Wakuu,
Kuna mvutano mzito unaoendelea huko Ulaya kati ya Bunge la Umoja wa Ulaya (European Parliament) na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (European Commission) kuhusu mpango wa kuipatia Tanzania msaada wa kimaendeleo wa kiasi cha Euro Milioni 156 (zaidi ya Tsh. Bilioni 440).
Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la Euractiv leo Juni 3, 2026, Wabunge wa Ulaya wameungana kupinga vikali kutolewa kwa fedha hizo kwa sasa. Wameituhumu Kamisheni ya Ulaya kwa kutaka kutoa fedha hizo bila kuweka masharti madhubuti ya kulinda haki za binadamu.
Mambo Muhimu Yaliyojitokeza Kwenye Sakata Hili:
Je, mnadhani hatua hii ya Wabunge wa Ulaya itakuwa na msaada wowote kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa inayoendelea nchini baada ya Uchaguzi wa 2025?

- Vurugu na Vifo vya Baada ya Uchaguzi (Oktoba 2025): Wabunge wa EU wameibua hoja nzito kuhusu ukandamizaji wa maandamano kufuatia uchaguzi mkuu uliopita wa Oktoba 2025. Kwenye taarifa yao, wanadai kuwa zaidi ya watu 500 walipoteza maisha kwenye vurugu hizo.
- Kufungwa kwa Tundu Lissu: Bunge hilo limehoji kuendelea kuswekwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu. Wabunge hawa (wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, David McAllister) wanadai mashtaka anayokabiliwa nayo ni ya kisiasa.
- Mvutano wa 'Nani Asimamie Fedha Hizo?': Awali, msaada huu ulisitishwa mwaka jana baada ya Bunge kupiga kelele. Ili kutatua hili, Kamisheni ya Ulaya ikapendekeza kuwa fedha hizo zisimamiwe nje ya udhibiti wa moja kwa moja wa Serikali ya Tanzania. Hata hivyo, Wabunge bado wamekataa wakisema mpango huo hauna masharti ya kutosha (meaningful conditionality) na hauoneshi hatua stahiki endapo hali ya Haki za Binadamu zitazidi kudorora.
- Kuzuiwa kwa Ziara ya Wabunge wa EU: Inaelezwa kuwa Mei mwaka huu (2026), Tanzania iliahirisha ziara iliyokuwa imepangwa ya Wabunge wa EU kutoka kamati ndogo ya Haki za Binadamu. Hatua hii imewakasirisha zaidi Wabunge hao wanaodai Tanzania haioneshi utayari wa kufanya mazungumzo.
Je, mnadhani hatua hii ya Wabunge wa Ulaya itakuwa na msaada wowote kwa kuzingatia hali halisi ya kisiasa inayoendelea nchini baada ya Uchaguzi wa 2025?
- Mpango wa Kamisheni ya Ulaya kutaka kutoa fedha hizo lakini nje ya udhibiti wa Serikali, mnauonaje kiusalama na kidiplomasia? Je, ni dharau kwa 'mamlaka ya nchi' (wazee wa 'sisi ni nchi huru' hapa najua wataibuka) au ni tahadhari ya wafadhili?
- Kama msaada huu wa Tsh. Bilioni 440+ ukikwama jumla, mnadhani sekta zipi za kimaendeleo zitaathirika zaidi?