajuaje kama humo kwenye mgahawa kama kazurumu mtu akawa anamfuatilia?acheni kabisa
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom