Viongozi wa CHADEMA mliwapokea Lowassa na Sumaye kwa ridhaa ya nani, na kwa manufaa ya nani?

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,934
Habari!

Mimi napenda kuwauliza viongozi wa CHADEMA. Je, uamuzi wa haraka wa kuwapokea na kuwapa nafasi haraka viongozi hawa wanaolipwa na kulindwa na serikali mpaka kifo chao mliotoa wapi?

Kwanini mliwapa nafasi ndani ya CHADEMA haraka? Mliamini ikulu mtaingia kupitia hawa? Mlitaka kuongeza ruzuku ndani ya chama mkiamini mtavuna wabunge wengi bila kujali matokeo ya mbeleni?

Je, mtakuwa tayari kuwaomba radhi wananchi kwa uamuzi wenu wa kukurupuka kwa kuwasajili Lowasa na wenzake ambao mliwaita mafisadi papa?

Niwawekee nukuu zenu za nyuma kuwakumbusha kuwa mnasahau haraka mnayoyasema majukwaani?

Je, mtakubali kuwa uwezo wenu wa kufanya reasoning ni mdogo na kwamba mna tatizo la akili?

Mwaka wa uchaguzi umefika, mtaletewa mamluki wengine; nanyi kwa tamaa ya pesa au uelewa mdogo mtawapokea kwa shangwe.
 
mbowe ashindwi kuchange gia angani tena mwaka huu Wa uchaghuzi na kisha kumwaga mwamba lisu
 
Hata CHADEMA au ACT kikiunda serikali bado viongozi uliowataja wataendelea kulipwa na kulindwa kwa mujibu wa Katiba yetu.

Mimi nadhani pamoja na Mh. Lowasa na Sumaye kurudi CCM bado wafaidika ni CHADEMA/UKAWA kwa maana ujio wao uliweza kuongeza idadi ya wabunge kwa upande wa vyama vya upinzani. Kwa uwiano wa wabunge kwa sasa sidhani kama wabunge wa CCM wanaweza kufanya mabadiliko ya katiba bila kupata uungwaji wa wenzao toka vyama vya upinzani.
 
Kwa kuwa CCM hawajawahi waomba radhi wananchi kwa umasikini uliokithiri kwa miaka 58 ya Uhuru.

Hivyo basi CHADEMA hawezi omba radhi wanachama kwa kutoa demokrasia ndani ya chama.
 
Mkuu lakini wabunge wakaunga juhudi hahahaha kazi tunayo.
Hata CHADEMA au ACT kikiunda serikali bado viongozi uliowataja wataendelea kulipwa na kulindwa kwa mujibu wa Katiba yetu.

Mimi nadhani pamoja na Mh. Lowasa na Sumaye kurudi CCM bado wafaidika ni CHADEMA/UKAWA kwa maana ujio wao uliweza kuongeza idadi ya wabunge kwa upande wa vyama vya upinzani. Kwa uwiano wa wabunge kwa sasa sidhani kama wabunge wa CCM wanaweza kufanya mabadiliko ya katiba bila kupata uungwaji wa wenzao toka vyama vya upinzani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ulitaka wapate ridhaa ya nani?.Kwani uyo lowasa na sumaye sio watanzania. na kama ni lowasa kura si alipata, swala lakushinda ilo ni jambo jingine kwasababu uchaguzi ni mchakato na ndo maana bado chaguzi zitaendelea kuwepo.Wewe ndiye ambaye unaona viongoz wa CDM walikosea kwasababu uangalii mambo kwa mapana.
 
Chadema walifaidika sana na ujio wa Lowassa,viti vingi vya ubunge, udiwani,walivyopata Chadema ilikua sababu ya Lowassa!

Lowassa alikua ni mtaji,hata kura zake Milioni sita alizozipata usitegemee zitapatikana kirahisi kwenye chaguzi zinazokuja!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chadema hawakumpokea Lowasa Wala Sumaye.Wao walipokea pesa ya Lowasa ,Sumaye na washirika wao.
Hawakuwa interested na Lowasa Wala Sumaye .Interest yao ilikuwa kwenye pesa zao na za washirika wao na wapenzi wao wao wa ndani na nje ya nchi na mitandaoni yao

Niseme wazi kwa Hilo chadema walifanikiwa Sana na walizivuna pesa Sana sio.mchezo .Lengo la kuu la Kwanza lilikuwa kuvuna pesa hilo.la Sijui ushindi.kwao lilikuwa sio issue Sana
Lowasa na Sumaye na washirika wao kwa kweli pesa nyingi mno wamepoteza hata Kama waliziiba wakiwa viongozi asilimia kubwa walishazirudisha kea kuliwa na chadema .Wamebaoi tinna hela za kawaida za kuwasulima tu wamalizie kipindi Cha uhai kilichobaki

Sumaye kawajengea hadi.makao.makuu ya Kanda mazuri ajabu Lakini hakujua maskini kuwa wameudhika kuwa anawaona wajinga kutojenga makao.makuu.Ile pesa aliyoijengea iliwauma walikuwa wanaitaka wapewe cash waile

Kifupi chadema Ni matapeli scammers kulikonwa Nigeria.Kama una pesa ukijitosa chadema jiandae kufilisika wataila pesa yako Kama mchwa ikiisha unasnza kuporomoshewa matusi Kama ambavyo Lowasa na Sumaye wamefanyiwa

Nyalandu kaa chonjo huko
 
Mimi napenda kuwauliza viongozi wa CHADEMA. Je, uamuzi wa haraka wa kuwapokea na kuwapa nafasi haraka viongozi hawa wanaolipwa na kulindwa na serikali mpaka kifo chao mliotoa wapi?
Ni wale milioni sita+ waliotoa kura zao kwa UKAWA
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom