Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
873
1,000
photo_2020-02-10_12-47-51.jpg


SUMAYE AREJEA RASMI CCM

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Februari 10, 2020 ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM)

Disemba 4, 2019 alitangaza kuachana na CHADEMA huku akidai alikosea kudhani kuna demokrasia ndani ya chama hicho.

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye alijtoa CCM mwaka 2015 ambapo alitangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuungana Waziri Mkuu wa awamu ya nne, Edward lowassa.

Sumaye alisema kuwa alifikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na uvunjaji wa kanuni ikiwemo katika harakati za kumteua mgombea wa Urais kwa upande wa CCM akidai Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete alitumia ubabe katika kuwaingiza watu wake "tano bora"

Akiwa ndani ya ukumbi, Mzee Sumaye aliyeonekana amesimama akizungumza akiwa karibu na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally, amesema:

"Mimi nimekaa ndani ya CCM kwa kuanzia TANU, niliingia chama wakati ule kama TANU Youth League nikiwa sekondari, na nilipomaliza tu nikaingia kuwa mwanachama wa TANU na baadaye kuwa mmojawapo wa wanachama waanzilishi wa CCM. Nimedumu ndani ya chama kwa muda mrefu nikaingia bungeni, kabla ya bungeni nilishika nafasi nyingi za uongozi katika CCM"


 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom