KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,600
Tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa 2015, vyama vya upinzani hali yake ni mbaya sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Mpaka ninavyoandika hapa na kama hali ikiendelea hivi, Uchaguzi Mkuu wa 2020 upinzani utaambulia anguko kubwa na la aibu la kihistoria.
Ni anguko la kihistoria kwa sababu baada ya hapo upinzani hautatamalaki tena katika ubora wake na sababu za kutotamalaki ni: CHADEMA pumzi imekata na itakata kabisa, ACT hakiaminiki na kitapoteza uaminifu kabisa na vyama vingine vitakosa mvuto. Kwa hali hii nani atashindana na CCM na akashinda?
Ambao wanafuatilia siasa za upinzani kwa karibu hasa za CHADEMA watakubaliana na mimi CHADEMA ya sasa siyo ile ya enzi zile, sio ile ya Balozi Dkt. Slaa, siyo ile ya hoja mkazo, siyo ile ya kuchakarika. CHADEMA ya sasa ni ya John Mnyika kijana aliyejificha kusaka fursa za kisiasa kwa maslahi yake binafsi, ni ya hoja nyepesi zisizo na mashiko wala uhalisia na hii ndio ishara ya kuonesha CHADEMA pumzi imekata. Haina pumzi ya kusimama tena mbele ya CCM.
CHADEMA imekimbiwa na kila mwanachama mwenye kujielewa na kila anayehama anatoa sababu zilezile ya kukubaliana na anayofanya Rais Magufuli na kutokubaliana na yanayoendelea CHADEMA. Ni yapi hayo? Kuna mengi ya kutaka kuyasikia kutoka huko ambayo yanakimbiwa? Je, ni suala la nafasi ya mwenyekti ambayo haiguswi na yeyote anayegusa anaambiwa usijaribu kuonja sumu kwa kulamba? Je, ni kuhusu kuhoji suala la ruzuku? Au ni ile sababu nyingine ambayo inasemwa sana?
Leo CHADEMA haipo kwenye ubora wake, CHADEMA imepoteza watu muhimu kama watu ambao wangekuwa kiungo muhimu kwa kujengea uwezo chama na wanachama wake. Mtu kama Sumaye ambaye angekuwa kiungo muhimu kuwafunda namna ya kuendesha chama na serikali kutokana na uzoefu wake hayupo tena, mtu kama Lowassa ambao wangewafunda uvumilivu na hekima katika siasa na uongozi hayupo, mtu kama Balozi Slaa ambaye angewafunda kujenga hoja nzito hayupo.
Kuksekana kwa watu kama hao ni ishara nyingine kubwa ya kukata pumzi kwa CHADEMA. Watu kama hao si wa kupatikana leo wala kesho ndani ya CHADEMA hasa ukizingatia watu hao wametokana na CCM. Je, watapambana vipi na CCM kama wanawategemea wanaCCM? CHADEMA bila wanaCCM pumzi inakata haraka na tumeona baada ya hao niliowataja kurudi CCM.
ACT na Zitto hawaaminiki wala hawakubaliki sana. Zitto anaonekana ni mtu asiye na misimamo linapokuja suala la kulinda na kutetea maslahi ya nchi yake. Ni msaka fursa kama ilivyo kwa Mnyika; anachokiangalia ni maslahi yake kulindwa kabla ya maslahi ya nchi.
Nasema maslahi yake kwa sababu ACT hakijababa maslahi yoyote kwa taifa na Zitto hajababa maaslahi ya ACT ila ACT ndio imebeba maslahi ya Zitto. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 Zitto kudhihirisha uchu wake ulivyo hatari. Kiongozi wa chama ambaye haaminiki yupo upande upi linapokuja suala la maslahi ya taifa, ataamikaje yeye na chama chake kupewa ridhaa ya kuongoza nchi yetu? Kwa ACT hii ya Zitto ndio inawaza kushindana na CCM kweli?
Ukiachana na CCM, ACT, CUF na CHADEMA ambavyo vina wanachama na mvuto kwa watanzania, vyama vingine havina mvuto kabisa. Ni vyama vya uchaguzi. Vinaibuka nyakati wa uchaguzi. Havina wagombea wakuwasimamisha kwa walau 20% kwa nafasi zote za uongozi.
Ni kama wanasubiri muujiza utokee lakini wanachoamini ni kimyume cha neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Mathayo 25:29 inasema ‘kwa maana kila mwenye kitu ataongezewa, naye atakuwa navyo kwa wingi. Lakini yule asiye na kitu hata kidogo alicho nacho atanyang’anywa. Ni vizuri watambue hilo.
Kwa mtazamo huu, kuna wa kushindana na CCM Uchaguzi Mkuu wa 2020 akashinda?