Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,911
- 16,510
Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, amesema kuwa nchi bado iko salama dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoripotiwa katika baadhi ya nchi za Afrika. Akijibu swali la Mbunge Asha Moto wakati wa kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo Bungeni Juni 4, 2026 Waziri Mkuu amesema serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo na kuchukua hatua za tahadhari ili kulinda afya ya wananchi.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa kutokana na mahusiano ya karibu ya kijamii na kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa jirani, pamoja na ukweli kwamba Tanzania si kisiwa, ipo haja ya wananchi kuendelea kuwa waangalifu.
Alibainisha kuwa milipuko ya magonjwa kama Ebola inaweza kutokea katika nchi yoyote, hivyo serikali imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kujikinga.