Featured content

Mabadiliko ya Kanuni za BoT (GN No. 206, 2026): Fursa au Mtego wa Kifedha kwa Tanzania?
Wakuu, nadhani mmeona Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia barua ya Agosti 6, 2026, ikizungumzia Maboresho ya Kanuni za Fedha za Kigeni kupitia Tangazo la Serikali (GN) Na. 206 la mwaka 2026 (Foreign Exchange (Amendment) Regulations, 2026). Suala hili limenivutia sana kutaka kulijua kwa undani: Uamuzi huu unamaanisha nini, una faida gani, na una hatari gani kwa uchumi wetu? Hatua hii ya BoT kuwaruhusu wawekezaji wote wa kigeni (wasio wakazi) kununua Hatifungani (Treasury Bonds)...
Heche: Kosa ambalo tumewahi kulifanya CHADEMA ni kuwaamini Watu wasioaminika
John Heche anasema anasema moja ya makosa ambayo wamewahi kuyafanya ni kuwaamini watu wasioaminika, anasema waliwaamini CCM kwenye maridhiano a Mbowe na kumbe ulikuwa ni ulaghai tu na kosa lingine ni kuwaamini CCM kwenye katiba mppya wakati ule wa mchakato bungeni na baada ya hapo CCM kupitia Rais Kikwete akawazunguka na kuongeza watu wa CCM kupita NGOs hali ambayo ikaongeza nguvu na kushindwa kuwapa watanzania katiba
Wafungua kesi wakitaka Mawakili 399 waondolewe katika orodha ya Mawakili
Je, kuwa na Shahada ya Sheria na kufanya kazi kwenye mazingira ya sheria ni sawa na kuwa na mafunzo maalumu yanayomwandaa mtu kuwa Wakili? Hili ni moja ya maswali makubwa ambayo mimi na wenzangu wengine wanne katika shauri hili tumeamua kulipeleka mbele ya Mahakama Kuu ya Tanzania. Tarehe 30 Julai 2026, tuliwasilisha shauri la kikatiba kuhusu namna kifungu cha 16(2) cha Sheria ya Mawakili kinavyotumika kutoa msamaha (exemption) kwa baadhi ya watu kutopitia mafunzo ya kitaaluma ya Law...
Tanzania yashuka kwa nafasi 20 katika orodha ya Nchi zenye amani zaidi Duniani
Ripoti ya Global Peace Index 2026 imeiweka Tanzania katika nafasi ya 98 kati ya nchi 163, ikiwa imeshuka nafasi 20, huku kiwango cha amani kikishuka kwa 7.3%. Ripoti hiyo inataja Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kuwa miongoni mwa sababu kuu za kushuka kwa Tanzania, huku Umoja wa Afrika ukisema uchaguzi huo haukuzingatia viwango vya uchaguzi wa kidemokrasia.
Mahakama yaamua Uchaguzi Mkuu Kenya unapaswa kufanyika Agosti 2026 na si Agosti 2027
Mahakama ya Malindi imeamua kuwa Uchaguzi Mkuu ujao wa Kenya unapaswa kufanyika Jumanne, Agosti 11, 2026, badala ya mwaka 2027. Hata hivyo, Jaji Mugure Thande amesitisha utekelezaji wa uamuzi huo hadi baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2027, akisema kufanyika kwa uchaguzi huo nje ya Agosti 2026 kutakiuka Katiba.
NAMIBIA | Chama cha AR chapinga uteuzi wa Jaji Damaseb kuwa Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Jinai
Chama cha upinzani cha Namibia, Affirmative Repositioning (AR), kimepinga uteuzi wa Naibu Jaji Mkuu, Petrus Tileinge Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume ya Rais ya Uchunguzi nchini Tanzania, kikisema unaweza kuhatarisha uhuru wa mahakama ya Namibia. Katika taarifa ya Agosti 6, 2026, AR imedai uteuzi huo ulifuatia ombi la serikali ya Tanzania baada ya ziara ya Rais Netumbo Nandi-Ndaitwah, ikisisitiza kuwa taratibu za kawaida za mahakama hazikufuatwa.
Tanzania yashika Namba 2 kwenye nchi ambazo Uhuru wa Raia umeshuka zaidi Duniani
Tanzania imeshika nafasi ya pili duniani kwa kuporomoka zaidi katika masuala ya haki za kisiasa na uhuru wa raia kwa mwaka 2025, kulingana na ripoti mpya ya shirika la kimataifa la Freedom House. Katika ripoti hiyo inayoitwa Freedom in the World 2026: The Growing Shadow of Autocracy, Tanzania imeshuka kwa alama saba (7) na kuzama zaidi kwenye kundi la nchi "Zisizo Huru" (Not Free) Matokeo haya yanaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili duniani kwa kuporomoka zaidi kwa viwango vya uhuru kwa...
Rais Samia: Tume imeshirikisha Majaji kutoka Uganda, Namibia ili kutafuta waliohusika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 07, 2026, amezindua rasmi Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Wahusika wa Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria katika Matukio ya Ghasia wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais Samia amebainisha kuwa ameunda tume hiyo kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32). Tume hiyo inakwenda kufanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika, waliotoa...
Kenya yapendekeza kufuta mfumo wa Ufadhili wa Masomo ya Vyuo Vikuu
Serikali imependekeza mageuzi makubwa katika mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu kwa kufuta mfumo wa sasa wa ufadhili wa masomo (scholarships na grants) na kuubadilisha na mfumo ambapo wanafunzi wote watakaodahiliwa katika vyuo vikuu na taasisi za umma watapata mikopo badala ya ruzuku. Pendekezo hilo liko mbele ya Bunge kupitia mswada mpya unaolenga kurekebisha mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu. Chini ya mfumo unaopendekezwa, wanafunzi watastahili kupata mkopo utakaogharamia ada na gharama...
Polisi: Dereva wa Pikipiki Simiyu alizuiwa kupisha Msafara wa Mwenge lakini alikaidi
Jeshi la Polisi Tanzania, lingependa kutoa ufafanuzi juu ya picha mjongeo inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha Dereva wa Pikipiki akizozana na Askari Polisi huku askari hao wakijitahidi kuyaondoa barabarani magunia ya alizeti aliyokuwa amebeba dereva huyo kwenye pikipiki. Tukio hilo lilitokea Julai 30,2026 Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu. Askari hao walikuwa wanapitisha msafara wa Mwenge wa Uhuru ndipo Dereva huyo wa pikipiki alisimamishwa kwa ajili ya usalama wake na wa watu...
EWURA yashusha bei za mafuta mwezi Agosti, hali ya nauli ikoje mtaani?
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza rasmi bei mpya kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli nchini, zikionyesha nafuu kubwa kwa wananchi kuanzia LEO Jumatano, Tarehe 05 Agosti 2026 saa 6:01 usiku. Katika mabadiliko hayo ya mwezi Agosti, bei za mafuta zimeshuka nchinzima kutokana na mwenendo wa bei katika soko la dunia: Petroli: Imeshuka kwa TZS 92 kwa kila lita. Dizeli: Imeshuka kwa TZS 204 kwa kila lita. Mafuta ya Taa: Yameshuka kwa TZS 440 kwa kila lita.
Kesi ya Ugaidi ya Mhadhiri wa UDOM yaahirishwa hadi Agosti 19, 2026
Shauri la ugaidi linalomkabili mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk. Melikisedeki Kaijage, limeahirishwa hadi Agosti 19, 2026 baada ya kutajwa leo, Agosti 5, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma. Shauri hilo lilitajwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Zabibu Mpangule, ambapo ilielezwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kulisikiliza. Badala yake, jukumu lake ni kuhakikisha taratibu za awali, ikiwemo ukamilishaji wa faili la shauri, zinakamilika kabla ya kesi kupelekwa katika mahakamani
Dkt. Koshuma: Kukaanga chapati kwa vipande vya Godoro kunaweza kuingiza kemikali kwenye chakula
Daktari mstaafu wa magonjwa ya ndani, aliyewahi kufanya kazi katika kitu cha afya kikubwa mkoani Dar es Salaam, Kituo cha Afya Sinza Dar es Salaam Dk. Phoibe Koshuma, anasema magodoro ya kisasa yanatengenezwa kwa povu la anachokitaja kwa jina ‘polyurethane’ ambayo ni aina ya plastiki laini yenye chembe nyingi za hewa ndani yake.
Tozo za Daraja la Mwalimu Nyerere (Kigamboni) zitaendelea hadi mwaka 2046
Daraja la Mwalimu Nyerere halikujengwa kwa mkopo wa kawaida wa Serikali. Lilijengwa kupitia mkataba wa aina ya DBFOT, ambapo Serikali ilichangia asilimia 40 ya gharama za mradi na NSSF asilimia 60. Serikali ilikubaliana kuirejeshea NSSF sehemu yake ya gharama, kwa kuendesha daraja la Mwalimu Nyerere na kukusanya tozo kwa miaka 30 ili kurejesha uwekezaji wake kabla ya kukabidhi daraja kwa Serikali baada ya kurejesha gharama.
Rais Samia: Misaada na Mikopo nafuu tuliyoizoea inaendelea kuondoka, tukaze Buti
Rais Samia Suluhu, amewataka Watanzania na viongozi kukaza buti na kufunga mikanda kutokana na mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa yanayoendelea duniani, amesema hayo Agosti 3, 2026 katika uzindizi wa Nyenzo za Utekelezaji wa Dira 2050 pamoja na kushiriki katika Mkutano wa Mazungumzo Maalum na Sekta Binafsi kuhusu Utekelezaji wa Dira 2050, Agosti 03, 2026 ''Misaada na mikopo tuliyo izoea inaendelea kuondoka tukaze buti "
Mnyika: Kauli ya Rais kuhusu 'Mwenzetu Kutafakari' haituhusu CHADEMA
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mnyika amesema kuwa chama hicho na Mwenyekiti wake Tundu Lissu mpaka hivi sasa hakijafanya mazungumzo yoyote na serikali huku akiipinga kauli iliyotolewa na Rais Samia Julai 30, 2026. Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari leo Agosti 3, 2026 ameeleza kauli ya Rais Samia alipokuwa akizungumza na vyama vya siasa kuwa yupo mwenzao mmoja ambaye anaendelea kutafakari masharti haikihusu CHADEMA.
Mkuu wa Polisi na Afisa wa Ulinzi wa zamani Sri Lanka wahukumiwa kifo kwa mashambulizi ya 2019
Mahakama Maalum (Permanent Trial-at-Bar) imewakuta na hatia aliyekuwa Mkuu wa Polisi nchini Sri Lanka, Pujith Jayasundara, na aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Ulinzi, Hemasiri Fernando, na kuwahukumu adhabu ya kifo kwa kushindwa kuzuia mashambulizi ya mabomu ya Pasaka 2019 yaliyosababisha vifo vya Watu 279.
Ado: Ukifunga Mlango wa Demokrasia, unafungua mlango wa machafuko
Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, amesema maridhiano ya kisiasa hayawezi kufanikiwa bila kuwepo kwa ukweli na uwajibikaji kuhusu matukio ya kisiasa yaliyotokea nchini. Amesema hatua ya kwanza katika mchakato wa maridhiano ni kuweka wazi ukweli kuhusu matukio yaliyojitokeza kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa mwaka 2025 akidai kuwa kipindi hicho kilizalisha wafungwa wa kisiasa, watu waliotekwa na wengine kuuawa.
Mrindoko: Polisi wanakukamata wanasema wameagizwa, ukiuliza kosa, wanajibu "Utajulia mbele"
Joseph Mrindoko wa Wachokonozi amesema kuna changamoto katika utawala wa sheria, utendaji wa baadhi ya watumishi wa serikali na uelewa wa wananchi kuhusu haki zao za kisheria. Amesema baadhi ya Watanzania huamini kuwa mtu anapohojiwa au kushikiliwa na polisi tayari ana hatia, badala ya kutambua kuwa anaweza kuwa anachunguzwa au anatuhumiwa bila hatia kuthibitishwa.
Serikali ya Ghana yaongeza Muhula wa rais na wabunge kutoka miaka 4 hadi 5
Serikali ya Ghana imekubali pendekezo la kuongeza muda wa muhula wa urais kutoka miaka minne hadi mitano, Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Dr. Dominic Akuritinga Ayine Rais John Dramani Mahama aliunda kamati mwaka 2025 kupitia upya Katiba ya mwaka 1992 na kutoa mapendekezo mbalimbali, ambapo baadhi yake yamekubaliwa na serikali. Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria, Dominic Ayine, amesema pia muda wa Bunge utaongezwa ili uendane na muhula mpya wa rais...
Back
Top Bottom