Featured content

Rais Samia: Tanzania haiko kwenye Vikwazo vyovyote
Rais Samia Suluhu amesema Tanzania haiko kwenye vikwazo vya kimataifa (sanctions) na kwamba Serikali inaendelea kujipanga kuharakisha maendeleo ya nchi. Akijibu swali kuhusu madai ya kuwepo kwa vikwazo dhidi ya Tanzania, alisisitiza kuwa hakuna hatua zozote za aina hiyo zinazoikabili nchi kwa sasa. Kauli hiyo ameitoa wakati akiwa na Rais wa Urusi, Vladimir Putin, katika Kongamano la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg (SPIEF’26) lililofanyika St. Petersburg, Urusi, tarehe 5 Juni 2026
Nchimbi: Rais Samia amekwenda kuliwakilisha Taifa Urusi na Mamlaka ya Urais amenikabidhi
Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi amesema Rais Samia Suluhu amekwenda Urusi kuliwakilisha Taifa, huku mamlaka ya urais yakikabidhiwa kwake kwa mujibu wa Katiba. Kauli hiyo ameitoa Juni 5, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma. Nchimbi amesema waandaaji walitamani Rais Samia awe mgeni rasmi wa tukio hilo kutokana na umuhimu wake, lakini ratiba zake za kitaifa na kimataifa zilifanya isiwezekane kushiriki.
Ufafanuzi wa Serikali kuhusu Kura ya Kamati za Bunge la Ulaya (EU) dhidi ya Tanzania
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema kura iliyopigwa katika Kamati ya Mambo ya Nje na Kamati ya Maendeleo ya Bunge la Ulaya kuhusu Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania bado si uamuzi wa mwisho. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 3, Wizara imefafanua kuwa mchakato huo bado unaendelea na mapendekezo hayo yanapaswa kuwasilishwa kwenye kikao cha Bunge zima la Ulaya kwa ajili ya mjadala na maamuzi ya mwisho mwezi huu.
Bunge la Ulaya (EU) lapinga Msaada wa Euro Milioni 156 (Tsh. Bilioni 440+) kwa Tanzania
Bunge la Umoja wa Ulaya (European Parliament) limepiga kura ya kupinga mpango wa Kamisheni ya Umoja huo wa kuipatia Tanzania msaada wa kimaendeleo wa Euro milioni 156 (zaidi ya Tsh. Bilioni 440). Hatua hiyo inakuja kufuatia ripoti ya jarida la Euractiv ya Juni 3, 2026, ikieleza kuwa wabunge hao wanaituhumu Kamisheni kwa kutaka kutoa fedha hizo bila kuweka masharti madhubuti ya kulinda haki za binadamu.
Mwigulu: Nchi iko salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola, tuzingatie tunayoelezwa na wataalam
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa nchi bado iko salama dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoripotiwa katika baadhi ya nchi za Afrika na serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo na kuchukua hatua za tahadhari ili kulinda afya ya wananchi. Mwigulu ameeleza kuwa kutokana na mahusiano ya karibu ya kijamii na kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa jirani, pamoja na ukweli kwamba Tanzania si kisiwa, ipo haja ya wananchi kuendelea kuwa waangalifu.
Zungu: Wabunge walioenda Morocco bila kibali wajieleze, kuna utoro umekithiri Bungeni
Spika wa Bunge, Mussa Zungu, ameonya vikali wabunge wanaojihusisha na utoro, akieleza kuwa baadhi yao wamekuwa wakifika asubuhi na jioni kwa ajili ya kuthibitisha mahudhurio pekee (verify) kisha kuondoka, huku wengine wakisainiwa na wenzao ili kuonekana wapo bungeni ilhali hawapo. Zungu amesisitiza kuwa wabunge wote wanaohusika na vitendo hivyo, ikiwemo wanaowasainia wenzao, watakabiliwa na hatua kali za kikanuni na kisheria.
Siasa za kumtaja na kumsifia Rais kila mahali hadi kwenye michezo zinaisaidiaje nchi?
Nimeshangaa kwenye mechi ya Serengeti boys na Senegal watu wanaimba nyimbo za kumsifia mama! Upande wa Senegal hawakuwa wakimuimba Rais wao Faye na wameshinda, Kenya huwa wanafanya vizuri sana kwenye michezo mingi duniani lakini huwezi kusikia wakiimba nyumba za kumsifu Uhuru au Ruto, DRC Congo pamoja na kuwa wanafanya vizuri zaidi kuliko sisi sijawahi kusikia wakiingiza siasa za kusifia watawala viwanjani, Timu za Africa zitakazocheza kombe la dunia huwezi kuona haya mambo. Kwa nini...
Asha-Rose Migiro: Sioni Sababu Watu kutoka Nje waje Watuamulie Mambo yetu ya Ndani
Katika mahojiano na Salim Kikeke wa Crown Media, Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amesema haoni sababu ya kuleta wataalamu au vyombo kutoka nje kuchunguza masuala ya ndani ya nchi, akisisitiza kuwa miaka 65 ya uhuru Tanzania ina weledi, uzoefu na watu wenye uwezo mkubwa wa kujiamulia mambo yake yenyewe.
Peter Msigwa: Nilipokuwa CHADEMA nilikuwa Mjinga
Mwanachama mpya CCM akitokea Upinzani, Mchungaji Peter Msigwa, amesema wakati alipokuwa CHADEMA hakuwa na ufahamu kwamba Mchakato wa Katiba Mpya ulikuwa unakwamishwa na baadhi ya Viongozi wa CHADEMA lakini amelijua hilo baada ya kujiunga na CCM. Alipoulziwa na Mtangazaji wa Kipindi cha Medani za Siasa cha StarTv, Edwin Odemba, kwamba alikuwa Mjinga akiwa CHADEMA, Mchungaji Msigwa amejibu "Ndio, kuna kipindi nilikuwa sina ufahamu nimeongezewa ufahamu nilikuwa napigania vitu ambavyo havipo"...
Mafao wanayopata wenza wa viongozi wakuu wastaafu ni kufuru
Tanzania = Tanganyika + Zanzibar 🙏 • Mke wa Mwl, Julius K. Nyerere, Maria Nyerere. • Wake wa Ali H. Mwinyi, Sitti na Khadija Mwinyi. • Mke wa Benjamin W. Mkapa, Anna Mkapa • Mke wa Jakaya M. Kikwete, Salma Kikwete • Mke wa John P. Magufuli, Janeth Magufuli • Mume wa Samia S. Hassan, Hafidh Ameir Kwa mujibu wa The Political Service Retirement Benefits Act [CAP. 225] kila mwezi hawa watalipwa 60% ya mshahara wa Rais aliyepo madarakani. Kama Rais aliyepo madarakani anapokea TZS 50,000,000...
Mafwele azuiwa kuingia Marekani. Ahusishwa na Utekaji, ukiukwaji wa haki za binadamu
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imemtaja Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania (TPF), Faustine Jackson Mafwele, chini ya Kifungu cha 7031(c), ikisema kuna taarifa za kuaminika zinazomhusisha na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Uamuzi huo unamzuia Mafwele kuingia nchini Marekani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwaka mmoja uliopita baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi Tanzania waliwakamata, kuwatesa na kuwafanyia ukatili wa kingono mwanaharakati wa Uganda Agather...
CHADEMA: Msaidizi wa Lissu amepatikana, aliwatoroka watekaji akiwa na pingu mkononi
Picha zikionyesha Msaidizi wa TUNDU LISSU akiwa ameumizwa vibaya na watekaji usiku wa kuamkia leo. David Djumbe alitekwa siku ya Jana Maeneo ya Bunju akiwa na rafiki yake wakati wa kutekwa alipiga kelele sana bodaboda wakafukuzia GARI kwa nyuma Walipofika umbali wa kilometa kama 3 watekaji walipoona bodaboda bado wanafuatilia GARI, watekaji walishuka na kuanza kupiga RISASI wakati huo Djumbe wakiwa wamemuacha ndani ya GARI. Soma Pia: David Djumbe (Msaidizi wa Lissu) adaiwa kutekwa Ndio...
David Djumbe (Msaidizi wa Lissu) atekwa
Msaidizi wa Tundu Lissu, David Djumbe inadaiwa ametekwa usiku huu na wanaodhaniwa kuwa Maafisa wa Usalama wa Taifa ambao walikuwa na silaha za moto. Djumbe ametekwa akiwa nje ya geti la nyumbani kwake, maeneo ya Bunju Dar es Salaam. Wananchi waliokuwa wanalikimbiza gari hilo lililomteka, wamesema wameliona likiingia kwenye nyumba za Usalama wa Taifa zilizo maeneo ya Mbweni. ===== https://www.instagram.com/p/DYkyDomueV1/?igsh=cTBocm1sa2g1M2Z0 ======================...
CHADEMA yamjibu Msajili: Ofisi yako siyo Mahakama, kukosoa Serikali na Uchaguzi siyo Uasi
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejibu barua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kikikataa tuhuma zote za ukiukwaji wa Sheria na kuzitaja kama mkakati wa Kisiasa wa kukandamiza upinzani. CHADEMA imesema mamlaka ya kuamua makosa ya jinai, kashfa, au uchochezi ni jukumu la Mahakama pekee, na hatua ya Msajili kujigeuza mwamuzi wa kauli za Kisiasa ni uingiliaji wa muhimili, huku chama kikigomea tishio lolote la kufutiwa usajili au kutozwa faini.
Maduhu: Kwa kauli za Chatanda, nategemea Msajili ataiandikia barua CCM kuionya au kuifuta
Wakili wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), William Maduhu, amesema anategemea kuona Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikiandikia barua Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuionya au kuchukua hatua madhubuti dhidi ya kauli zilizotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa chama hicho Taifa (UWT), Mary Chatanda.
Arsenal yatwaa ubingwa EPL msimu wa 2025/26
Arsenal wameandika historia mpya kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England (EPL) msimu wa 2025/26 baada ya kusubiri kwa miaka 22. Ubingwa huo unafuatia baada ya Manchester City kwenda sare ya 1-1 dhidi ya Bournemouth katika mchezo uliomalizika usiku wa Mei 19, 2026.
Tanzania yapangwa Kundi L, ipo na Nigeria, Guinea-Bissau, Madagascar AFCON 2027
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limefanya droo rasmi ya upangaji wa makundi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, ambapo Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imepangwa katika Kundi L pamoja na timu za taifa za Nigeria, Madagascar na Guinea-Bissau.
Neymar arejea Kikosi cha Brazil kwa Kombe la Dunia 2026!
Neymar amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 26 cha Timu ya Taifa ya Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia 2026. Nyota huyo anarejea rasmi kuiongoza timu ya taifa baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipocheza mechi yake ya mwisho. Kocha Carlo Ancelotti amemtaja Neymar baada ya kurejea katika kiwango bora na Klabu ya Santos.
Rais Samia aunda Tume ya Uchunguzi wa Kijinai Ghasia za Uchaguzi Mwaka 2025
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shabani Ally Lila kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Kijinai wa Matukio ya ghasia ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Tume hiyo inalenga kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani ili kuchukua hatua stahiki na kuimarisha usalama wa Taifa.
Hakikisha mwenye nyumba anakupa funguo zote, nimemkuta ndani wakati niliacha mlango umefungwa
Mdau amesema baada ya kurudi nyumbani, alimemkuta mwenye nyumba wake akiwa ndani ya nyumba aliyopanga bila ridhaa yake, na cha kushangaza hata baada ya kuniona hakushtuka, mpaka sasa sijui alikuwa na lengo gani. Amesema hakukuwa na ukarabati wala sababu yoyote ya msingi ya kuingia ndani, tena bila ridhaa yangu. Hakikisha kwenye hiyo nyumba unayoenda kupanga, au umepanga unapewa funguo zako zote kama ni tatu, ni tatu, zote au ubadilishe kitasa kabisa.
Back
Top Bottom