CHADEMA kwa muda mrefu sasa haijapokea madiwani wala wabunge kutoka vyama vingine. Je, haipendwi?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,886
141,818
Najiuliza tu maana tangia wamchukue Lazaro Nyalandu kutoka CCM hawa jamaa wa CHADEMA hawajapokea diwani wala Mbunge tena kutoka chama tofauti.

CCM wao karibia kila mwezi wanapokea madiwani kutoka vyama vya upinzani wanaojiunga nacho kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Je, CHADEMA kimepoteza mvuto au wanawapokea kimya kimya?

Maendeleo hayana vyama!
 
Sisi hatununui watu. Hao mnaofurahia kuwanunua ni sawa na kujilisha upepo kwani hawana mapenzi ya dhati na CCM bali wamefuata maslahi binafsi. Hivi ukienda Corner Bar ukichukua demu utasema umepata mpenzi?
 
Hivi Sumaye na Lowassa wanaipenda CCM au wame rudi kutetea Maslahi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamerudi kujiunga na majizi wenzao ili wapige pigo la mwisho kwani wanajua kuwa mwisho wao umefika
FB_IMG_1581491063368.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo diwani au mbunge atakae thubutu kuiacha CCM wakati huu tukielekea uchaguzi mkuu tena chini ya utawala huu tulionao aende upinzani ndie atakuwa mzalendo wa dhati kwa taifa, kwasababu anajua kabisa chances zake za kushinda ni ndogo ila ataamua kuwa upande wa haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najiuliza tu maana tangia wamchukue Lazaro Nyalandu kutoka CCM hawa jamaa wa CHADEMA hawajapokea diwani wala Mbunge tena kutoka chama tofauti.

CCM wao karibia kila mwezi wanapokea madiwani kutoka vyama vya upinzani wanaojiunga nacho kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Je, CHADEMA kimepoteza mvuto au wanawapokea kimya kimya?

Maendeleo hayana vyama!
Usishangilie, unakuja utaratibu wa Kambale, utaratibu ambao mara nyingi huzaa machafuko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom